Mwambieni alete tu lakini atawapa nyie ambao hamna ujasiri wa kufanya intellectual criticism kwa sababu mshakubali prima facie and by doing that your doing all of us a huge disservice. I'm quite sure yeyote kati yenu akiamua tu kidogo kufanya ukosoaji wa madai ya Bw. Said anaweza kujikuta anasikia uchungu. Ila inahitaji ujasiri kweli kumkosoa mtu ambaye tayari umekubali hata kabla hujasikia amesema nini. Na ninaombea kuwa wanaofanya hivyo si wasomi bali wanatumia imani kuamua na siyo uwezo wao waliopewa na Mwenyezi Mungu kuhoji, kuuliza, kusahihisha na hatimaye kuboresha kile wanachosikia.
Ukiona watu wanaoitwa wasomi - au wanaoamini kuwa ni wasomi - wanakubali maelezo ya msomi mwenzio bila kujaribu kuyakosoa basi ujue wana maslahi ambayo ni kinyume na kuutafuta ukweli kwani kwao ukweli siyo kile kinachosemwa bali yule anayesema. A tradegy of sort if you will.
So in your thinking msomi wa kweli ni yule mwenye kucriticise sio? Hivi unafahamu the difference between critique and criticism Mwanakijiji?
Hakuna aliyemeza article za mohamed said at first sight (prima facie). Mie kabla sijamsoma Mohamed Said nilishasoma vitabu vingi na kujua mengi kumbuka nilishawahi kufanya mjadala na Sheikh Ali Nabwa nikajiona nina mapungufu sana katika ufahamu wangu historia. I used to believe in the same context kama wewe. Nikaanza kusoma vitabu vya historia pale maktaba kuu zanzibar. Nikahamia Dar. Na pia kupitia article za watu nje ya nchi. Mkuu there is more that meets the eye. ushauri wangu ni hivi hebu kuwa na open thinking. Soma kama vile hujui kitu ili uweze kujua (sheikh wetu madras alikuwa akituambia hivyo).
Hakuna mtu anamaslahi mzee this is an intellectual challenge which you do not have the authority to challenge labda akina Dr Kiyaruzi, Professor Shivji na wengineo ndio wanaweza ila sio wewe.