FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Ndio maana nashindwa kujibizana na watu wa aina yako na hii itakuwa mara yangu ya mwisho kurespond kwa hizi hoja za kipuuzi na kwangu anayezileta nina jina moja tu kwake, ni mpuuzi, period. Unajua wakazi wengi wa Dar es Salaam waliishi kwenye nyumba za aina gani wakati tunapata uhuru ? Unajua nyumba za mbavu za mbwa kama alivyoziita Al Haji Ali Hasan Mwinyi ? Hapo nyuma nimekuuliza kama unaijua "Operation Makuti" ilifanyika wakati gani na lengo lake lilikuwa nini. Je unajua sura ya Dares Salaam ilivyobadilika katika kipindi cha miaka mitano baada ya uhuru ? Tuchukue mfano mdogo tu wa Magomeni;
Unajua mitaa ya Uweje, Idrisa, Sikukuu n.k ilivyokuwa wakati wa uhuru na ilivyoweza kubadilika miaka mitano baadaye. Unajua mitaa karibu yote iliwekewa lami na hali hii iliwapa shida sana Waswahili waliozoea kuchimba mashimo ya taka barabarani na walivyolalamika kuhusu hizo barabara za lami ? Je unajua hadi public toilets mitaani ilijengwa lakini tabia za uswahilini zikazaa sokomoko nyingine katika utumiaji na utunzaji wake ? FaizaFoxy, usitake twende huko, maendeleo yaliyofanyika Magomeni, Ilala hadi Temeke yalikuwa makubwa lakini watu wake hawakuwa tayari kwa hayo maendeleo.
The bottomline ni kwamba watu wa Dar walikuwa wazito katika kuitikia mabadiliko hasa katika nyanja ya maendeleo. Utalia nikikusimulia jumba la kwanza la DDC lilipojengwa Kariakoo na kuwekewa vyoo vya kisasa. Matengenezo makubwa ilibidi yafanyike baada ya muda mfupi na ramani mpya zitayarishwe kwa sababu wakazi wengi wa Kariakoo walipata taabu ku "cope" na vifaa vingi vya kisasa vilivowekwa humo. Kama kuna kitu kimoja kilichoshusha hadhi ya taifa jipya la Tanganyika ni makao makuu ya taifa kuwa Dar es Salaam. Lakini tusiende huko !
Wewe unataka kunihadithia kwetu? labda mimi ndio nikupe somo, lakini naona Mohamed Said darsa lake umelipata na hukumtaja tena jina, Umegwaya kwani kisha sema ukimtaja jina tu, anashusha Nyundo.
Lingine lote povu. Sisi tumepewa darsa humu, hatutukani.
Dar Es Salaam, mpaka "carnival" tulikuwa nazo kabla ya Nyerere kuja (si kuwa Rais tu), utatueleza nini wakuja?
Hiyo DDC yenyewe unayoisema "Msimbazi" ndio wewe ulipoingia Dar ukakumbana nayo nini? ukaiona ya maana? Unanchekesha.
Maswali yangu kutokana na maneno yako mwenyewe, umeshindwa kuyajibu umekuja povu linakutoka, inaonesha ni vipi una maneno ya kubuni-buni tena yasiyokuwa na maana hata kidogo ndio maana ukiulizwa hayohayo wewe mwenyewe yanakutoa povu na unashindwa kujitetea. Pole sana.
Nachukulia hayo mawili ya mwanzo umeshindwa kuyajibu, nakuja na maswali mengine kutokana na mabandiko yako, natokea kulekule mwanzo, ya huku ntayakuta kama hujayaondoa.
