Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Mwanakijiji nakushukuru kwa kuniadhimisha na wewe nakuombea dua Allah akuongoze uujue ukweli tuwe
pamoja katika kupigania haki.
Amin.
Miye kwa kweli ningefurahi sana kukuona unapigania haki za Watanzania wote usogee niliko miye. Maana naamini kabisa ujuzi wote ulionao tungeweza kuutumia vizuri sana kupambana na ufisadi ambao unawadhuru watu wetu -Waislamu na Wakristu. Ningefurahi kuona unatumia historia uijuayo kuupinga MFUMO FISADI ambao umeundwa na kutengenezwa na watu wenye imani na wasio na imani, wazungu na weusi, Wakristu na Waislamu. Ndio mfumo hatari zaidi unaowaweka watu wetu chini. Kupigana na "Mfumo Kristu" ni sawa na kupigana na hewa tu.
Namwomba Mnyezi Mungu akupe ujasiri wa kutambua kuwa nchi yetu inasumbuliwa na ufisadi na utawala uliojengwa kwa msingi wa ufisadi na ya kwamba ni sisi wana na mabinti wa taifa hili tukisimama pamoja na kutambua hilo ndipo tunaweza kupigania haki yetu na utu wetu kwa pamoja ni katika kufanya hivyo iutaona kuwa hakutakuwa na Waislamuw watakaolalamika kuwa wanadhulumiwa kwani matatizo yao ni matatizo yetu sote na mafanikio ya taifa ni mafanikio yao pia.
Wazee wetu walikuwa pamoja kupigana na ukoloni wa kisiasa na wakawa pamoja hadi mwisho; leo hii tunakabiriwa na ukoloni wa ufisadi lakini tunagawanywa. Karibu upande huu tuwapiganie Watanzania wote, tuupinge mfumo huu wa utawala wa kifisadi uliojengwa chini ya utawala wa CCM ili kwa pamoja tuweze kuleta nuru mpya kwa Watanzania wote ili asiwepo Mtanzania ambaye anajihisi anadhulumiwa, duni au ambaye hana nafasi sawa na mwingine.
Unasemaje?