Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Tatizo lako Mohamed ni kudhani kuwa wewe unaelewa sana kuliko waislam wengine wa Tanzania. Nimeeleza kuwa angalia nani anashangilia na anashangilia nini. Je, anajua anachokishangilia na yupo tayari kukitetea kwa hoja kile anachoshangilia
Nguruvu3,
Si wewe wa kutuuliza sisi Waislam swali hilo. Sisi hatukutuhumu wewe kwa lolote. Mimi hapa jamvini nimejitahidi kueleza hali ya mambo ilivyo nchini kwetu kwa kutegemea kuwa wengi watakapolijua hili tatizo ndiyo nji ya kwanza ya kutafuta suluhisho.
Wengi kama nawe unavyoona hawaamini kuwa lipo tatizo na sasa kuna "shift" kwenye graphics, bao, mkole nk. Hii ni dalili kuwa kazi tuliyonayo Waislam mbele yetu kwa kuwapata ndugu zetu kwa njia ya ustaarabu bado ngumu.
Ama kwa Waislam wenyewe kote tulipopita mikoani mafanikii ni makubwa pasi kiasi. Neno "mfumokristo" linafahamika vyema kabisa. Na katika kutatua hili tatizo wamekuja na na kauli mbiu "kushugulika" wengine huongeza "kushughulika vizuuuri." Hizo "u" za kuvuta sijajua maana yake.
Nchi yetu ina vyombo vya usalama naamini taarifa zishakwenda kwa wahusika na bila shaka wametoa nini kifanyike kuondoa hili janga linalonyemelea taifa letu.
Waislam ni watu wa subira.
Tunasubiri. Sasa namaliza kwa kusema wewe huoni tatizo sasa kama hakuna tatizo hata nikikupa mapendekezo ya kuondoa tatizo itasaidia nini ndugu yangu? Mohamed
Hao unaosema wanashangilia na kuelewa maana ya mfumo kristo nakuambia wanaimba. Wanaimba kwasababu wewe unayewaambia huwezi kueleza umma wa JF nini maana yake. Kama utaweza nisute pasi kusita.
Mohamed nchi yetu haitegemei vyombo vya usalama kwa usalama wetu, usalama wetu ni jukumu letu. Vyombo vya usalama vina majukumu inapofikia mahali pake. Jukumu la kwanza la raia kama wewe si kuchochea halafu uombe vyombo vya ulinzi. Kwa taarifa yako vyombo vya ulinzi vingeingilia uchochezi wenu, huo ni mfumokristo kama unavyolaumu vyombo vya habari kwa kuacha kuandika uchochezi.
Ulipokwenda mikoani hukueleza vyombo vya usalama, sasa umeshavuruga unataka viingilie kati.
Unachokifanya hapa ni fitna halafu unajikosha kwa unafiki. Ni maneno makali lakini nimeangalia kamusi ya kiswahili hakuna mbadala, niwie radhi kama ni karaha lakini kijiko tuite kijiko na sio koleo.
Mkandara ameeleza vizuri sana, tatizo sio waislam ni kikundi cha akina Mohamed ambacho kimedhamiria kuliona taifa lina mgogoro. Kikundi hiki kinadhani kuwa kufanya hivyo ni sehemu ya biashara halali na ni thawabu kwa mwenyezi mungu. Huo si uislam ni sawa na wale wanaodhani kuwa ukilipua ubalozi wa Tanzania na kuua Watanzania ni sehemu ya kwenda peponi. Ni kuichafua dini tu, hakuna ukweli wa hilo hata kidogo
Nikukumbushe kuwa suala la kadhi lilikuwa hivi hivi, badala ya wasomi kama Mohamed kutafuta logic ya tatizo wakatafuta logistic za kwenda mikoani. Leo Mohamed ni aibu tupu unapoandika historia na kutaja wazee wako wakati huo huo hujui kuwa mahakama ya kadhi ilikuwepo na wala haikuondolewa. Hujajifunza Mzee Said.
Mzee Said sijui kama unajua unaongea nini, maana sentensi zako zinakusuta. Umesema kuwa umeliona tatizo na kulieza, halafu unasema tena kuwa vyombo vya uslama vishughulikie!!
Wewe umeliona tatizo hili miaka 20 iliyopita na hujaweza kueleza nini hasa unachotaka, na wala, kamwe asilani na abadan Mohamed Salim Salum hajatoa pendekezo lolote la nini kifanyike. Pendekezo analotoa ni la vyombo vya usalama kushughulikia kitu asichoweza kushauri.
Ikifika hapo, mimi huwa najiuliza unakwenda ulaya na marekani kutoa maarifa gani ambayo hujayoatoa nyumbani kwenu.
Too low mzee wangu and the more you talk the more you lose credibility. To be honest with you.
Badala ya kwenda kueneza fitna kaeni chini mujiulize tatizo la msingi lipo wapi. Mkandara amesema, uta replace nini kwa nothing.
Mumeandika matamko yaliyowadhalilisha waislam na Mohamed unahusika halafu unasema kuna dhulma na sio kujidhulumu
Kaeni chini mfikiri kujenga hospitali ya rufaa Singida ili mumsaidie mwanadamu na muombe MoU.
Kaeni chini mseme hivi, kwa vile wenzetu wakristo wanahuduma za hospitali za rufaa, sisi tutaanzisha shule za watoto wadogo mikoani na wiliayani hasa maeneo yalioyo nyuma kielimu kama pwani, tunawasilisha MoU yetu hii.
Kaeni mjiulize kwanini shule za taasisi za kiislam zinaongoza kutoka kusini mwa matokeo
Uislam hauhimizi fitna, unahimiza jitihada na maarifa.Uislam unasimama bila ya jina la Sykes. Kama Sykes na akina Nyerere wangekuwa wanahimiza chuki na fitna historia yetu ingekuwa tofauti. Usiandike Nyerere alikula nini waambie watu wanajifunza nini kutoka kwa maisha ya akina Sykes na Nyerere.