Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Kuliko unavyoweza kufikiria.

Mwanangu mmoja (mtoto wa kaka yangu) alikuwa anaoa.
Mmoja wa waliotoa hotuba katika harusi ile ni mtoto wa
Mzee John Rupia na yeye na mkewe walikuwa meza kuu.

Mohamed
MS

sasa hapa inakuwa kazi kwa sababu swali langu ni jepesi sana na hujalijibu na umelikwepa kimtindo kabisa - aliyeoa ni mtoto wa kakako (mwanao) na mtoto wa John Rupia alikuwa meza kuu! Haijibu kama unamuona mzee John Rupia mwenyewe kuwa ni miongoni mwa "wazee wako". Sijui niliwekeje ili swali lipate jibu la "ndio" au "hapana" au "kwa kweli sitaki kujibu" au "sijui".
 
Hao unaojidai upo nao karibu hao ndio wamempa Mohamed Said nyaraka nyingi tu za kitabu chake. Leo nani asiyetaka Baba'ke ajulikane mchango wake katika Historia? unashangaza sana.

Jihad (strive hard in any good cause) ni kujitahidi ni nani asiyependa kujitahidi? wewe?

Mag3,

Umerudi na hii "cock and bull story" unadhani wewe unaweza kutia fitna kati yetu.

Babu yangu Salum Abdallah na Kleist walikuwa marafiki wote waajiriwa wa Tanganyika Railways na nyumba zao ziunatazamana pale Kipata.

Bibi yangu Zena bint Farijala na mkewe Kleist Bi Mluguru bint Mussa walikuwa mashoga.

Baba yangu Said Salum na Abdulwahid Sykes umri wao mmoja, mchezo wao mmoja wamesoma darasa moja wamekulia mji mmoja wamefanya mengi pamoja katika utoto hadi ujana wao hadi marehemu Abdu anafariki.

Simu ya taarifa ya kifo cha Abdulwahid Sykes nimepokea mimi baba alikuwa hayupo nyumbani.

Mama yangu marehemu Bi Baya na mama yake Daisy, Bi Mwamvua mke wa Abdu Sykes walikuwa mashoga.

Mjomba wangu Bwana Hamisi kapewa ubao na Abdu Sykes wa kufanya biashara pale sokoni Karikaoo.

Tunazaliwa sisi watoto tunajuana hadi leo tunatembeleana na kuadhimishana sana.

Na sisi tumepata watoto wanaijua historia hii ya udugu uliokuwapo pale Gerezani nk.

Huwezi kutufitinisha hata kidogo na kwa taarifa yako tunapokutana hakuna kitu kinachotawala mazungumzo yetu kama "reminicencing" kuhusu wazee wetu walio mbele ya haki kukumbuka "the days gone by." Tunaimba hadi nyimbo walizokuwa wakipiga wazee wetu kwenye gramaphone zao.

Hawa wazee waliishi kaka yangu usifanye mchezo naweza kuandika kitabu kizima kuhusu watu hawa.

Mohamed
 
sasa hapa inakuwa kazi kwa sababu swali langu ni jepesi sana na hujalijibu na umelikwepa kimtindo kabisa - aliyeoa ni mtoto wa kakako (mwanao) na mtoto wa John Rupia alikuwa meza kuu! Haijibu kama unamuona mzee John Rupia mwenyewe kuwa ni miongoni mwa "wazee wako". Sijui niliwekeje ili swali lipate jibu la "ndio" au "hapana" au "kwa kweli sitaki kujibu" au "sijui".

Mwanakijiji,

You are pretending you cant be this dull.
Or you want to urge for the sake of urguing.

Nguruvi3 nimemshauri apate darsa la "the standard of the reasonable man." Wanaukumbi kama kuna mwanasheria humu please SOS tunahitaji msaada.

Mohamed

Mohamed,
Wa kutusimulia ili tuandike kama wewe hayupo. Hatuna wazee wetu "Wakristo" waliokuwa TAA ambao wako hai sasa. Mimi ni mmoja wa wanaoogopa sana kuwasemea marehemu. Pili, ukianza simulizi kwa kutumia DINI, KABILA, JINSIA,......, inakuwa sio historia tena.
Halafu, wazee wako hawa, Mohamed hawakuwa na mapungufu hata kidogo kama ulivyomwanika Mwalimu?

Ahali yangu si vizuri kudandia treni kwa mbele.

Ni vizuri umsome vizuri sana Sheikh Mohamed said katika maandiko yake na nia yake likuwa ni nini.

Lakini kwa kukusaidia nia na dhumuni ya kundika historia hii ni si kubadilisha historia iliyokuwepo ya tanganyika BALI NA KUANDIKA ILE HISTORIA ILIYOFICHWA NA KUJIFICHA iwe kwa makusudi maalum au kwa bahati mbaya.

Lakini msingi mkuu ni kutujuza.
 
Kuliko unavyoweza kufikiria.

Mwanangu mmoja (mtoto wa kaka yangu) alikuwa anaoa.
Mmoja wa waliotoa hotuba katika harusi ile ni mtoto wa Mzee John Rupia na yeye na mkewe walikuwa meza kuu.

Mohamed
PS: Mwanakijiji hebu niulize maswali ya chemsha bongo haya sasa hayana muhimu katika historia au umechoka? Kama "fatigue" inakunyemelea basi tupumzike sote. Tulochangia hapa jamvini si haba. MS

Hahahahah "Nyundo" zimemlewesha, anaona nyota nyota, si unaona huko juu, mara hii sio historia ni simulizi mara hii ni historia. Ana-haha.

Unajuwa Sheikh Mohamed Said, hii shock si wao tu inaowapata hata sisi Waislaam imetupata kwa kiasi fulani labda sisi imetupata kivingine. Ngoja nikuelezee kwa upande wangu kwa ufupi sana:

Kwanza nnapokisoma ulichokiandika, huwa nnasema hakika Mwenyeezi Mungu ni mwingi wa rehema na shani zote ni zake, huwa nnasema leo angetokea Muislaam mwingine ambae hana mnasaba kabisa na hawa wazee na hakutokea katika jamii na ahli hiyo, sijui hayo matusi yangekuwaje? maana kila wanapotaka kujaribu huwa jibu ni kuwa anaeandika anawafahamu ni wao na anayoyasema ni kweli. Hapo sasa.

Hakuna humu hata mmoja aliyekuja akasema hapana, huyo Mzee uliemtaja hakuwepo na hakuwa na wadhifa huo au hakufanya harakati hizo.

Inayobaki wanaanza, mbona fulani hukumuuliza, mbona fulani hukumuuliza. Hivi ni kweli wao wanashindwa kuwauliza hao wanaowataka wao? Au wanawauliza na majibu ndio hawana pakuyaweka? Hiyo ndio shock inayonipata mimi.

Watu wanakuja na kufanya kila hila kuutowa huu mjadala kutoka kwa wazee na kuupeleka kwenye EPA, wanapoambiwa 83% ni wao, wanaanza kuuliza imetoka wapi, wanashindwa kufanya kautafiti kadogo tu wakaja hapa waseme hapa hiyo asilimia si kweli, asilimia sahihi ni hii hapa kwa ushahidi huu na huu.

Unapowaambia umeiona historia iliyoandikwa Kigamboni na imewasahau wazee waasisi wa AA na TAA na TANU na unapowabainisha kinaga-ubaga, wanashindwa kusema hao wazee si wa ukweli hawakuwepo, kama hilo linawashinda na kweli walikuwepo ni nini zaidi kinachowasumbuwa? Ni rahisi sana kuelewa, ni shock, na masikio yao na bongo zao zimeaminisha kuwa ilikuwa "One man show" sasa kuja kuona si hivyo, inakuwa vigumu sana wao ku "insert" haya ya ukweli.

Shock yangu ni kwanini inawawia vigumu?
 
Kama muislamu anaongoza nchi na unalalamika itakuwaje akiwa mkristu?

atajilipua kwa mabomu kwa hasira, napendekeza Mohamed Said achukue fomu za kugombea urais 2015 ili aweze kuyatatua matatizo haya anayosema maana waislamu wenzako hawaamini.
 
Mwanakijiji,

You are pretending you cant be this dull.
Or you want to urge for the sake of urguing.

Nguruvi3 nimemshauri apate darsa la "the standard of the reasonable man." Wanaukumbi kama kuna mwanasheria humu please SOS tunahitaji msaada.

Mohamed

Anatafuta pakutokea hapaoni, akipata hata ka nyufa au kaupenyo anaona ndio hapahapa, ili mradi haeleweki mara simulizi mara historia mara EPA mara Rupia, tungoje na Riali sasa.
 
Ahali yangu si vizuri kudandia treni kwa mbele.

Ni vizuri umsome vizuri sana Sheikh Mohamed said katika maandiko yake na nia yake likuwa ni nini.

Lakini kwa kukusaidia nia na dhumuni ya kundika historia hii ni si kubadilisha historia iliyokuwepo ya tanganyika BALI NA KUANDIKA ILE HISTORIA ILIYOFICHWA NA KUJIFICHA iwe kwa makusudi maalum au kwa bahati mbaya.

Lakini msingi mkuu ni kutujuza.
Hii ya Mohamed ukiisoma vizuri na kama fasihi yako ya kidato cha nne itakusaidia agenda kubwa hapa ni WAISLAMU na UISLAMU wa Tanzania. Kila tukijaribukumwelesha humu kuwa historia ya nchi hii inaweza ikajisimamia yenyewe bila DINI mzee wetu hataki kuelewa. Anataka WAISLAMU watajwe kwa majina yao matamu ya Kiislamu kama YESU au MTUME MOHAMED( S.A.W,) wanavyotajwa kwenye vitabu vitukufu/vitakatifu.
 
Sio vibaya mtu kutoa mchango wake kwa anachojua kuhusu Historia ya nchi yetu lakini sio vizuri pia kulaumu kuwa historia imepotoshwa makusudi ili kukandamiza kundi fulani. Mi naona tatizo ni kuzingatia tu uandishi bila kuzingatia Historia kama taaluma. Sio killa anayejua kuandika nimtaaalam wa Historia. Kama wanaolalamika kupotoshwa kwa Historia wangejua kuwa kanuni kuu kwamba Historia kamwe haihusiani na kila tukio bali baadhi ya matukio kulingana na mwandishi, na mahitaji ya wakati. Kwa hiyo kuamua lipi liachwe nalipi liwemo kwenye Historia ni maamuzi ya mwandishi au wakati mwingine na ideology ya nchi. Kwa mfano tunaambiwa kuwa wakoloni walitunyonya kwa kutulipisha kodi na walijenga barabara ili kutunyonya. Leo hii matukio hayo yanaitwa maendeleo kulingana na wakati na wa sasa. Twaambiwa shaka alijenga dola ya kizulu kana kwamba alikuwa peke yake au Napoleone aliibadili Ufaransa kana kwamba alikuwa peke yake. Kwamba Kinjekitile alipigana vita vya majimaji alikuwa peke yake? Wanasema historia inahusu matendo makuu ya watu mashuhuri. Ndio maaana inahimizwa watu tofauti kuandika historia ili tuweze kupata picha kamili . Ila ni kosa kubwa kulalamika kwani hakuna mtu anayeweza kuandika historia ikamlizisha killa mtu. Ikitokea hivo hiyo haiewzi kuwa Historia.

Historia sio hadithi wala kumbukumbu nitaaluma mahususi ambayo huandikwa kwa malengo. Mfano historia ya Africa pamoja na malengo mengine inalenga kuondoa mtizamo hasi wa kimagharibi kuwa Africa imelaaniwa, waafrika hawakuwa na Mungu, hawana akili, ni wachawi na hwakuwa na maendeleo kabla ya wazungu kuja. Ndio maaana tafsili ya Historia ya wazungu kujenga barabara, reli na bandari Africa kwa mzungu ni maendeleo kwa mwafrika ni unyonyaji.

Lengo la pili la historia yetu ilikuwa kujenga jamii moja bila kujali dini, jimbo, matabaka ili kuwa na taifa moja la Tanzania ili kuleta umoja uliokuwa umevurugwa na wakoloni. Kwa hiyo kuonyesha kuwa kabila furani au jimbo furani au dini firani au watu furani ndio waliofanyakazi kubwa zaidi ya kuleta uhuru kuliko watu wengine ni kubomoa taifa na umoja wake. Hulka ya binadamu tunaijua tukianza kuonyeshana nani zaidi katika nchi hii hatakuwa na taifa amini naawambia wazee wetu hawakuwa wajinga,kujenga taifa hili.

Mnayoyaona kama mapungufu ya historia ndio hayo yaliyoshona taifa letu kama kitu kimoja. Hivi leo uwaweke juu wahaya kuwa walijitoa zaidi katika maendeleo ya nchi hii, utakuwa unatumaujumbe upi kwa makabila ambayo yananyanyuka sasa? Leo hii uanze kusema dini furani ndo ilo leta uhuru unatuma ujumbe gani kwa dini nyingine.

Ukoloni ulimtesa kila mtu bila kujali rangi, dini, au jimbo. Watu wote walichangia walivo weza , wengine kwa pesa, wengine kwa mali zao wengine kwa kulalamika tu , wengine kwa machozi yao, wengine kwa kuhudhuria mikutano, wengine kwa kushangilia mpaka uhuru ukapatikana. Utawaandika wote? ili iweje. Hivi haitoshi kusema kuwa uhuru uliletwa na watanzania? Tuwe makini na upande wapili wa uhuru wa kutoa maoni. kilamtu anouhuru wa kutoa maoni lakini tusije tukasahau ajenda ya taifa(kujenga umoja na upendo miongoni mwetu). Kufarakana huanza na kujikweza na kujiona zaidi. Tunavipawa ntofauti kimakundi, kijimbo kidini na ki binadamu tutumie hizo tunu kujenga kitu kamili. Ndugu zangu hizi ni dalili za ubaguzina matokeo yake tutayajutia. Utafutaje udini kama utaendelea kuandika historia zinazotukuza udiini na sio utaifa? utafutaje ukabila kama utaendelea kutukuza uzuri wa kabila furani tu kwa taifa badala ya kutukuza utaifa? HISTORI ZA WAKILISTO , HISTORIA ZA WAISLAM, HISTORIA ZA MAJIMBO,MAKABILA ZISIGEUZWE KUWA NDIO HISTORIA ZA TAIFA LETU. KUNA WATU HAWAAAMINI HIZI DINI ZA KIGENI JE SIO WATANZANIA?
 
Mohamed,
Wa kutusimulia ili tuandike kama wewe hayupo. Hatuna wazee wetu "Wakristo" waliokuwa TAA ambao wako hai sasa. Mimi ni mmoja wa wanaoogopa sana kuwasemea marehemu. Pili, ukianza simulizi kwa kutumia DINI, KABILA, JINSIA,......, inakuwa sio historia tena.
Halafu, wazee wako hawa, Mohamed hawakuwa na mapungufu hata kidogo kama ulivyomwanika Mwalimu?

WC,

Kama wewe mwoga basi kaa pembeni kwani hujasikia ule msemo aliyekaa kando haangukiwa na mti? Usinipime mimi kwa viwango vyako.

Hii kama wewe unaiona siyo historia majarida makubwa duniani wameifanyia "review" na mabingwa wa somo hili wamenialika katika vyuo vyao tukafanye mnakasha.

Wazaramo wana msemo wao, "Kalaga bao" maana yake, "We bakia hivyo hivyo " ati hii ni dini hii ni kadha wa kadha. Sasa ikiwa dini ndiyo hairuhusiwa kuwa "area of research?"

Mwenzako mmoja alikuja na moja kuwa ninapuuzwa nakamjibu sawa lakini mabingwa wa historia hawakunipuuza.
Waswahili tuna msemo, "Mmashomvi mmoja hawezi kufunga soko."

Mohamed
 
Hii ya Mohamed ukiisoma vizuri na kama fasihi yako ya kidato cha nne itakusaidia agenda kubwa hapa ni WAISLAMU na UISLAMU wa Tanzania. Kila tukijaribukumwelesha humu kuwa historia ya nchi hii inaweza ikajisimamia yenyewe bila DINI mzee wetu hataki kuelewa. Anataka WAISLAMU watajwe kwa majina yao matamu ya Kiislamu kama YESU au MTUME MOHAMED( S.A.W,) wanavyotajwa kwenye vitabu vitukufu/vitakatifu.

WC,

Kwani we umeingia lini katika mnakasha huu?

Tatizo ni kuwa historia hii ilikuwa haipo kabisa. Haijapata kuandikwa. Au huna habari hizi?

Mimi ndiyo nimeandika historia hii ya wazee wangu na hapo ndipo tulipopata nafasi ya kuizungumza humu.

Kabla yangu historia ya uhuru wa Tanganyika ilikuwa ni ile rasmi inayoanza na Nyerere.

Rudi nyuma usome nyuzi zilizopita.

Mohamed
 
atajilipua kwa mabomu kwa hasira, napendekeza Mohamed Said achukue fomu za kugombea urais 2015 ili aweze kuyatatua matatizo haya anayosema maana waislamu wenzako hawaamini.

Baadhi ya wanaukumbi taaban.

Naona jamani hebu tupumzike ingawa Sheikh Malik (Mungu amrehemu) alikuwa na msemo wake anasema, "Kuna barkaz huko utapumzika hadi kiama hapa duniani mahali pa kufanyakazi ukapumzke vizuri barkaz."

Sasa maneno kama haya...jamvi limetota halikaliki au tuagize deli jingine la kahawa na kashata zake?

Mohamed
 
Hahahahah "Nyundo" zimemlewesha, anaona nyota nyota, si unaona huko juu, mara hii sio historia ni simulizi mara hii ni historia. Ana-haha.

Unajuwa Sheikh Mohamed Said, hii shock si wao tu inaowapata hata sisi Waislaam imetupata kwa kiasi fulani labda sisi imetupata kivingine. Ngoja nikuelezee kwa upande wangu kwa ufupi sana:

Kwanza nnapokisoma ulichokiandika, huwa nnasema hakika Mwenyeezi Mungu ni mwingi wa rehema na shani zote ni zake, huwa nnasema leo angetokea Muislaam mwingine ambae hana mnasaba kabisa na hawa wazee na hakutokea katika jamii na ahli hiyo, sijui hayo matusi yangekuwaje? maana kila wanapotaka kujaribu huwa jibu ni kuwa anaeandika anawafahamu ni wao na anayoyasema ni kweli. Hapo sasa.

Hakuna humu hata mmoja aliyekuja akasema hapana, huyo Mzee uliemtaja hakuwepo na hakuwa na wadhifa huo au hakufanya harakati hizo.

Inayobaki wanaanza, mbona fulani hukumuuliza, mbona fulani hukumuuliza. Hivi ni kweli wao wanashindwa kuwauliza hao wanaowataka wao? Au wanawauliza na majibu ndio hawana pakuyaweka? Hiyo ndio shock inayonipata mimi.

Watu wanakuja na kufanya kila hila kuutowa huu mjadala kutoka kwa wazee na kuupeleka kwenye EPA, wanapoambiwa 83% ni wao, wanaanza kuuliza imetoka wapi, wanashindwa kufanya kautafiti kadogo tu wakaja hapa waseme hapa hiyo asilimia si kweli, asilimia sahihi ni hii hapa kwa ushahidi huu na huu.

Unapowaambia umeiona historia iliyoandikwa Kigamboni na imewasahau wazee waasisi wa AA na TAA na TANU na unapowabainisha kinaga-ubaga, wanashindwa kusema hao wazee si wa ukweli hawakuwepo, kama hilo linawashinda na kweli walikuwepo ni nini zaidi kinachowasumbuwa? Ni rahisi sana kuelewa, ni shock, na masikio yao na bongo zao zimeaminisha kuwa ilikuwa "One man show" sasa kuja kuona si hivyo, inakuwa vigumu sana wao ku "insert" haya ya ukweli.

Shock yangu ni kwanini inawawia vigumu?

FF,

Ahsante sana.
Wajibu wetu ni kuelimisha tusichoke.

Mohamed
 
Hotuba inasemekana haionekani sehemu yoyote kwa mujibu wa Mzee Said.
Huko kwenye archieve kumebaki ile picha Nyerere akiwa na soksi ndeefu hadi magotini.
Tulishaambiwa kuwa Sykes alitunza nyaraka zake vema sana na ameziona, sijui hakuona draft ya hotuba ya UN!

Wanasayansi wa siasa wanasema, siasa ni kitu 'fuid' kwamba kubadilika kwake ni suala la dakika na sio siku. Kuanzia mwaka 1950 hadi Nyerere alipokwenda UN kulikuwa na mabadiliko makubwa sana. Sina uhakika hiyo hotuba iliyokuwa katika mfumo wa siasa ilishindwaje kubadilika(stagnant) hadi isome vile vile.

Alipofika Dar alikuwa na MA, na alishakuwa na exposure tayari katika masula ya kimataifa.
Mwaka 1950 Nyerere alikuwa hajajulikana sana katika medani ya siasa.
Kama hotuba iliandikwa mwaka 1950, je ilikusudiwa ikasomwe lini na nani ndani ya UN?

Kuna Maswali niliuliza hapo juu,
ilikuwaje Wazee wa Gerezani walimpokea Nyerere tena kwa Kumfuata shuleni Pugu, wakamlipia, Chakula na kumpangishia Nyumba (Mohamed Saidi) wakati Nyerere alikuwa Wakuja tu, Tena Mgalatia, Na Kakabila kake kalikuwa hakajulikani kama Wamanyema?
Nyerere alikuwa na Umuhimu gani kwenye Kijiwe cha Wazee wa Gerezani kama wakina Sykes wenye uwezo mkubwa walikuwepo?

Maana kwa maelezo yote ya Bwana Mohamed Saidi Nyerere hakuwa na Msaada na wala Hakuwa wa Muhimu,

Lakini Mzee Saadan Kandoro,
ndani ya kitabu chake cha MWITO WA UHURU ambacho kimeeleza historia ya TANU kwa kina. Katika ukurasa wa 72 anaandika hivi:
“Bwana Lameck Bugohe Makaranga ndiye aliyetoa jina la ‘TANU’ likapata msaada kwa Bwana Kandoro. Majina mengine yakawekwa mezani na jina la “TANU” likapata kura zaidi na ndipo chama chetu kikawa ‘TANU’ tangu tarehe 7/7/54. Ndipo Bwana Rais Julius K. Nyerere akatunga sheria za chama na zikajadiliwa na kukubaliwa.”

Sasa kama Sheria(Katiba) hizo za TANU, aliachiwa Nyerere azitunge (kwa Mujibu wa Mtu aliyekuwepo ndani) wakati wa kina Sykes wapo, Mtu huyo kweli ndio wa kuandikiwa Hotuba ya kwenda UNO?
 
Kituko una vituko kama jina lako nani kakwambia Mzee Saadan Kandoro alikuwa muIslam safi huyu alikuwa mgalatia hana maana hata kidogo kwanza ajenda yake ilikuwa kutuunganisha waTanganyika kitabu chake MWITO WA UHURU hakifahi kuwa rejea hata kidogo.

Kuna Maswali niliuliza hapo juu,
ilikuwaje Wazee wa Gerezani walimpokea Nyerere tena kwa Kumfuata shuleni Pugu, wakamlipia, Chakula na kumpangishia Nyumba (Mohamed Saidi) wakati Nyerere alikuwa Wakuja tu, Tena Mgalatia, Na Kakabila kake kalikuwa hakajulikani kama Wamanyema?
Nyerere alikuwa na Umuhimu gani kwenye Kijiwe cha Wazee wa Gerezani kama wakina Sykes wenye uwezo mkubwa walikuwepo?

Maana kwa maelezo yote ya Bwana Mohamed Saidi Nyerere hakuwa na Msaada na wala Hakuwa wa Muhimu,

Lakini Mzee Saadan Kandoro,
ndani ya kitabu chake cha MWITO WA UHURU ambacho kimeeleza historia ya TANU kwa kina. Katika ukurasa wa 72 anaandika hivi:
"Bwana Lameck Bugohe Makaranga ndiye aliyetoa jina la ‘TANU' likapata msaada kwa Bwana Kandoro. Majina mengine yakawekwa mezani na jina la "TANU" likapata kura zaidi na ndipo chama chetu kikawa ‘TANU' tangu tarehe 7/7/54. Ndipo Bwana Rais Julius K. Nyerere akatunga sheria za chama na zikajadiliwa na kukubaliwa."

Sasa kama Sheria(Katiba) hizo za TANU, aliachiwa Nyerere azitunge (kwa Mujibu wa Mtu aliyekuwepo ndani) wakati wa kina Sykes wapo, Mtu huyo kweli ndio wa kuandikiwa Hotuba ya kwenda UNO?
 
Hahahahah "Nyundo" zimemlewesha, anaona nyota nyota, si unaona huko juu, mara hii sio historia ni simulizi mara hii ni historia. Ana-haha.

Unajuwa Sheikh Mohamed Said, hii shock si wao tu inaowapata hata sisi Waislaam imetupata kwa kiasi fulani labda sisi imetupata kivingine. Ngoja nikuelezee kwa upande wangu kwa ufupi sana:

Kwanza nnapokisoma ulichokiandika, huwa nnasema hakika Mwenyeezi Mungu ni mwingi wa rehema na shani zote ni zake, huwa nnasema leo angetokea Muislaam mwingine ambae hana mnasaba kabisa na hawa wazee na hakutokea katika jamii na ahli hiyo, sijui hayo matusi yangekuwaje? maana kila wanapotaka kujaribu huwa jibu ni kuwa anaeandika anawafahamu ni wao na anayoyasema ni kweli. Hapo sasa.

Hakuna humu hata mmoja aliyekuja akasema hapana, huyo Mzee uliemtaja hakuwepo na hakuwa na wadhifa huo au hakufanya harakati hizo.

Inayobaki wanaanza, mbona fulani hukumuuliza, mbona fulani hukumuuliza. Hivi ni kweli wao wanashindwa kuwauliza hao wanaowataka wao? Au wanawauliza na majibu ndio hawana pakuyaweka? Hiyo ndio shock inayonipata mimi.

Watu wanakuja na kufanya kila hila kuutowa huu mjadala kutoka kwa wazee na kuupeleka kwenye EPA, wanapoambiwa 83% ni wao, wanaanza kuuliza imetoka wapi, wanashindwa kufanya kautafiti kadogo tu wakaja hapa waseme hapa hiyo asilimia si kweli, asilimia sahihi ni hii hapa kwa ushahidi huu na huu.

Unapowaambia umeiona historia iliyoandikwa Kigamboni na imewasahau wazee waasisi wa AA na TAA na TANU na unapowabainisha kinaga-ubaga, wanashindwa kusema hao wazee si wa ukweli hawakuwepo, kama hilo linawashinda na kweli walikuwepo ni nini zaidi kinachowasumbuwa? Ni rahisi sana kuelewa, ni shock, na masikio yao na bongo zao zimeaminisha kuwa ilikuwa "One man show" sasa kuja kuona si hivyo, inakuwa vigumu sana wao ku "insert" haya ya ukweli.

Shock yangu ni kwanini inawawia vigumu?

Jibu Faiza fupi sana wanaadamu wengi hawakubali makosa yao hata kama vp wanajaribu kila namna kujustify their actions na sad enough hawajui kuwa ndio wanajiharibia.

Nguruvi aliniuliza kuhusu Aga Khan sikumjibu kwani nilishafahamu anakoelekea ila alisahau Aga Khan ni muislamu pia despite the fact wanafanya biashara ambazo kwa mujibu wa uislamu ni haram but haimaanishi yeye sio muislamu au haruhusiwi kujenga msikiti au jumuiya. Hivyo alitaka kuivunja hoja EAMWS but amenikuta sijaingia katika mtego wake.

Swali la msingi ni kipi kiliwafanya wazee wa kigamboni kuwatengua akina Sykes, Mshume Kiyate, Sheikh Hassan Bin Ameir na waalim wenzie, katika historia? Vp historia inadai waliopigana vita vya maji maji walikuwa wazee wapagani wakiongozwa na mganga wao Kinjekitile Ngwale wakati sio ilivyokuwa kwani hawakuwa wapagani bali ni waislamu na wengi ni watu wa tariqatul shadhiliya kwani ndio tariqa ya mwanzo kuingia Tanzania tangu mwaka wa 6 Hijri Calendar. Why they took all the efforts to erased these things? Niliwahi kuwaambia kizazi cha dot com jamani msikidharau yatakuja kuulizwa haya maswali kwa ufasaha!!! These issue zinahitajika kufafanuliwa kwa upana.
 
hili mimi nami nilishalishauri zamani tu; japo kwangu sikutaka iwe Truth and Reconciliation bali Historical Commission on Truth and Unity..

Hili halina shaka na siwezi kushangaa kwani ni mwanafunzi mzuri tu wa historia ya Kanisa katoliki pote duniani. Lakini kuishia kusema hivyo hakutoshi kwa sababu mtu mwingine anaweza kusema kuwa kutokana na madhara ya utumwa "Uislamu" ulikuwa na maovu yake kisa tu wahusika wake wengine walikuwa ni "Waislamu". Hata unaposema "maovu" ya kanisa yanaweza kabisa kuonesha ni jinsi gani pia Kanisa hilo hilo limefanya mengi sana kwenye jamii ya Watanganyika hadi leo hii na linaendelea kufanya hivyo.

Hili linasemwa lakini halina ushahidi wa kihistoria kwa sababu hakuna hoja ya kisayansi ambayo imewezakuoneha ikilinganishwa na vingine. Kwa mfano, ni kwa kiasi gani kwa mfano Wamang'ati na watu wa makabila mengine yanaoishia kijadi wanawakilishwa katika serikali? Je wanabaguliwa? Nani anawabagua? Je, mtu anaweza kusema kuwa Wakristu na Waislamu wanapendelewa Tanzania?

Je ni kweli Wakristu wote wananufaika na mfumo uliopo kiasi kwamba wana interests ya kuona unaendelezwa?

Ni kweli - lakini fikiria kuwa tayari mmeshafikia hitimisho kuwa kuna "dhulma" je watu watakuwa tayari kuambiwa "hakuna" kama uchunguzi yakinifu wa kisayansi na historia ukifanyika? Jibu ni kuwa "haiwezekani" kwa sababu watu wameshahitimisha kuwa kuna dhulma. Hata wewe unaweza kushangaa kabisa endapo tume kama hiyo ikaja na taarifa huru kabisa ya kuonesha kuwa hakuna "systematic discrimination of Muslims"! Utapigwa na butwaa!

Ni jambo moja kutaka kuutafuta ukweli lakini jingine kutaka kuthibitisha kinachodhaniwa kuwa ni kweli. Wengi wameshakubali hoja ya M. Said kuwa kuna dhulma nchini na hawataki kujiuliza maswali yoyote zaidi ya kurudia tu "Waislamu wanadhulumiwa, Waislamu wanadhulumiwa".

Je ndugu yangu Mdondoaji uko tayari kuona inaundwa tume huru ya Historia, Ukweli na Umoja ambayo itafanya kazi yake kwa uwazi na wazi katika kukusanya, kuchambua, kuhifadhi taarifa mbalimbali za historia yetu ikitafuta kujua majibu ya maswali mbalimbali? Je utakuwa open minded kukubali matokeo yake endapo yataenda kinyume na vile ambavyo tayari unaamini?

Mwanakijiji,

Unajua kuna baadhi ya hoja nakubaliana na wewe. Ila nasita kuanzishwa kwa Commision for Truth and Unity kwasababu ya historia ya nchi hii. Hembu nikuulize ikianzishwa hiyo commision do you think kweli waislamu wataiamini? If not why? Je unadhani walivyopoteza kumbukumbu za mwanzo sasa hivi ndio watazitokomeza kabisa!!!! Hebu fikiria kwa upande wa pili mwanakijiji. Ndio maana nasema ni vema ikawepo Truth and reconciliation committee kwanza tuwekane sawa na kuombana radhi yaishe. Then turekebishe historia na mwelekeo wa nchi mbele. Vyenginevyo itakuwa ni hadithi ya merry go round!!!!
 
Mdondoaji,

Katika miaka ya 1960s tukicheza mpira pale Mnazi Mmoja club yetu ikiitwa Evarton ni katika club kali za watoto wa Kariakoo. Hakuna kitu ambacho sote tulikijua kibaya kufanya kama kurudisha mpira nyuma.

Iwe itakavyokuwa lazima upeleke mpira mbele.

Mwanakijiji ni kama kisa cha Higgins anakimbizana na Mahdi jangwani.

Mahdi alimpa "merry go round" kumchosha kabla hajajitokeza kupambananae uso kwa uso.

Mwanakijiji atatuchosha.

Anapiga pasi za nyuma "back pass."

NImejitahidi kwake si haba.

Mohamed
 
Kituko una vituko kama jina lako nani kakwambia Mzee Saadan Kandoro alikuwa muIslam safi huyu alikuwa mgalatia hana maana hata kidogo kwanza ajenda yake ilikuwa kutuunganisha waTanganyika kitabu chake MWITO WA UHURU hakifahi kuwa rejea hata kidogo.

Kituko,

Ulikuwa wapi?

Hayo yote nilishatoa majibu.

Sasa wewe unapiga pasi za nyuma.

Utatuchosha.

Mohamed
 
Hotuba iliyosomwa Umoja wa Mataifa 1955 imenyambuliwa mle ndani.

Mohamed,
Ungesema hivi tangu mwanzo tusingekuvalia bango. Hotuba aliyoitoa Mwalimu UN 1955 "imenyambuliwa kutokan memoranda ya 1950" Lakini hukusema hivyo. Jinsi ulivyosema/ulivyoandika ni kwamba hotuba iliandikwa na Sykes na Mwalimu akaisoma word for word. Kumbe ile memorandum ya 1950 ilitumika kama hadidu za rejea? Ndio maana nilikuuliza, lini ulipogundua kuwa kura tatu za Tabora zilikuwa ni uamuzi wa busara? Kwa sababu katika kitabu chako, toleo la kwanza, uliandika kuwa ni ushahidi wa kuwabagua Waislamu. Tuendelee.
 
Back
Top Bottom