Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Jasusi,

Nizue uongo ili iweje?

Mangapi ya ukweli hata nione hayatoshi nijazie kwa uzushi?
Kama kuaminika wengi wameniamini sina sababu ya kusema uongo.

Isitoshe hilo la nyaraka zilizopotea si mimi peke yangu ninalolijua ukipenda
fika Maktaba ya CCM Dodoma, TNA Dar es Salaam na wewe ufanye utafiti.

Mswada wa historia ya TANU aloandika Abdu na Dr Kleruu si umeibiwa hapo
hapo?

We ukiyajua haya? Au na hili nasema uongo?

Mohamed

Mie naomba kuuliza Sheikh Mohamed. Pengine hili swali liko vichwani mwa wengine je hizo page ulizoziona zimenyofolewa uliwauliza wahusika mbona kuna page zinamiss katika maktaba? Kama ni muswada uliwaulizia wahusika kama wanaweza kukupatia maelezo ya kwanini vimekosekana au kupotea? Nataka kufahamu zaidi.
 
Asante sana sheikh mohamed,

Ndio sababu nilimuuliza Maranya je mtu mzima akiwa hajataka kuonana na wewe hufahamu tu jibu lake? Huu msumari ni hatari Mohamed unalo la kujitetea Maranya?

Mdondoaji,

Nijitetee kwani nimeshitakiwa? Tofauti iliyopo kati yangu na wewe ni kwamba mimi sishindani na mtu hapa. Tangu mjadala huu umeanza tumekuwa tukijibishana kwa kuangalia ukweli. Hata faiza alitaka kugeuza mnaksha huu kuwa sehemu ya mashindano nikamwambia mimi siko hapa kushindana na mtu yeyote.

Kusema kwamba anajua majibu atakayoyatoa mama Maria kutokana na haya anayoyasimulia nadhani si sahihi hata kidogo. Huku ni kujaribu kumuwekea maneno mdomoni, na hilo siwezi kuliamini hata kidogo. Kwa kuzingatia muktadha huu ambapo Nyerere (marhum) na Abdulwahid (marhum) ndio wahusika wakuu katika hii historia inayodaiwa kupotoshwa, ukimuhoji mtu wa upande mmoja, awe shangazi, dada, kaka, mjomba ama mtoto ni dhahiri atavutia upande wake. Lakini wakihojiwa pande zote mbili na majibu yao yakaletwa barazani, hapo ndipo tutapata nafasi ya kuchambua pumba na mchele toka kwa pande zote mbili.

Hili ni muhimu kwakuwa Sheikh mohamed anaposema kwenda kumnhoji mama Maria ni kumfedhehesha, sitoshangaa akisema hakwenda kumhoji Nyerere kwa kuhofia kumfedhehesha!! Si jambo lenye afya sana kwa mnakasha huu ku-rely kwenye mazungumzo yaliyosimuliwa na watu ambao sasa ni marhum. Kwanini tusiwatumie wale wangali hai ili kuondoa uwezekano wa kupindisha mambo na kujenga taswira ya kutoaminiana?? kwanini tuamini yale tu yaliyosimuliwa na watu ambao tayari ni marhum??
 
Tuchukulie basi imepotoshwa na kusema uongo. Unajua examination ya utafiti inafanywaje mkuu? Wanatoka watu na kwenda kufatilia vyanzo vya habari ya ndugu Mohamed Said kujua yasemwayo kweli au uongo? Na vile vile kuulizia the opposite side wanasemaje? Sasa mie nakushauri chukua makala za Mohamed Said wapelekee wazee wetu wa Kigoda cha Mwalimu, au Mama Maria ili wakanushe yanayosemwa. I do not defend Mohamed ila mkuu usimhukumu mtu kwanza kabla hujafanya utafiti. Nakushauri fanya utafiti kwanza halafu uje na maafikiano haya unayosema wewe
 
MM,

Ngoja nikufahamishe mimi nimekuja vipi kuelewa haya.

Kwanza kabisa "infusion" wazee wanaeleza habari za zamani nami nipo nasikiliza.

Kisha nikaja kufanya utafiti.

Ndiyo maana style ya maandiko yangu ni "autobiographical approach"
yaani yale niliyoeleza na mimi ndani nimo.

Hili la Mama Maria nakuombeni tuliache si muhimu sana isipokuwa ni kuwa upasi ulianza mwaka 1963 baada ya Nyerere pambana na Sheikh Hassan na Bilali Rehani Waikela. Ugomvi ule ukaja hitimishwa kwa Sheikh Hassan bin Amir kukamatwa na kufukuzwa Bara na Waikela kuwekwa kizuizini.

Ikafuatia kukamatwa na masheikh na kutiwa kuzuizini na mmoja wa waliokamatwa ni jamaa yake Abdulwahid Sykes, Maalim Matar.

Lakini kubwa na pale Waislam walipobaini kuwa sasa Nyerere keshakalia kiti hana haja na kuungwa mkono na Waislam wala akina Abdu au Dossa.

Hazina ya serikali imo mikononi mwake hana haja na vile vijipesa vyao na aliwahi katika hotuba moja kusema wakati wa kuwategemea watu umepita.

Ujumbe ukawa umewafikia wazee wangu "loud and clear" na wao kwa uungwana wakakaa pembeni hadi walipoondoka duniani.

Na historia yao yote kama mlivyoisoma hapa ukumbini ikawa imefutwa.

Mama Maria anayajua yote haya.

Sasa ungependa nimuhoji kuhusu haya? Ili iwe uthibitisho au kitu gani?

Mohamed
 
Sheikh Mohammed basi..utaliza wengi humu ndani. Yaani Nyerere huyuhuyu kisha asema kama hakumbuki Abdul alikuwa na nafasigani katika TAA!!! hii sasa kufru.
Hivi kweli mnaweza kutuwekea hapa nukuu yoyote au hata sauti ya Nyerere akisema kuwa hakumbuki Abdul alikuwa na nafasi gani katika TAA? Hizi ndizo ninazoita "hearsay" zenye lengo la kumchafua tu Nyerere.
 
Tuchukulie basi imepotoshwa na kusema uongo. Unajua examination ya utafiti inafanywaje mkuu? Wanatoka watu na kwenda kufatilia vyanzo vya habari ya ndugu Mohamed Said kujua yasemwayo kweli au uongo? Na vile vile kuulizia the opposite side wanasemaje? Sasa mie nakushauri chukua makala za Mohamed Said wapelekee wazee wetu wa Kigoda cha Mwalimu, au Mama Maria ili wakanushe yanayosemwa. I do not defend Mohamed ila mkuu usimhukumu mtu kwanza kabla hujafanya utafiti. Nakushauri fanya utafiti kwanza halafu uje na maafikiano haya unayosema wewe

Mdondoaji,

Mama Maria siku alipofikishiwa taarifa za kifo cha Abdu alianguka akapoteza fahamu.

Unajua Nyerere alikuwa na dada yake anaitwa Sophia ni marehemu. Huyu mama aliolewa
na Lawrence Gama.

Basi Bwana Abdu kwa mapenzi aliyokuwanayo kwa Sophia alikuwa haipiti siku mbili tatu atakwenda
kumjulia hali na gari yake kwenye buti katika vitu kwa ajili ya watoto wa Sophia.

Watoto wa Gama ni wakubwa sasa bila shaka wanakumbuka "Uncle Abdu." Wote hawa
wakija kwa Bi Mluguru pale Kirk Street. Mimi pale nikenda kumfuata 'pacha mwenzangu" Ebby.

Nimelisema hili sikutaka lakini nia ni kukufahamisha hawa mie nawajua ni wazee wangu.

Siku hizo Abdu anaendesha Mercedes Benz.

Mohamed
 
Jasusi,

Nashukuru kuwa hata wewe imekuingia simanzi. Mkanda uko TBC utafute uusikize.

Kaeleza kisa kizima kakutana vipi na Abdu kamtaja Kasella Bantu ndiye aliyempeleka ila hakusema kuwa mkononi alikuwa na barua ya Hamza Mwapachu kutoka Cardiff amletee Abdu Sykes.

Mohamed
 
Mie naomba kuuliza Sheikh Mohamed. Pengine hili swali liko vichwani mwa wengine je hizo page ulizoziona zimenyofolewa uliwauliza wahusika mbona kuna page zinamiss katika maktaba? Kama ni muswada uliwaulizia wahusika kama wanaweza kukupatia maelezo ya kwanini vimekosekana au kupotea? Nataka kufahamu zaidi.

M,

Walisema wanahisi ni "foul play."

Mohamed
 
Mdondoaji,

Nijitetee kwani nimeshitakiwa? Tofauti iliyopo kati yangu na wewe ni kwamba mimi sishindani na mtu hapa. Tangu mjadala huu umeanza tumekuwa tukijibishana kwa kuangalia ukweli. Hata faiza alitaka kugeuza mnaksha huu kuwa sehemu ya mashindano nikamwambia mimi siko hapa kushindana na mtu yeyote.

Kusema kwamba anajua majibu atakayoyatoa mama Maria kutokana na haya anayoyasimulia nadhani si sahihi hata kidogo. Huku ni kujaribu kumuwekea maneno mdomoni, na hilo siwezi kuliamini hata kidogo. Kwa kuzingatia muktadha huu ambapo Nyerere (marhum) na Abdulwahid (marhum) ndio wahusika wakuu katika hii historia inayodaiwa kupotoshwa, ukimuhoji mtu wa upande mmoja, awe shangazi, dada, kaka, mjomba ama mtoto ni dhahiri atavutia upande wake. Lakini wakihojiwa pande zote mbili na majibu yao yakaletwa barazani, hapo ndipo tutapata nafasi ya kuchambua pumba na mchele toka kwa pande zote mbili.

Hili ni muhimu kwakuwa Sheikh mohamed anaposema kwenda kumnhoji mama Maria ni kumfedhehesha, sitoshangaa akisema hakwenda kumhoji Nyerere kwa kuhofia kumfedhehesha!! Si jambo lenye afya sana kwa mnakasha huu ku-rely kwenye mazungumzo yaliyosimuliwa na watu ambao sasa ni marhum. Kwanini tusiwatumie wale wangali hai ili kuondoa uwezekano wa kupindisha mambo na kujenga taswira ya kutoaminiana?? kwanini tuamini yale tu yaliyosimuliwa na watu ambao tayari ni marhum??

Wewe upo hapa kuuharibu mnakasha na ndio maana nikakwambia uhodari sana na umeshinda.

Mdondoaji, hawa wote wanafanya hila za mjadala husika uonekane hauna maana kwa kuleta ubishi usio na mpango, bado hujawastukia tu? achana na kubishana nao, hawa ni kuwaswaga machinjioni tu, wameshasikia harufu ya damu. Mchinjaji kwa "Nyundo" yupo, tuwaswage kule tu.

Nimewastukia zamaaani, ndio maana nikawaambia "sidanganyiiiki".
 
Tuchukulie basi imepotoshwa na kusema uongo. Unajua examination ya utafiti inafanywaje mkuu? Wanatoka watu na kwenda kufatilia vyanzo vya habari ya ndugu Mohamed Said kujua yasemwayo kweli au uongo? Na vile vile kuulizia the opposite side wanasemaje? Sasa mie nakushauri chukua makala za Mohamed Said wapelekee wazee wetu wa Kigoda cha Mwalimu, au Mama Maria ili wakanushe yanayosemwa. I do not defend Mohamed ila mkuu usimhukumu mtu kwanza kabla hujafanya utafiti. Nakushauri fanya utafiti kwanza halafu uje na maafikiano haya unayosema wewe

Mdondoaji,

Nakuelewa unachosema, lakini usisahau kwamba si wote tulioko hapa ni wanahistoria. Kuna wengine ni madaktari(MD), kuna wahandisi, kuna wachumi, kuna waalimu,n.k, n.k

Kwakuwa sheikh mohamed ni mwanahistoria na mtafiti, ndio maana nikadhani angeweza kutusaidia hilo. Kwahiyo utaona kwamba nilikuwa simhukumu mtu bali nilikuwa natoa chagizo tu ili tufike mahali, ukweli udhihiri na hatimaye tuukate mzizi wa fitna.
 
Tawire mkuu au kwa jina lengine ni No research no right to speak mkuu au vp? Ila sio mbaya ukatupatia elimu yake ameishia darasa la ngapi au degree ya ngapi. Fahamu kuwa enzi zile ukijua kuongea kiingereza tu unakuwa mwalimu. Ukiwa mstaarabu unajua kuvaa vizuri basi unakuwa tarishi. Hebu tupatie elimu yake mkuu tutashukuru sana!!!
Ninachojua Mama Maria alisoma Uganda, na kabla ya kuolewa alifundisha shule ya wasichana Moshi. Sidhani kama alikuwa na elimu ya University lakini alikuwa na elimu ya kutosha kufundisha Moshi--enzi hizo ukimaliza darasa la kumi na kwenda teacher's college unapsngiwa kufundisha Middle School level. Na wakati Mwalimu alipokuwa Edinburgh mama Maria alichukua kozi ya Kiingereza St. Joseph's Dar-es-Salaam.
 
Wewe upo hapa kuuharibu nakasha na ndio maana nikakwambia uhodari sana na umeshinda.

Mdondoaji, hawa wote wanafanya hila za mjadala husika uonekane hauna maana kwa kuleta ubishi usio na mpango, bado hujawastukia tu? achana na kubishana nao, hawa ni kuwaswaga machinjioni tu, wameshasikia harufu ya damu. Mchinjaji kwa "Nyundo" yupo, tuwaswage kule tu.

Nimewastukia zamaaani, ndio maana nikawaambia "sidanganyiiiki".

Kama umeishiwa cha kusema ni bora ukae kimya. Kama unatafuta mashindano katafute mwingine. Mimi sihitaji kushindana hapa na mtu yeyote.
Nyie ndo mnaharibu mnakasha halafu mnaanza kusingizia wengine. Sheikh Mohamed yuko hapa, ninamuuliza maswali na anayajibu vizuri, nikionyesha kuwa na wasiwasi mahali popote anaposimulia, anatolea ufafanuzi bila kinyongo, na tunasonga mbele. Sasa sijui ni kitu gani kinachokuwasha.
 
Sawa, nimeishiwa, na huko kwa Mohamed Said ndipo nnapotaka mimi uende. Sina kinachoniwasha, chunga lugha yako. "Message Delivered".
 
mohamed Said,kwa heshima zote, sasa tunaomba utwambie kitabu chako kilimfikia vipi Nyerere na reaction yake ilikuwa vipi? Ni hilo tu.
 
SoA,

Kitabu kilimfikia kupitia mmoja wa vijana ambao wameoa katika familia ya Nyerere.

Huyu kijana alinitafuta tukaonana na akanieleza kuwa yeye alikisoma kitabu na akampelekea Nyerere.

Nyerere akakisoma na akasema kuwa hivi ilivyoandikwa ni sawa hivi ndivyo mambo yalivyokuwa lakini watu hawatamuamini Mohamed Said.

Taarifa nilizopata ni kuwa waliokuwa karibu na Nyerere waliumizwa na kitabu kile khasa ile "aspect" ya mchango Abdu na wa Waislam na wakamsihi na yeye aandike.

Mohamed
 
MM,

Ngoja nikufahamishe mimi nimekuja vipi kuelewa haya.
Kwanza kabisa "infusion" wazee wanaeleza habari za zamani nami nipo nasikiliza.
Kisha nikaja kufanya utafiti.
Ndiyo maana style ya maandiko yangu ni "autobiographical approach"
yaani yale niliyoeleza na mimi ndani nimo.
Hili la Mama Maria nakuombeni tuliache si muhimu sana isipokuwa ni kuwa upasi ulianza mwaka 1963 baada ya Nyerere pambana na Sheikh Hassan na Bilali Rehani Waikela. Ugomvi ule ukaja hitimishwa kwa Sheikh Hassan bin Amir kukamatwa na kufukuzwa Bara na Waikela kuwekwa kizuizini.
Ikafuatia kukamatwa na masheikh na kutiwa kuzuizini na mmoja wa waliokamatwa ni jamaa yake Abdulwahid Sykes, Maalim Matar.
Lakini kubwa na pale Waislam walipobaini kuwa sasa Nyerere keshakalia kiti hana haja na kuungwa mkono na Waislam wala akina Abdu au Dossa.
Hazina ya serikali imo mikononi mwake hana haja na vile vijipesa vyao na aliwahi katika hotuba moja kusema wakati wa kuwategemea watu umepita.
Ujumbe ukawa umewafikia wazee wangu "loud and clear" na wao kwa uungwana wakakaa pembeni hadi walipoondoka duniani.
Na historia yao yote kama mlivyoisoma hapa ukumbini ikawa imefutwa.

Mama Maria anayajua yote haya.

Sasa ungependa nimuhoji kuhusu haya? Ili iwe uthibitisho au kitu gani?

Mohamed

Sheikh Mohamed, ahsante kwa ufafanuzi wa hoja. Na hilo la mama Nyerere nimekubali tuachane nalo, hadi hapo nimekusoma.

Lakini nina machache ya kusema hapa;
Kama kumbukumbu yangu iko vizuri, Farka kati ya Nyerere na akina sheikh hassan na waikela pamoja na mambo mengine lilikuja baada ya kupitishwa uamuzi wa kulivunja baraza la wazee wa TANU. Na uamuzi wa kulivunja baraza la wazee wa TANU ulifikiwa na kamati kuu ya TANU ambayo nilikuuliza kama unaweza kutufahamisha wajumbe wake walikuwa ni akina nani, ukasema unahitaji kufanya utafiti.

Kwakuwa watu waliowekwa kizuizini ama kupelekwa nje ya nchi kwa majukumu mengine ama kutoroka wao wenyewe katika miaka hiyo ni wengi na hawakuwa waislamu peke yao, kulikuwa na wakristo wenzake pia. Hapo ninapata ukakasi kukubali moja kwa moja kwamba Nyerere alikuwa na agenda ya dhulma dhidi ya waislamu, kama una ushahidi mahsusi unaweza kunifahamisha.

Hili la kukataa kupokea michango ya fedha toka kwa wapigania uhuru wenzake, mimi naliona kama halikuwa suala la kuwatenga waislamu, bila shaka wale wote waliokuwa wakichanga fedha kwa ajili ya shughuli za TANU hawakuendelea kuchangia tena, kwakuwa sasa TANU iko madarakani na ina vyanzo vingine vya mapato. Labda kama kuna uthibitisho kwamba Nyerere aligoma kupokea fedha za wazee wako lakini wakati huo huo akawa anapokea fedha kutoka kwa wakristo wenzake.

Hata baada ya Nyerere kuondoka madarakani tumeshuhudia baadhi ya watanzania wanavyowekwa kizuizini na serikali yao kwa sababu tu ya kuhitilafiana misimamo juu ya mambo fulani fulani, bila kujali dini zao ama kabila zao(Viongozi wakuu wa CUF ni mfano wa hivi karibuni kabisa). Kwahiyo naona kwamba serikali yoyote lazima itawashughulikia watu "wowote" inaodhani kwamba wanakwenda kinyume na taratibu zilizopo.
 
Sawa, nimeishiwa, na huko kwa Mohamed Said ndipo nnapotaka mimi uende. Sina kinachoniwasha, chunga lugha yako. "Message Delivered".

Nilikusoma ulivyokuwa unamtisha mzee mwanakijiji, sasa sijui hapa niseme kwamba unajaribu kunitisha ama ndio unanitisha? je una uhakika kwamba na mimi huwa ninatishwa? na kwamba nikitishwa huwa natishika? usivamie pori usilolijua! utaliwa na simba kweupeeeee!!
 
Duuh! pole sana Da Faiza...hii ndio JF tuliyoizoea na mamodereta wetu. Kwa taarifa tuu huyu Mwanakijiji yeye pia no modereta na anauwezo wakufanya yoote hayo aliyoyafanya. We have been here for longtime na hii ndio ''organisation behaviour '' yetu..tartiiibu utatueelewa. Hii posts kufutwa au kunyofolewa ..n.k. muuliza sana the famous '' Malaria Sugu'' atakupa khabari zake.

Nayajuwa hayo, si ndio maana nawaambia hawana ufahamu hata robo ya nilionao. Na nilishawaambia humuhumu, hivi wakifanya hivyo huwa wanazisuta nafsi zao? kitu ambacho hawawezi. Hao ndio katika wale wanaofanya vitendo visiwe na wanaadam na si kuzikonga nafsi zao wenyewe kwanza, huwa nafsi zinawasuta hawana raha na chochote kwa kuwa zimejaa msuto wandani kwa ndani basi kila wanaloambiwa wao huanza kwa kujisuta kwanza kabla hata ya kulitia maanani. Usijali nawafaham sana, na wao wananijuwa sana.
 
Back
Top Bottom