Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Mwanakijiji nakushukuru kwa kuniadhimisha na wewe nakuombea dua Allah akuongoze uujue ukweli tuwe
pamoja katika kupigania haki.

Amin.

Miye kwa kweli ningefurahi sana kukuona unapigania haki za Watanzania wote usogee niliko miye. Maana naamini kabisa ujuzi wote ulionao tungeweza kuutumia vizuri sana kupambana na ufisadi ambao unawadhuru watu wetu -Waislamu na Wakristu. Ningefurahi kuona unatumia historia uijuayo kuupinga MFUMO FISADI ambao umeundwa na kutengenezwa na watu wenye imani na wasio na imani, wazungu na weusi, Wakristu na Waislamu. Ndio mfumo hatari zaidi unaowaweka watu wetu chini. Kupigana na "Mfumo Kristu" ni sawa na kupigana na hewa tu.

Namwomba Mnyezi Mungu akupe ujasiri wa kutambua kuwa nchi yetu inasumbuliwa na ufisadi na utawala uliojengwa kwa msingi wa ufisadi na ya kwamba ni sisi wana na mabinti wa taifa hili tukisimama pamoja na kutambua hilo ndipo tunaweza kupigania haki yetu na utu wetu kwa pamoja ni katika kufanya hivyo iutaona kuwa hakutakuwa na Waislamuw watakaolalamika kuwa wanadhulumiwa kwani matatizo yao ni matatizo yetu sote na mafanikio ya taifa ni mafanikio yao pia.

Wazee wetu walikuwa pamoja kupigana na ukoloni wa kisiasa na wakawa pamoja hadi mwisho; leo hii tunakabiriwa na ukoloni wa ufisadi lakini tunagawanywa. Karibu upande huu tuwapiganie Watanzania wote, tuupinge mfumo huu wa utawala wa kifisadi uliojengwa chini ya utawala wa CCM ili kwa pamoja tuweze kuleta nuru mpya kwa Watanzania wote ili asiwepo Mtanzania ambaye anajihisi anadhulumiwa, duni au ambaye hana nafasi sawa na mwingine.

Unasemaje?
 
Wasomi ambao wanakuja na data za kupotosha zikipigwa nyundo, zinachakachuliwa. Kuna post yangu moja niliijibu ya Mwita humu ikaongezewa neno Tanganyika na ikabadilishwa maneno, nani anawapa haki wasomi kubadili maneno? Kuna post ulibandika wewe na nikaitaja sana namba 162 iliyojibiwa na Mohamed Said katika post 167 ikachakachuliwa na sasa haipo kwenye namba hizo na sijui kama ipo kwingine au imebanduliwa kabisa. Huo ndio usomi?

Ikiwa ni elimu, msituone hatujaenda shule, ingawa ni wachache lakini tupo tulioenda shule kwa kadri yetu, tena sana tu.

Faiza,

Sikuwa nikiamini kwamba unaweza kuwa muongo kiasi hiki! Ile post yangu iko vile vile wala haijabadilishwa na wewe kuna mahali ulini quote wakati ukijaribu kujenga hoja yako. Sasa unataka kunishangaza kwamba hata yale uliyoyaandika kwa mkono wako mwenyewe yamebadilishwa, na nani??

Kimsingi ni kwamba katika ile hoja ya Nyerere kuwaunganisha wazee wako na wa maeneo mengine ya Tanganyika hukuwa umeielewa ama kama uliielewa ulikuwa unafanya kusudi kuipotosha ndipo nikaendelea kutoa ufafanuzi ili unielewe. Sasa ulipoona umeshindwa hoja ukakimbilia kusema kuna maneno yameongezwa. Huo ni uongo wa mchana na ni aibu kwa mwanamke wa kiislamu kuongopa. Katika hili unatakiwa uone aibu na umuogope japo muumba wakjo kama huwezi kuwaheshimu binadamu wenzako!
 
Mwanakijiji,

Napenda nikufahamishe kitu kimoja ambacho huenda labda mimi sijakiweka vyema ndiyo maana mara kwa mara unamtaja Mama Maria.

Nyerere aliondokea nyumbani kwa Abdulwahid Sykes kwenda Musoma kumuoa Mama Maria. Mama yake Nyerere Bi Mugaya, mama yake Abdu na Ally Sykes Bi Mluguru, Bi Mwamvua mkewe Abdu pamoja na Dossa na Mama yake Mama Ally (mama yake Dossa) waliishi kama ndugu.

Bi/ Mluguru alikuwa akifua nguo za Abdu na Nyerere kwenye ndoo moja na akizianika uani kwake na kuzipiga pasi. Yako mengi sana.

Wote hao wakishinda nyumbani kwa Bi Mluguru. Opposite na nyumba hiyo akiishi shangazi yangu Sikuzani bint Salum na muwewe Msafiri Mgawe. Shangazi yangu wakati ule ni msichana mdogo.

Yote haya kayaona. Shangazi yangu yu hai anaishi Temeke Dar es Salaam. Hadi Mama Maria anaanzisha biashara ya kuuza mafuta ya taa Mtaa wa Mchikichiki siku za mwanzo za TANU... Hii ndiyo historia ya hawa watu ni historia ya "sacrifice, love and devotion."

Kokote mimi ninapoihadithia historia hii hawakosi watu kutokwa na machozi hasa ninapoingia kueleza fitna ilipoingia kati ya watu hawa baada ya uhuru kupatikana hadi leo utadhani hawakupata kujuana kiasi sisi leo tunabishana kwa vitu ambavyo wala kwa wakati ule havikuwa vikubwa.

Nyerere siku alipokwenda kuhani kifo cha Dossa Mlandizi. Alizungumza hadi akalia.

Na sielezi haya kwa masimango naeleza haya ili muone roho za wazee wetu zilikuwaje. Dossa kafa masikini kwa ajili ya TANU.

Abdu alifilisika biashara yake ya Petrol Station kwa ajili ya TANU na mtu aliyemuokoa alikuwa Nazerali kwa kumkopesha fedha na dhamana nyumba yake ya Stanley.

Mohamed

Sheikh Mohammed basi..utaliza wengi humu ndani. Yaani Nyerere huyuhuyu kisha asema kama hakumbuki Abdul alikuwa na nafasigani katika TAA!!! hii sasa kufru.
 
What if they are both right (wazee wa kigamboni na Mohamed Said). Unajuaje pengine Mohamed Said alikuwa hana access kwa Nyerere au Nyerere hataki kuongea nae? Umejuaje, kama Mama Maria naye hataki kuongea na Mohamed Said? Umejuaje wazee wa kigamboni waliandika historia kwa maamrisho ya state house? Matokeo yake wakaandika historia ya superman Nyerere? Hizo ndio limitation na mapungufu ya utafiti ambao wewe au mtu mwengine anaweza kuuendeleza zaidi tukafaidika. Nakuhamasisha uuendeleze utafiti mkuu ili tujifunze zaidi.

Mwenyewe yupo hapa hajajibu mambo ya kujuaje ntajuaje kama alikuwa ameenda sayari ya Zebaki na Nyerere akiwa Zuhura?
 
Huyu huyu Nyerere aliyekuwa anachukia Uislamu na Waislamu na akamlilia Dossa?

NImesoma baadhi ya haya kwenye kitabu chako lakini hujajibu hilo swali kwanini hujatafuta muda kuzungumza na Mama Maria Nyerere au nawe unaamini kuwa hajasoma hivyo siyo mtu wa kumuuliza au hafai kuulizwa?

Mwanakijiji,

Hebu tusaidiane katika hili maana Mama Maria kakukaa sana kooni. Mathalan nishafika Mwitongo na Mama Maria yuko mbele yangu.

Sasa ungependa nimuulize swali gani?

Mohamed
 
Believe me I can. DON'T DOUBT IT.

Do it if you can, ntakugaragaza, chagua mada yoyote uipendayo na kwa masharti yoyote uyatakayo na kwa lugha yoyote uijuayo. Nakuambia huniwezi, sharti langu ni moja tu, funguwa nyuzi ya pekee, usitafute pakutokea humu kwenye mada ya Mohamed Said.
 
Mwanakijiji,

Hebu tusaidiane katika hili maana Mama Maria kakukaa sana kooni. Mathalan nishafika Mwitongo na Mama Maria yuko mbele yangu.

Sasa ungependa nimuulize swali gani?

Mohamed

aah Nyerere alikuwa anachuki na Uislamu au alikuwa anachukia Waislamu? au kama hilo ni gumu unaweza ukauliza tu jingine linalohusu mawazo ya Nyerere kuhusu kina Aziz, Sykes na kumbukumbu zake za Nyerere na Abdulwahi Sykes kwa mfano. Akupe tu picha ya upande huu mwingine kwa maoni yako. Unafikiri kuna mtu alikuwa anamjua Nyerere zaidi kuliko mke wake?
 
Naona unajipa shida ya bure tu maneno yote mawili yanahusiana na asili yake ni moja na labda wewe huyajui maana yake na kuweza kuyatofautisha vizuri. Ningetaka kutumia neno "critique" ningelitumia nililolitumia ndio nalimaanisha. Halafu kushambuliwa sidhani kama mna uwezo huo.

There is your problem ndugu critique sio sawa na criticism. Critique is a serious examination and judgement of something. Criticism is a disapproval expressed by pointing out faults or shortcoming of someone. Wasomi wanacritique na sio criticism. Kama unataka kutoa mapungufu ya Mohamed Said leta nondo za kukosoa hayo na sio dhana zako na mitazamo yako.
 
Do it if you can, ntakugaragaza, chagua mada yoyote uipendayo na kwa masharti yoyote uyatakayo na kwa lugha yoyote uijuayo. Nakuambia huniwezi, sharti langu ni moja tu, funguwa nyuzi ya pekee, usitafute pakutokea humu kwenye mada ya Mohamed Said.

Mbona nimeshakuambia kuwa wewe hiyo heshima ya kujadiliana nami huna katika kiwango hicho. Labda ukiendelea kujionesha unaweza kuendesha mjadala wa kiakili naweza kukaa nawe tukajadiliana. Lakini so far sijaona kama una uwezo wa kukaa nami kujadiilana. Ila kama ni mipasho na vitimbi ni wazi uko katika ligi yako mwenyewe sikuwezi huko.
 
Mwenyewe yupo hapa hajajibu mambo ya kujuaje ntajuaje kama alikuwa ameenda sayari ya Zebaki na Nyerere akiwa Zuhura?

Kwanini nimuulize Mohamed Said wakati yeye keshasema limitation zake? Je uliwauliza wazee wa kigamboni kwanini hawakuwahoji akina Sykes na wengineo? Mwanakijiji vp mbona unakimbia?
 
There is your problem ndugu critique sio sawa na criticism. Critique is a serious examination and judgement of something. Criticism is a disapproval expressed by pointing out faults or shortcoming of someone. Wasomi wanacritique na sio criticism. Kama unataka kutoa mapungufu ya Mohamed Said leta nondo za kukosoa hayo na sio dhana zako na mitazamo yako.

embu tafuta hiyo dictionary na weka maana ya hayo maneno mawili... maana ukitaka semantics I'm very good at it too..
 
aah Nyerere alikuwa anachuki na Uislamu au alikuwa anachukia Waislamu? au kama hilo ni gumu unaweza ukauliza tu jingine linalohusu mawazo ya Nyerere kuhusu kina Aziz, Sykes na kumbukumbu zake za Nyerere na Abdulwahi Sykes kwa mfano. Akupe tu picha ya upande huu mwingine kwa maoni yako. Unafikiri kuna mtu alikuwa anamjua Nyerere zaidi kuliko mke wake?

Hivi unafahamu msemo unaosema birds of same feathers fly together??? Unajua kuwa rafiki yako wa karibu anakujua zaidi kuliko hata mkeo. Especially yule mlieshibana naye? Kama umeoa mkuu utafahamu kwamba kuna mambo mengine huwezi kumwambia mke mathalani mfano ukipatwa na matatizo fulani ambayo unayamudu ni aghlabu sana kwa wanaume kuwaambia wake zao mpaka pale akiwa hana jinsi kwa kuhofia mkewe asianze kupatwa na wasiwasi na kupanic? Did you ever asked yourself that?
 
Faiza,

Sikuwa nikiamini kwamba unaweza kuwa muongo kiasi hiki! Ile post yangu iko vile vile wala haijabadilishwa na wewe kuna mahali ulini quote wakati ukijaribu kujenga hoja yako. Sasa unataka kunishangaza kwamba hata yale uliyoyaandika kwa mkono wako mwenyewe yamebadilishwa, na nani??

Kimsingi ni kwamba katika ile hoja ya Nyerere kuwaunganisha wazee wako na wa maeneo mengine ya Tanganyika hukuwa umeielewa ama kama uliielewa ulikuwa unafanya kusudi kuipotosha ndipo nikaendelea kutoa ufafanuzi ili unielewe. Sasa ulipoona umeshindwa hoja ukakimbilia kusema kuna maneno yameongezwa. Huo ni uongo wa mchana na ni aibu kwa mwanamke wa kiislamu kuongopa. Katika hili unatakiwa uone aibu na umuogope japo muumba wakjo kama huwezi kuwaheshimu binadamu wenzako!

Huyo nani simjui, mtajua nyinyi mliochakachuwa au kusaidiana kuchakachuwa. Uongo si sifa yangu. Lakini kama mdomo wako umeamuwa iwe hivyo sina cha kuunyamazisha. Ukweli ndio huu.
 
Ngoja nikupeni siri yangu kwa nini mimi nimejaaliwa kujua mengi ninayokuhadithieni.

Abdulwahid Sykes ana mwanae anaitwa Ebby (huyu ni baba yake Dully Sykes mwanamuziki).

Ebby kazaliwa leo mie nikazaliwa kesho yake. Tena cha ajabu kitanda alicholala mama yake Ebby
akazaliwa Ebby ndicho alichokuja kulala mama yangu nikazaliwa mimi.

Hospitali tulozaliwa ilikuwa pale karibu na Traffic Police.

Sasa akina mama wakitoka kwa Bwana Abdu kumuangalia mzazi wanakuja kwetu kumona mama
yangu.

Mimi na Ebby tunaitana ndugu. Nyumbani kwao ni nyumbani kwetu wala sikujua kuna siku niliyokuwa
naelezwa na wazee wangu yatakuja kuwa na umuhimu kwa kiasi hiki.

Mohamed
 
embu tafuta hiyo dictionary na weka maana ya hayo maneno mawili... maana ukitaka semantics I'm very good at it too..

Chukua dictionary unayoijua wewe soma tofauti ya maneno hayo! Criticism is used informally kama critical evaluation of someone's work (constructive criticism) but formally ni kama describing one's fault or shortcomings. Critique is critical evaluation of someone's work na sio kukosoa.
 
What if they are both right (wazee wa kigamboni na Mohamed Said). Unajuaje pengine Mohamed Said alikuwa hana access kwa Nyerere au Nyerere hataki kuongea nae? Umejuaje, kama Mama Maria naye hataki kuongea na Mohamed Said? Umejuaje wazee wa kigamboni waliandika historia kwa maamrisho ya state house? Matokeo yake wakaandika historia ya superman Nyerere? Hizo ndio limitation na mapungufu ya utafiti ambao wewe au mtu mwengine anaweza kuuendeleza zaidi tukafaidika. Nakuhamasisha uuendeleze utafiti mkuu ili tujifunze zaidi.

Mdondoaji,
Wakati mwingine mnajaribu kujenga hoja kumuunga mkono Sheikh Mohamed hadi mnamharibia bila kujua.

Sheikh Mohamed hajasema kwamba hakuwa na access na Nyerere, na hajasema kwamba Nyerere alikataa kuongea nae. Sheikh Mohamed hajasema kwamba ameshindwa kumhoji mama Maria na hajasema kwamba mama Maria amekataa kuongea nae.

Sheikh Mohamed ameandika hapa kwamba atatufahamisha jinsi kitabu chake kilivyomfikia Nyerere, na alitoa comment gani baada ya kukisoma.

Sasa mkuu hizi assumptions unazitoa wapi ikiwa mhusika mwenyewe yupo hapa na hajasema hivyo?? tatizo hapa unatafuta ushindi badala ya kutafuta facts!
 
Mbona nimeshakuambia kuwa wewe hiyo heshima ya kujadiliana nami huna katika kiwango hicho. Labda ukiendelea kujionesha unaweza kuendesha mjadala wa kiakili naweza kukaa nawe tukajadiliana. Lakini so far sijaona kama una uwezo wa kukaa nami kujadiilana. Ila kama ni mipasho na vitimbi ni wazi uko katika ligi yako mwenyewe sikuwezi huko.

Huna dear. Tafuta pakutokea, nyundo zimekukolea. Basi usiendelee kujitamba kuwa unaweza kumchallenge yoyote, wengine ligi zetu huziwezi kama ulivyokiri hapo kwenye nyekundu. Usite (nimekuheshimu sana kukwambia "usite" neno lake hapo lilikuwa "ukome") ku challenge watu usiowajuwa. Si ki elimu wala kiufahamu hunipati hata robo.
 
Hivi unafahamu msemo unaosema birds of same feathers fly together??? Unajua kuwa rafiki yako wa karibu anakujua zaidi kuliko hata mkeo. Especially yule mlieshibana naye? Kama umeoa mkuu utafahamu kwamba kuna mambo mengine huwezi kumwambia mke mathalani mfano ukipatwa na matatizo fulani ambayo unayamudu ni aghlabu sana kwa wanaume kuwaambia wake zao mpaka pale akiwa hana jinsi kwa kuhofia mkewe asianze kupatwa na wasiwasi na kupanic? Did you ever asked yourself that?

Mdondoaji, huyu anaejitambulisha kama Mzee Mwanakijiji, maji yako shingoni nae hana pakutokea, nyundo za Mohamed Said zimemuingia na sasa anakubali kuwa kajifunza mengi sana, nakuomba usimpe fursa kwa kumbadilishia mada, ndio anapopataka huko pakutokea. Mrudishe kwa Mohamed Said kwa kuwa yeye mwenyewe kaomba kupewa darsa kwa sasa.
 
Mdondoaji,
Wakati mwingine mnajaribu kujenga hoja kumuunga mkono Sheikh Mohamed hadi mnamharibia bila kujua.

Sheikh Mohamed hajasema kwamba hakuwa na access na Nyerere, na hajasema kwamba Nyerere alikataa kuongea nae. Sheikh Mohamed hajasema kwamba ameshindwa kumhoji mama Maria na hajasema kwamba mama Maria amekataa kuongea nae.

Sheikh Mohamed ameandika hapa kwamba atatufahamisha jinsi kitabu chake kilivyomfikia Nyerere, na alitoa comment gani baada ya kukisoma.

Sasa mkuu hizi assumptions unazitoa wapi ikiwa mhusika mwenyewe yupo hapa na hajasema hivyo?? tatizo hapa unatafuta ushindi badala ya kutafuta facts!

Mkuu,

Nakushauri hebu msome Mohamed Said vizuri. Kwa kukusaidia alishasema kuna mtu alimuahidi kuwa wataandaa makutano ya yeye Mohamed na Nyerere. Mkutano huo haukumaterialise. Kuna sehemu pia nimesoma kuna mwengine alimuahidi mkutano na Mama Maria mkutano haukumaterialise. Hayo ndio mapungufu ya utafiti kwani hata unapoandaa questionaires au interviews kuna watakaojibu na wengine hawajibu au kutokupa kabisa interview. Nakushauri msaidie basi Mohamed Said apate interview na Mama Maria ufurahi roho yako !!!!!!
 
Mdondoaji, huyu anajitambulisha kama Mzee Mwanakijiji, maji yako shingoni nae hana pakutokea, nyindo za Mohamed Said zimemuingia na sasa anakubali kuwa kajifunza mengi sana, nakuomba usimpe fursa kwa kumbadilishia mada, ndio anapopataka huko pakutokea. Mrudishe kwa Mohamed Said kwa kuwa yeye mwenyewe kaomba kupewa darsa kwa sasa.

Point taken,

Wacha nimwachie bahari lake Sheikh Mohamed aendelee. Bahati mbaya mie historia ni somo sikuwapo sana mshabiki ijapokuwa nina msonge wake sekondari. Ila bahari hii mimi sifai wacha niwe msomaji. Endeleeni Faiza Foxy na Sheikh Mohamed Said na Mwanakijiji mie kuanzia sasa ni msomaji. By the way yuko wapi Mag3 amekimbia?
 
Back
Top Bottom