Mag3 nakurudisha tena kwenye maswali yangu, tafadhali nijibu ili tuendelee, kama ulikosea, japo ukiri makosa na uombe msamaha, maana naona mpaka sasa huna jibu licha ya majibu:
Nakurudisha tena kwenye maswali yangu, tafadhali nijibu ili tuendelee:
1) Naomba tuonyeshe ni wapi hoja imefinyangwafinyangwa.
2) Huyo hajiiti, bali sisi ndio humuita jina lake alilopewa kwao. Hivi wewe hujiita mwenyewe?
Twende taratibu tutafika. Usinijazie mlolongo wa maandishi mpaka nikashindwa kukuelewa ndio maana nafupisha "nondo" zako ili tuzichambuwe kwa raha kabisa.
FaizaFoxy, tofauti na wewe mimi ni binadamu nahitaji kulala, nahitaji kupumzika na nahitaji kufanya kazi na katu si kuwa hapa JF masaa ishirini na nne. Tofauti na wewe, mimi nasukumwa na mapenzi yangu kwa taifa langu ninalolipenda na nawaenzi watu wote waliopigania uhuru wa nchi hii bila kubaguana kidini, kikabila wala kirangi. Naomba hapo tuelewane kwanza.
Pili mchochezi Mohamed Said ambaye ametanguliza chuki dhidi ya Watanzania wenzake kwa sababu tu wanatofautiana kidini mimi sina muda wa kujibizana naye, sasa hapa kisichoeleweka ni kitu gani ? Ninapoingia JF sikurupuki tu nikaanza kujibu mipasho ya Gerezani na mtaa gani vile alikozaliwa FaizaFoxy !
Hapana, nachukua time kusoma maoni mbali mbali halafu nachagua yapi ya maana niyajibu na yapi ni porojo zisizoweza kutusaidia Watanzania kulijenga taifa letu. Tofauti na wewe mimi sipewi briefing (kama una akili kidogo utanielewa) lakini kama akili yako yote imejaa udini nakupa tu pole lakini nakuhakikishia Watanzania walio wengi hata mihadhara ya Mohamed ikifanyika 24/7, watayapima na kuyatafakari kabla ya kuyameza.
Unaniuliza ni yapi yanafinyangwa na mchochezi Mohamed Said mtoto wa Gerezani na huku unajua wazi kuwa simulizi zake zinatokana na hadithi alizosimuliwa na wazee wake. Sisi tuliozaliwa nyakati hizo ilikuwa ni kawaida vijana kukaa na wazee wao wakisikiliza hadithi ambazo nyingi zilihusu mashujaa enzi zao kwa hivyo hadithi za Mohamed Said hazina tofauti na hizo tulizozisikia wengine.
Labda tujiulize ni wapi hadithi inaacha kuwa hadithi na kugeuka historia.
Huko ndiko kufinyangwa ninakoelezea, hadithi inalazimishwa kuwa historia lakini kwa lengo kuu la kuleta machafuko na uhasama miongoni mwa jamii ya Watanzania. Hadithi za Wazee wa Mohamed zinalazimishwa kuwa historia ya Tanganyika, duh ! hapa mimi siwezi kuwa na simile, nitapinga na nitatumia uwezo wangu mdogo kuutetea ukweli dhidi ya hizo porojo za Mohamed na Wazee wake wa Gerezani.
Nimeeleza kuwa wazee wa Mohamed hawakujulikana nje ya Dar es Salaam na shahidi wangu ni mimi kwa sababu sikusimuliwa, nilikuwepo. Huko tuliyasikia majina kama Zuberi Mtemvu, Christpoher Kasanga Tumbo, Paul Bomani na wengineo lakini Sykes ? No, never. Sana sana baadaye sana nilishangaa jinsi huu ukoo wa Sykes ulivyopewa upendeleo maalum kwenye nyanja mbali mbali kama biashara na makazi.
Halafu leo anatokea huyu mchochezi na kudai Mwalimu Nyerere aliwakandamiza Waislam kwa chuki zake dhidi ya Uislaam na mfano eti ni huo ukoo wa Sykes. Sasa hapa ukoo wa Balozi Kasanga Tumbo utasemaje ? Huyu shujaa pamoja na madhara aliyopata, nafasi ya kuipinga CCM waziwazi ilipotokea tu mwaka 1992, alikuwa moja wa waanzilishi wa mageuzi. Je ukoo wa Sykes ulikuwa wapi ?
Mtoto wa Kasanga Tumbo hivi sasa yuko kwenye mapambano dhidi ya mfumo fisadi wa CCM, yuko wapi mtoto wa Sykes katika haya mapambano ? Je ni udini au ni kwa sababu ya fadhila walizopewa wazazi wake na serikali za TANU/CCM ? Wana JF Mohamed Said ni mtu hatari katika jamii kwani hivi sasa wazalendo wa kweli wanapigania haki na usawa (katiba mpya), yeye amejikita katika kuchochea mifarakano ya kidini.