Jasusi,
Nizue uongo ili iweje?
Mangapi ya ukweli hata nione hayatoshi nijazie kwa uzushi?
Kama kuaminika wengi wameniamini sina sababu ya kusema uongo.
Isitoshe hilo la nyaraka zilizopotea si mimi peke yangu ninalolijua ukipenda
fika Maktaba ya CCM Dodoma, TNA Dar es Salaam na wewe ufanye utafiti.
Mswada wa historia ya TANU aloandika Abdu na Dr Kleruu si umeibiwa hapo
hapo?
We ukiyajua haya? Au na hili nasema uongo?
Mohamed
Mie naomba kuuliza Sheikh Mohamed. Pengine hili swali liko vichwani mwa wengine je hizo page ulizoziona zimenyofolewa uliwauliza wahusika mbona kuna page zinamiss katika maktaba? Kama ni muswada uliwaulizia wahusika kama wanaweza kukupatia maelezo ya kwanini vimekosekana au kupotea? Nataka kufahamu zaidi.