Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Nguruvu3,
Si wewe wa kutuuliza sisi Waislam swali hilo. Sisi hatukutuhumu wewe kwa lolote. Mimi hapa jamvini nimejitahidi kueleza hali ya mambo ilivyo nchini kwetu kwa kutegemea kuwa wengi watakapolijua hili tatizo ndiyo nji ya kwanza ya kutafuta suluhisho.

Wengi kama nawe unavyoona hawaamini kuwa lipo tatizo na sasa kuna "shift" kwenye graphics, bao, mkole nk. Hii ni dalili kuwa kazi tuliyonayo Waislam mbele yetu kwa kuwapata ndugu zetu kwa njia ya ustaarabu bado ngumu.

Ama kwa Waislam wenyewe kote tulipopita mikoani mafanikii ni makubwa pasi kiasi. Neno "mfumokristo" linafahamika vyema kabisa. Na katika kutatua hili tatizo wamekuja na na kauli mbiu "kushugulika" wengine huongeza "kushughulika vizuuuri." Hizo "u" za kuvuta sijajua maana yake.

Nchi yetu ina vyombo vya usalama naamini taarifa zishakwenda kwa wahusika na bila shaka wametoa nini kifanyike kuondoa hili janga linalonyemelea taifa letu.

Waislam ni watu wa subira.
Tunasubiri. Sasa namaliza kwa kusema wewe huoni tatizo sasa kama hakuna tatizo hata nikikupa mapendekezo ya kuondoa tatizo itasaidia nini ndugu yangu? Mohamed
Tatizo lako Mohamed ni kudhani kuwa wewe unaelewa sana kuliko waislam wengine wa Tanzania. Nimeeleza kuwa angalia nani anashangilia na anashangilia nini. Je, anajua anachokishangilia na yupo tayari kukitetea kwa hoja kile anachoshangilia

Hao unaosema wanashangilia na kuelewa maana ya mfumo kristo nakuambia wanaimba. Wanaimba kwasababu wewe unayewaambia huwezi kueleza umma wa JF nini maana yake. Kama utaweza nisute pasi kusita.

Mohamed nchi yetu haitegemei vyombo vya usalama kwa usalama wetu, usalama wetu ni jukumu letu. Vyombo vya usalama vina majukumu inapofikia mahali pake. Jukumu la kwanza la raia kama wewe si kuchochea halafu uombe vyombo vya ulinzi. Kwa taarifa yako vyombo vya ulinzi vingeingilia uchochezi wenu, huo ni mfumokristo kama unavyolaumu vyombo vya habari kwa kuacha kuandika uchochezi.
Ulipokwenda mikoani hukueleza vyombo vya usalama, sasa umeshavuruga unataka viingilie kati.

Unachokifanya hapa ni fitna halafu unajikosha kwa unafiki. Ni maneno makali lakini nimeangalia kamusi ya kiswahili hakuna mbadala, niwie radhi kama ni karaha lakini kijiko tuite kijiko na sio koleo.

Mkandara ameeleza vizuri sana, tatizo sio waislam ni kikundi cha akina Mohamed ambacho kimedhamiria kuliona taifa lina mgogoro. Kikundi hiki kinadhani kuwa kufanya hivyo ni sehemu ya biashara halali na ni thawabu kwa mwenyezi mungu. Huo si uislam ni sawa na wale wanaodhani kuwa ukilipua ubalozi wa Tanzania na kuua Watanzania ni sehemu ya kwenda peponi. Ni kuichafua dini tu, hakuna ukweli wa hilo hata kidogo

Nikukumbushe kuwa suala la kadhi lilikuwa hivi hivi, badala ya wasomi kama Mohamed kutafuta logic ya tatizo wakatafuta logistic za kwenda mikoani. Leo Mohamed ni aibu tupu unapoandika historia na kutaja wazee wako wakati huo huo hujui kuwa mahakama ya kadhi ilikuwepo na wala haikuondolewa. Hujajifunza Mzee Said.

Mzee Said sijui kama unajua unaongea nini, maana sentensi zako zinakusuta. Umesema kuwa umeliona tatizo na kulieza, halafu unasema tena kuwa vyombo vya uslama vishughulikie!!

Wewe umeliona tatizo hili miaka 20 iliyopita na hujaweza kueleza nini hasa unachotaka, na wala, kamwe asilani na abadan Mohamed Salim Salum hajatoa pendekezo lolote la nini kifanyike. Pendekezo analotoa ni la vyombo vya usalama kushughulikia kitu asichoweza kushauri.
Ikifika hapo, mimi huwa najiuliza unakwenda ulaya na marekani kutoa maarifa gani ambayo hujayoatoa nyumbani kwenu.
Too low mzee wangu and the more you talk the more you lose credibility. To be honest with you.

Badala ya kwenda kueneza fitna kaeni chini mujiulize tatizo la msingi lipo wapi. Mkandara amesema, uta replace nini kwa nothing.
Mumeandika matamko yaliyowadhalilisha waislam na Mohamed unahusika halafu unasema kuna dhulma na sio kujidhulumu

Kaeni chini mfikiri kujenga hospitali ya rufaa Singida ili mumsaidie mwanadamu na muombe MoU.
Kaeni chini mseme hivi, kwa vile wenzetu wakristo wanahuduma za hospitali za rufaa, sisi tutaanzisha shule za watoto wadogo mikoani na wiliayani hasa maeneo yalioyo nyuma kielimu kama pwani, tunawasilisha MoU yetu hii.
Kaeni mjiulize kwanini shule za taasisi za kiislam zinaongoza kutoka kusini mwa matokeo

Uislam hauhimizi fitna, unahimiza jitihada na maarifa.Uislam unasimama bila ya jina la Sykes. Kama Sykes na akina Nyerere wangekuwa wanahimiza chuki na fitna historia yetu ingekuwa tofauti. Usiandike Nyerere alikula nini waambie watu wanajifunza nini kutoka kwa maisha ya akina Sykes na Nyerere.
 
Nguruvi3,

Nimekusoma.
Umeeleza mengi lakini kote huko tushapita somo limeeleweka.

Nitakujibu kitu kimoja tu.

Mimi sijifanyi ninajua. Kwa kweli ninajua somo hili na ni "scholar"
wa kutegemewa ndani na nje ya nchi na ushahidi nilishauweka hapa.

Umeona historia ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ndani ya gazeti
Mwananchi. Mwandishi ni Mohamed Said.

Unataka ushahidi gani nikupe uamini kuwa ninajua.

Mwisho Waislam wa Tanzania nzima wananiitikadi mimi kama kiongozi.

Kama unabisha waulize.

Mohamed
 
Jamani nimeuliza swali: ni mfumo gani mnaoutaka kuchukua nafasi ya mfumo wa utawala mnaouita mfumokristo? Mnataka tuwe na utawala kama walivyo Wairan? Mnataka tuwe na utawala wa Saudi Arabia au mnataka tuwe na utawala wa Taleban waliokuwa nao Afghanistan? Maana hatuwezi kuwa na ombwe la utawala. Ndugu zetu Libya wamemwondoa Qaddafi angalieni watakavyohangaika kujaza hilo ombwe la utawala. Misri wamemwondoa Mubarak lakini jeshi bado linashika hatamu. Sasa sisi Tanzania kama Waislamu mtafanikiwa kuondoa huu mfumo mnaouita "kristo," mtatuwekea mfumo gani?
 
Mzee Mohamed, sisi watu wa pwani tunatabia moja ya kujipenda tu.
Nani akupe mji kwa kushindwa kujibu Nyerere alikuja lini Dar es Salaam. Kuna maswali ya MM, Mag3 yamerudia mara 4 hujibu licha ya makumi yaliyotangulia, unakimbilia kusema tukamwue santuri twende mbele. Ungekuwa na data ungeshindwa kuelewa majina ya wajumbe wa kamati kuu ya TANU.

Ni kweli kuwa wewe humhoji mwanadamu aliye hai hadi mauti yamfike. Mwinyi Yupo humhoji, Malima amefariki tunaanza kuona dodosa.
Salim Ahmed Salim, Butiku, Shivji, Sivalon, Jumbe n.k hao huwahoji.

Tunachosikia ni tuhuma za kuua EAMWS za Marhumu mzee Fundikira ambaye miaka michache iliyopita alikuwa anapatikana hadi mitaani.
Hadithi za Kitundu aliyefariki saa chache kabla hujamhoji! tuhuma za Nyerere, Rajab Diwani n.k.

Kuna tofauti kati ya data na uchochezi, data zinamajibu yanayotoa suluhu , uchochezi una hamasa isiyo na suluhu.
Kama una data usingeshindwa kuonyesha hata sehemu moja ya suluhu ya tatizo kwa miaka 20 unayoandika. Kama kuna mahali umetoa suluhu nipe ushahidi wa maandishi, vinginevyo usipige kifua kwasababu ilisemwa debe tupu..

Nguruvi3, Mwkjj, Mkandara na wengine... inaonekana mnashindwa kuelewa maana ya historia. Hivi historia tokea lini ikaandikwa upande mmoja?
MS anaandika kutokana na ushahidi alikokuwa nao. Na nyinyi mnasoma historia yenu iliyopangwa na Hollywood writers-Pro Nyerere.

Sasa kupinga historia inavyoandikwa na MS ni kushindwa kuelewa taaluma kamili ya uandishi wa historia.

Hivi mnajua historia ya USA kuhusu Civil War iilivyoandikwa? North vs South

Hivi manjua historia Slavery in USA ilivyoandikwa? White vs Black or Black vs Black in Africa?

Hivi mnajua historia ilivyoandikwa kuhusu Roman Empire vs Muslims or Jews?

Kama WTZ tulitakiwa tushukuru mchango mkubwa wa MS ktk kuijulisha jamii kuhusu historia ya TZ.

Kuwa critics kwa kila hoja haikufanyi kuwa smart... C'mon let's be honest..
 
Na wewe Mr. Wrong,'
Nani kakuambia historia ya Mohammed ya kusimuliwa na wazazi wake ndiyo historia sahihi? Mambo ya kusimuliwa katika elimu huitwa "hearsay."
 
Jamani nimeuliza swali: ni mfumo gani mnaoutaka kuchukua nafasi ya mfumo wa utawala mnaouita mfumokristo? Mnataka tuwe na utawala kama walivyo Wairan? Mnataka tuwe na utawala wa Saudi Arabia au mnataka tuwe na utawala wa Taleban waliokuwa nao Afghanistan? Maana hatuwezi kuwa na ombwe la utawala. Ndugu zetu Libya wamemwondoa Qaddafi angalieni watakavyohangaika kujaza hilo ombwe la utawala. Misri wamemwondoa Mubarak lakini jeshi bado linashika hatamu. Sasa sisi Tanzania kama Waislamu mtafanikiwa kuondoa huu mfumo mnaouita "kristo," mtatuwekea mfumo gani?

Jasusi rudia topic ili ujue hoja kamili ya hii article.

Kuwa na mfumo kristo au secular siyo hoja- muhimu ni kuwa na mfumo ambao una haki, usiokuwa na dhulma. Wakristo, Waislam na binadamu sote tuna agenda moja- maisha mazuri kwa raia wote bila ya ubaguzi wowote.

Waislamu wanapigania haki yao ya msingi; na dhulma inayofanywa kwa misingi ya ubaguzi wa Kidini. Waislamu wanataka system yenye haki bila ya kuwa na upendeleo wowote.

USA walikuwa na Civil Right movement in 1961-1969 kupigania haki za msingi kwa raia wote bila ya kujali rangi zao, dini zao, au gender zao. Kabla ya Uhuru Tanganyika ilikuwa na issue kama hiyo. Waislam wakawa kipaumbele ktk Uhuru-lakni matokeo yake Nyerere akawatosa.

Sasa hivi Muslims wanataka another Independent ambayo itawakomboa ktk system hii ya dhulma.
 
Na wewe Mr. Wrong,'
Nani kakuambia historia ya Mohammed ya kusimuliwa na wazazi wake ndiyo historia sahihi? Mambo ya kusimuliwa katika elimu huitwa "hearsay."

Naona unashindwa kuelewa issue ya MS na hearsay. Issue ya MS SIYO hearsay kama unavyosema wewe. Sykes is known person to TZ historian also around the world. So, in this manner, kuna ushahidi wa kutosha kwamba haya maneno anayoyasema MS ni 100% true based on Sykes mwenyewe.

Kumbuka, hearsay inakuja tu pale mtu anaezungumzwa hajatoa ushahidi wake hadharani. Sykes alishiriki ktk Uhuru kwa hiyo huwezi kusema hii ni hearsay.
 
ooh ok.. nilidhani mfumo wa Magharibi uliletwa na kujengwa na wakoloni wa nchi za Kimagharibi; Nyerere alizaliwa aliukuta kina Sykes waliupigania na kunufaika nao na wao waliukuta na hata Bw. Said naye ameutumikia na amenufaika nao na hawezi kuishi bila kuutumikia?

Oooh kwa hiyo hapo ni nani mwenye makosa, bwana Saidi anaeandika ya Wazee wake wa Gerezani au Nyerere aliekuwa kwenye madaraka yenye uwezo wa kuubadilisha asiweze? Naona unajaribu kila hila kutupeleka unakotaka taka wewe, sasa tueleze ni Mzee yupi anaemuandika Mohamed Said na wasifu wake ikawa si alivyo andika Mohamed Said na wewe utupe mbadala kama ulivyoaribu katika famous post #162 ikala nyundo kwenye post#167 ukabana kimyaa hukuigusa tena, basi hata ku appreciate somo ulilopewa imekushinda? Unanshangaza.
 
Nguruvi3,

Nimekusoma.
Umeeleza mengi lakini kote huko tushapita somo limeeleweka.

Nitakujibu kitu kimoja tu.

Mimi sijifanyi ninajua. Kwa kweli ninajua somo hili na ni "scholar"
wa kutegemewa ndani na nje ya nchi na ushahidi nilishauweka hapa.

Umeona historia ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ndani ya gazeti
Mwananchi. Mwandishi ni Mohamed Said.

Unataka ushahidi gani nikupe uamini kuwa ninajua.

Mwisho Waislam wa Tanzania nzima wananiitikadi mimi kama kiongozi.

Kama unabisha waulize.

Mohamed

Hapana hata kidogo; ukweli wa kile unachoandika hautokani na wewe kuandika kwenye gazeti lolote duniani au hata kutoa mihadhara sehemu mbalimbali duniani. Wewe kualikwa kutoa mihadhara au kuelezea unachokiita historia hakifanyi kuwa kile unachosema kuwa ni historia. Marekani wanaamini sana - katika vyuo vikuu hasa - kile kinachoitwa "academic freedom" ambapo wasomi wanaruhusiwa kutoa mawazo hata kama si mawazo yanaykubalika na jamii kubwa ya watu. Wanapotoa mawazo hayo hujiweka katika nafasi ya kuhojiwa ili wayatetee hoja kwa hoja, neno kwa neno.

Msomi ambaye kwa mfano anapendekeza mauaji ya huruma (mercy killings) ya wazee au wagonjwa anaweza kutumia hoja mbalimbali za kisomi lakini hawezi kulazimisha kuwa ni kweli kwa vile yeye ni msomi kasema hivyo. Historia ni hivyo hivyo. Bahati mbaya unachoandika kwa muda mrefu siyo historia ni mchangano wa hisia na uanaharakati wa kidini (a mixture of history and religious activism). Unajaribu kutumia historia kutekeleza harakati za kile ambacho umekiita ni "dhulma ya Waislamu".

Sasa kwa vile ushaona dhulma umetoka na kwenda kutafuta ushahidi wa kihistoria wa dhulma hizo. Ukagundua kabisa kuwa ili hoja yako ya dhulma ikamilike ni lazima mambo fulani yafanyike. Yafuatayo yanafanyika:

a. Udai hii ni historia ya 'wazee wako' na ya kuwa uliisikia moja kwa moja kutoka ka "baba" au mzee fulani. Kwa kudai hivyo ni vigumu kwa mtu yeyote kupinga kwani utapigangana vipi na sauti ya wazee ambao hawapo leo? Hivyo watu wanatokea kuamini tu kuwa ukishasema "mzee x aliambiwa na Nyerere naye akamwambia mzee y ambaye alimwambia mzee wako basi watu wanatakiwa wakubali. Ukiulizwa juu ya hili unasema "mi niliawambiwa na wazee wangu na hilo latosha". Well.. hiyo siyo historia tena.

b. Unatafuta na kufuatilia majina ya Kiislamu tu na mchango wao katika harakati za uhuru na kuweka pembeni mchango wa watu wengine wote. Kwa mfano japo umeandika kitabu cha Abdulwahid Sykes sitegemei kuwa unafikiria au hata unaweza kuandika kitabu cha Dr. Vedastus Kyaruzi. Kwanini? Well Sykes ni Muislamu na Kyaruzi ni Mkristu japo wote wawili walifahamika sana na wazee wako na siwezi kushangaa kuwa hata mzee wako alikuwa anamfahamu kwa karibu Kyaruzi! Utaona hata historia ya TANU kabla ya Nyerere kuingia hasa unaiweka kwa misingi ya dini; huwagusi wala kuwataja wazee "wetu" kina Stephan Mhando au kina Kirilo Japhet na wengine wengi tu. Wewe ukizungumzia wanaharakati wa Tabora unawaruka Wakristu au unaweka msisitizo katika Waislamu! Sasa hiyo huwezi kuita historia!

c. Katika kuandika historia yako ulitumia zaidi ya maiaka mitano kukusanya taarifa na ushahidi mbalimbali wa kuandika kitabu cha Sykes. Kikachapwa mwaka 1998 wakati Nyerere yuko hai. Hata mara moja hujaandika barua kutaka kuonana na Nyerere au kutaka kumuuliza. Ila unatuambia (kwa kumtumia Marehemu mwingine) kuwa Prof. Othman kuwa ndiye aliyeenda kumwambia Nyerere atoe majibu ya hoja zako na za shehe Barwan. Wewe mwenyewe hata mara moja hukwenda kumtafuta Mwalimu au hata kuandika Barua iliyokuwa na hoja au maswali yako na kutaka Nyerere ajibu. ULikuwa na miaka mitano ya kufanya hivyo hukufanya. Lakini Prof. Othman akionesha weledi na umakini wa kisomi alijua uzito wa hoja zako akaamua kwendea Mwalimu na kumwambia hayo. Tena nikiamini maneno yako kusema kuwa Prof. Othman akamwambia Nyerere "ni lazima ujibu". Huyu huyu Nyerere tunayeambiwa alikuwa na chuki na Waislamu na tena huweki hata msisitizo wa jibu lake. Unatuambia kwenye masimulizi yako kuwa Nyerere alikubali tena akamwomba Muislamu - rafiki yako na mwalimu wako kuandika historia yake! Hilo huoni wewe ni la kheri la kuonesha kuwa Mwalimu alikuwa hana hofu na waislamu na alikuwa na majibu ya hoja zako zote. Tena unatuambia hata tume ilishaundwa - japo hutaki kutaja majina yao.

d. Hilo la "c" linaenda mbilimbili. Miaka zaidi ya kumi ya kuandika kitabu cha Sykes hujamuendea Mama Maria Nyerere na kumuuliza kuhusu mume wake ambaye tunajua kabisa alikuwa naye tangu wanakuja Dar, wameishi wote.. na kwa hakika kabisa hakuna mtu aliyekuwa anawajua kwa karibu Sykes na Nyerere na wapigania uhuru wengine wa awali kama Mama Maria. Lakini utasubiri huyu mama afe alafu utujie na simulizi la jinsi Mama Nyerere ndiye alikuwa anamshawishi Nyerere kuwakimbia kina Sykes! Na wapo watakaoamini hivyo!

Leo hii unachoandika wapo wanaoamini kuwa ni historia "iliyofichwa". Hawajui katika simulizi la historia "iliyofichwa" historia nyingine nayo "imefichwa". Yaani kile kile unachomtuhumu Nyerere kuwa alikifanya kuhusu "wazee wako" na wewe unakifanya kuhusu "wazee wetu" na hapa "wazee wetu" kinyume na wewe simaanisha "wazee wakristu". Namaanisha wazee wetu wote walioshiriki katika harakati za uhuru.

Ningelikuwa na muda wa kutosha na vitendea kazi vya kutosha ningeweza kabisa kutumia kitabu chako peke yake kuweza kuiandika historia yetu vizuri kweli bila kuweka au kulazimisha hisia za kidini kwa uhakika kabisa ni kitabu kizuri cha burudani na huchangamsha fikra lakini kukiita cha kihistoria ni kukebehei sayansi hii ya historia. Ni sawasawa na unalazimisha mbuzi wawili kuwafunga jembe la plau na kuwalazimisha kulima. Kweli wataonekana wamefungwa vizuri tu lakini hawatlima. Hii ya kwako Shehe siyo historia - ni histosia! Yaani historia inayotumika kuelezea hisia na sio matukio yaliyotukia.

Na kweli kabisa kama kuna watu wana usomi au hata wanadalili ya usomi ambao wanapokea masimulizi haya kama historia na kuyakubali bila kuyakosoa kisomi kwa kuhoji the credibility and plausibility of the evidence presented na wakaamini unachosema basi tuna matatizo makubwa zaidi katika wasomi wetu kuliko tunavyofikiria. Msomi ni lazima aulize maswali na msomi mzuri ni yule anayejibu maswali ya wasomi wenzake. Siyo kutuambia ati "naalikwa miye huko na huko duniani" au "napendwa miye na Waislamu wenzangu" au "Nalipwa mabuku mengimengi kwa kuzungumza" hayo yote yaweza kuwa mema na ya kheri kwako lakini hayafanyi unachosema kuwa ni kweli. Kwani hata kikundi cha DDC Kibisa walikuwa wanaenda pote Tanzania na duniani kutumbuiza na wakaigiza vizuri tu na kufurahisha kadamnasi. Lakini haikuwafanya kudai usomi au weledi.

NIna uhakika siku utakayoamua kuandika historia kweli itakuwa nzuri sana kwani kama kipaji unacho na vyanzo uanvyo lakini itakubidi utoke kwanza kwenye uanaharakati na kuwa msomi kweli wa historia na kuufuata ushahidi wa historia popote utakakokupeleka.
 
Duh! I didn't know that, kumbe the subject is this wide!

Soma kichwa cha hii nyuzi. Hatuoni panapokosolewa aliyoandika Mohamed Said ambapo hajayapa jibu ila tunaona mjadala unapanuliwa kutafuta pa kutokea as wider as the escape routes would be.

Jee, unaweza msaidia Mzee Mwanakijiji kujibu post #167 iliyomjibu post yake #162 ambayo imembonda vibaya sana kiasi ambacho hata kuirudia ile mada imekuwa ni muhali basi hata ku "appreciate" darsa alilopewa? na nyie washabik wake hata hamkutia japo "Ahsante"? msaidieni mwenzenu anapopotoka kutaka kupotosha wengine kwani yale yasingetupotosha sisi tu yasingewekwa sawa na Mohamed Said, hata nyinyi mngekuwa mmepotoshwa au hamlioni hilo?
 
Bibie naona MKandara kamaliza kila kitu.. Point zimekuishia ukaona uongeze idadi ya post zako

Sana tena, kamaliza kila kitu, na namsifu na nnakusifu wewe kwa kuliona hilo. Tuendelee na mada.

Wapi Mohamed Said ame "finyangafinyanga" hoja yake mtuoneshe ili Mohamed Said apate fursa ya kumwaga nyundo, msitake kuupeleka huu mjadala kwa FaizaFoxy, sidanganyiki!
 
Mzee Mohamed, sisi watu wa pwani tunatabia moja ya kujipenda tu.
Nani akupe mji kwa kushindwa kujibu Nyerere alikuja lini Dar es Salaam. Kuna maswali ya MM, Mag3 yamerudia mara 4 hujibu licha ya makumi yaliyotangulia, unakimbilia kusema tukamwue santuri twende mbele. Ungekuwa na data ungeshindwa kuelewa majina ya wajumbe wa kamati kuu ya TANU.

Ni kweli kuwa wewe humhoji mwanadamu aliye hai hadi mauti yamfike. Mwinyi Yupo humhoji, Malima amefariki tunaanza kuona dodosa.
Salim Ahmed Salim, Butiku, Shivji, Sivalon, Jumbe n.k hao huwahoji.

Tunachosikia ni tuhuma za kuua EAMWS za Marhumu mzee Fundikira ambaye miaka michache iliyopita alikuwa anapatikana hadi mitaani.
Hadithi za Kitundu aliyefariki saa chache kabla hujamhoji! tuhuma za Nyerere, Rajab Diwani n.k.

Kuna tofauti kati ya data na uchochezi, data zinamajibu yanayotoa suluhu , uchochezi una hamasa isiyo na suluhu.
Kama una data usingeshindwa kuonyesha hata sehemu moja ya suluhu ya tatizo kwa miaka 20 unayoandika. Kama kuna mahali umetoa suluhu nipe ushahidi wa maandishi, vinginevyo usipige kifua kwasababu ilisemwa debe tupu..

Nyerere amhoji nini na Mohamed Said kashusha "nyundo" wakati Nyerere yu hai na kisha kujibu Profeessor Haroub akamwambia Nyerere ajibu, Nyerere akabana, analo jibu? ulitaka ujibiwe nini zaidi? na mmoja wenu aliuliza kuhusu hilo la Nyerere kuulizwa na Professor Haroub, akapewa jibu ya kitabu na kinakopatikana yaliyopo hayo maneno, vipi mmehakiki kuwa ni sawa au si sawa? hamjarudi, mnazunguka. Hoja hujibiwa na hoja na si viroja.
 
Soma kichwa cha hii nyuzi. Hatuoni panapokosolewa aliyoandika Mohamed Said ambapo hajayapa jibu ila tunaona mjadala unapanuliwa kutafuta pa kutokea as wider as the escape routes would be.

Jee, unaweza msaidia Mzee Mwanakijiji kujibu post #167 iliyomjibu post yake #162 ambayo imembonda vibaya sana kiasi ambacho hata kuirudia ile mada imekuwa ni muhal basi hata ku "appreciate" darsa alilopewa? na nyie washabik wake hata hamkutia japa "Ahsante"? msaidieni mwenzenu anapopotoka kutaka kupotosha wengine kwani yale yasingetupotsha sisis tu yasingewekwa sawa na Mohamed Said, hata nyinyi mngekuwa mmepotoshwa au hamlioni hilo?

Oyaa hiyo tabia yako ya ligi ni asili na uelewe kitu kimoja kwamba hapa kila mtu anatoa maoni yake kwa jinsi anavyoona yeye. Hatushindani hapa at least that is the way I personally believe. Na hii habari ya nyinyi na wao ndiyo inakufanya usielewe kinachojadiliwa hisia mbele kama kawaida. Mjadala wako na Mkjj iweje utake kulazimisha watu wengine waingie? Vipi mbona unaanza kuchezesha kimkia mapema mbele ya wanaume? Man up toa hoja sio kila wakati ligi ligi tuuuuuuuuuuuu!!!!!!
 
Basi hata kuna mjadala? nimepitia kusoma hizo posts na hakuna yoyote ambayo naweza kusema inahitaji maelezo ya ziada ndio maana nikaziachia.
 
U
Hapana hata kidogo; ukweli wa kile unachoandika hautokani na wewe kuandika kwenye gazeti lolote duniani au hata kutoa mihadhara sehemu mbalimbali duniani. Wewe kualikwa kutoa mihadhara au kuelezea unachokiita historia hakifanyi kuwa kile unachosema kuwa ni historia. Marekani wanaamini sana - katika vyuo vikuu hasa - kile kinachoitwa "academic freedom" ambapo wasomi wanaruhusiwa kutoa mawazo hata kama si mawazo yanaykubalika na jamii kubwa ya watu. Wanapotoa mawazo hayo hujiweka katika nafasi ya kuhojiwa ili wayatetee hoja kwa hoja, neno kwa neno.

Msomi ambaye kwa mfano anapendekeza mauaji ya huruma (mercy killings) ya wazee au wagonjwa anaweza kutumia hoja mbalimbali za kisomi lakini hawezi kulazimisha kuwa ni kweli kwa vile yeye ni msomi kasema hivyo. Historia ni hivyo hivyo. Bahati mbaya unachoandika kwa muda mrefu siyo historia ni mchangano wa hisia na uanaharakati wa kidini (a mixture of history and religious activism). Unajaribu kutumia historia kutekeleza harakati za kile ambacho umekiita ni "dhulma ya Waislamu".

Sasa kwa vile ushaona dhulma umetoka na kwenda kutafuta ushahidi wa kihistoria wa dhulma hizo. Ukagundua kabisa kuwa ili hoja yako ya dhulma ikamilike ni lazima mambo fulani yafanyike. Yafuatayo yanafanyika:

a. Udai hii ni historia ya 'wazee wako' na ya kuwa uliisikia moja kwa moja kutoka ka "baba" au mzee fulani. Kwa kudai hivyo ni vigumu kwa mtu yeyote kupinga kwani utapigangana vipi na sauti ya wazee ambao hawapo leo? Hivyo watu wanatokea kuamini tu kuwa ukishasema "mzee x aliambiwa na Nyerere naye akamwambia mzee y ambaye alimwambia mzee wako basi watu wanatakiwa wakubali. Ukiulizwa juu ya hili unasema "mi niliawambiwa na wazee wangu na hilo latosha". Well.. hiyo siyo historia tena.

b. Unatafuta na kufuatilia majina ya Kiislamu tu na mchango wao katika harakati za uhuru na kuweka pembeni mchango wa watu wengine wote. Kwa mfano japo umeandika kitabu cha Abdulwahid Sykes sitegemei kuwa unafikiria au hata unaweza kuandika kitabu cha Dr. Vedastus Kyaruzi. Kwanini? Well Sykes ni Muislamu na Kyaruzi ni Mkristu japo wote wawili walifahamika sana na wazee wako na siwezi kushangaa kuwa hata mzee wako alikuwa anamfahamu kwa karibu Kyaruzi! Utaona hata historia ya TANU kabla ya Nyerere kuingia hasa unaiweka kwa misingi ya dini; huwagusi wala kuwataja wazee "wetu" kina Stephan Mhando au kina Kirilo Japhet na wengine wengi tu. Wewe ukizungumzia wanaharakati wa Tabora unawaruka Wakristu au unaweka msisitizo katika Waislamu! Sasa hiyo huwezi kuita historia!

c. Katika kuandika historia yako ulitumia zaidi ya maiaka mitano kukusanya taarifa na ushahidi mbalimbali wa kuandika kitabu cha Sykes. Kikachapwa mwaka 1998 wakati Nyerere yuko hai. Hata mara moja hujaandika barua kutaka kuonana na Nyerere au kutaka kumuuliza. Ila unatuambia (kwa kumtumia Marehemu mwingine) kuwa Prof. Othman kuwa ndiye aliyeenda kumwambia Nyerere atoe majibu ya hoja zako na za shehe Barwan. Wewe mwenyewe hata mara moja hukwenda kumtafuta Mwalimu au hata kuandika Barua iliyokuwa na hoja au maswali yako na kutaka Nyerere ajibu. ULikuwa na miaka mitano ya kufanya hivyo hukufanya. Lakini Prof. Othman akionesha weledi na umakini wa kisomi alijua uzito wa hoja zako akaamua kwendea Mwalimu na kumwambia hayo. Tena nikiamini maneno yako kusema kuwa Prof. Othman akamwambia Nyerere "ni lazima ujibu". Huyu huyu Nyerere tunayeambiwa alikuwa na chuki na Waislamu na tena huweki hata msisitizo wa jibu lake. Unatuambia kwenye masimulizi yako kuwa Nyerere alikubali tena akamwomba Muislamu - rafiki yako na mwalimu wako kuandika historia yake! Hilo huoni wewe ni la kheri la kuonesha kuwa Mwalimu alikuwa hana hofu na waislamu na alikuwa na majibu ya hoja zako zote. Tena unatuambia hata tume ilishaundwa - japo hutaki kutaja majina yao.

d. Hilo la "c" linaenda mbilimbili. Miaka zaidi ya kumi ya kuandika kitabu cha Sykes hujamuendea Mama Maria Nyerere na kumuuliza kuhusu mume wake ambaye tunajua kabisa alikuwa naye tangu wanakuja Dar, wameishi wote.. na kwa hakika kabisa hakuna mtu aliyekuwa anawajua kwa karibu Sykes na Nyerere na wapigania uhuru wengine wa awali kama Mama Maria. Lakini utasubiri huyu mama afe alafu utujie na simulizi la jinsi Mama Nyerere ndiye alikuwa anamshawishi Nyerere kuwakimbia kina Sykes! Na wapo watakaoamini hivyo!

Leo hii unachoandika wapo wanaoamini kuwa ni historia "iliyofichwa". Hawajui katika simulizi la historia "iliyofichwa" historia nyingine nayo "imefichwa". Yaani kile kile unachomtuhumu Nyerere kuwa alikifanya kuhusu "wazee wako" na wewe unakifanya kuhusu "wazee wetu" na hapa "wazee wetu" kinyume na wewe simaanisha "wazee wakristu". Namaanisha wazee wetu wote walioshiriki katika harakati za uhuru.

Ningelikuwa na muda wa kutosha na vitendea kazi vya kutosha ningeweza kabisa kutumia kitabu chako peke yake kuweza kuiandika historia yetu vizuri kweli bila kuweka au kulazimisha hisia za kidini kwa uhakika kabisa ni kitabu kizuri cha burudani na huchangamsha fikra lakini kukiita cha kihistoria ni kukebehei sayansi hii ya historia. Ni sawasawa na unalazimisha mbuzi wawili kuwafunga jembe la plau na kuwalazimisha kulima. Kweli wataonekana wamefungwa vizuri tu lakini hawatlima. Hii ya kwako Shehe siyo historia - ni histosia! Yaani historia inayotumika kuelezea hisia na sio matukio yaliyotukia.

Na kweli kabisa kama kuna watu wana usomi au hata wanadalili ya usomi ambao wanapokea masimulizi haya kama historia na kuyakubali bila kuyakosoa kisomi kwa kuhoji the credibility and plausibility of the evidence presented na wakaamini unachosema basi tuna matatizo makubwa zaidi katika wasomi wetu kuliko tunavyofikiria. Msomi ni lazima aulize maswali na msomi mzuri ni yule anayejibu maswali ya wasomi wenzake. Siyo kutuambia ati "naalikwa miye huko na huko duniani" au "napendwa miye na Waislamu wenzangu" au "Nalipwa mabuku mengimengi kwa kuzungumza" hayo yote yaweza kuwa mema na ya kheri kwako lakini hayafanyi unachosema kuwa ni kweli. Kwani hata kikundi cha DDC Kibisa walikuwa wanaenda pote Tanzania na duniani kutumbuiza na wakaigiza vizuri tu na kufurahisha kadamnasi. Lakini haikuwafanya kudai usomi au weledi.

NIna uhakika siku utakayoamua kuandika historia kweli itakuwa nzuri sana kwani kama kipaji unacho na vyanzo uanvyo lakini itakubidi utoke kwanza kwenye uanaharakati na kuwa msomi kweli wa historia na kuufuata ushahidi wa historia popote utakakokupeleka.

Mkuu MWKKJ,
Umeongea vizuri sana na umejenga hoja nzuri kama kawaida yako,ila hilo ni kuendelea kumfanya Muhamed Said "punching bag".kama Muhamed Said ameeandika "HISTOHISIA" ya "wazee" wake walio kufaa basi "wazee wako" kama Mama Maria,Vedasto Kialuzi na wengineo si wako hai?waandikie historia itakayo kinzana na MS
 
Nguruvi3,

Nimekusoma.
Umeeleza mengi lakini kote huko tushapita somo limeeleweka.

Nitakujibu kitu kimoja tu.

Mimi sijifanyi ninajua. Kwa kweli ninajua somo hili na ni "scholar"
wa kutegemewa ndani na nje ya nchi na ushahidi nilishauweka hapa.

Umeona historia ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ndani ya gazeti
Mwananchi. Mwandishi ni Mohamed Said.

Unataka ushahidi gani nikupe uamini kuwa ninajua.

Mwisho Waislam wa Tanzania nzima wananiitikadi mimi kama kiongozi.

Kama unabisha waulize.

Mohamed

Hana haja ya kuuliza, tupo hapa na tunahakikisha hilo ni sahihi. Muislaam ataepinga hilo basi huyo haishi Tanzania na haijuwi Tanzania.
 
U

Mkuu MWKKJ,
Umeongea vizuri sana na umejenga hoja nzuri kama kawaida yako,ila hilo ni kuendelea kumfanya Muhamed Said "punching bag".kama Muhamed Said ameeandika "HISTOHISIA" ya "wazee" wake walio kufaa basi "wazee wako" kama Mama Maria,Vedasto Kialuzi na wengineo si wako hai?waandikie historia itakayo kinzana na MS

You are missing the point. Kwangu mimi kina Sykes, kina Tambaza, kina Bi. Titi na wale wote ambao yeye anawataja kuwa ni wazee "wake" kwa sababu ya Uislamu wao kwangu mimi ni wazee "wangu" kwa sababu ya Utanganyika/Utanzania wao. Historia anayoidai ni ya "wazee wake" kwangu mimi ni historia ya "wazee wetu". Hadi atakapoweza kuona anahitaji kuandika historia ya wazee "wetu" ndio ataitendea haki historia. Bahati mbaya hataki kuandika historia yetu, au ya taifa letu au ya wale waliotoa mchango katika historia hiyo ambao wamesahauliwa na historia - Wakristu kwa Waislamu. Lakini hawezi kufanya hivyo na that my friend is a tragedy of historical proportion!
 
Oyaa hiyo tabia yako ya ligi ni asili na uelewe kitu kimoja kwamba hapa kila mtu anatoa maoni yake kwa jinsi anavyoona yeye. Hatushindani hapa at least that is the way I personally believe. Na hii habari ya nyinyi na wao ndiyo inakufanya usielewe kinachojadiliwa hisia mbele kama kawaida. Mjadala wako na Mkjj iweje utake kulazimisha watu wengine waingie? Vipi mbona unaanza kuchezesha kimkia mapema mbele ya wanaume? Man up toa hoja sio kila wakati ligi ligi tuuuuuuuuuuuu!!!!!!

Soma kichwa cha hii nyuzi. Hatuoni panapokosolewa aliyoandika Mohamed Said ambapo hajayapa jibu ila tunaona mjadala unapanuliwa kutafuta pakutokea as wider as the escape routes would be.

Back
Top Bottom