Jasusi hebu pitia hii:
"Hivi sasa kuna vitabu viwilivilivyoandikwa na Wakristo wenyewe vinavyothibitisha kuwa Wakristo wametumianyadhifa zao katika serikali kuuhujumu Uislam na Waislam. Jan P van Bergenkatika kitabu chake, Development and Religion in Tanzania,(1981) [1]ametoboa siri kuhusu uadui aliokuwa nao Rais Mstaafu, Nyerere dhidi ya Uislamna Waislam. Kitabu kinaeleza kwa ufasaha jinsi Nyerere wakati alipokuwamadarakani alivyokuwa akifanya mikutano ya siri na viongozi wa Kanisa kuwekamikakati ya kuupa nguvu Ukristo. Katika mikutano hiyo Nyerere aliwahakikishiaviongozi wa Kanisa kuwa anaaunga mkono Ukristo. Kitabu hicho kinaeleza jinsiNyerere alivyotimiza ahadi yake hiyo kwa Kanisa kwa kuhakikisha kuwa anawapaWakristo nafasi za juu katika serikali na chama. Kitabu hiki kilikuwa kinauzwaCatholic Bookshop, Dar es Salaam. Lakini ilipokuja kudhihirikia Kanisa kuwakitabu hiki kilikuwa kinatoa habari nyeti na siri za Kanisa kuhusu njama dhidiya Waislam, kwa haraka sana kikaacha kuuzwa. [1] Hadi hivi sasa kitabuhicho ni marufuku kuletwa tena Tanzania.Kitabu cha pili ni cha Dr John C.Sivalon, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985 (1992). [1]Kitabu hiki kinaeleza njama ndani ya serikali kuuhujumu Uislam. Sivalonanafichua kuwa kuanzia mwaka 1961 baada ya Tanganyika kupata uhuru, Kanisalilikuwa na hofu mbili. Hofu ya kwanza ilikuwa umoja wa madhehebu za Kiislamkati ya Sunni, Bohora, Ismailia na Ithnasheri. Hofu ya pili ilikuwa kuhamishwakwa makao makuu ya EAMWS kutoka Mombasa kuja Dar es Salaam. Kanisa lilikuwalinahofu kuwa mali walizokuwanazo Waasia Waislam zikitiwa katika harakati za Waislamambao walikuwa na nguvu kubwa katika uwanja wa siasa zitaathiri maslahi ya Ukristo katika Afrika yaMashariki. Kwa ajili hii Kanisa likatanganza kuwa Uislam ni adui wake naikaanza mikakati ya hujma dhidi ya Uislam ili kuudhoofisha. [1]Kuna kazi mbili zilizoandikwa na Waislam kuhusu uhusiano baina ya serikali naWaislam. Kazi ya kwanza ni tasnifu ya Kiwanuka, ëThe Politics of Islam inBukoba Districtí (1973); [1]kazi ya pili ni makala ya utafiti ëIslam and Politics in Tanzaniaí (1989) [1]iliyoandikwana mwandishi wa kitabu hiki. Ilikuwa baada ya kusoma tasnifu yaKiwanuka na kuona jinsi ukweli wa kuvunjwa kwa EAMWS kulivyopoteshwa ndipo kamaMuislam na kama ada ya Uislam inavyodai kuwa pande mbili za mgogoro zote lazimazisikilizwe, ndipo nilipoamua kufanya utafiti na kuandika tatizo lile kwamtazamo wa Waislam. Ukweli ambao kwa miongo miwili ulizuiwa usifahamike kwaWaislam. Kiwanuka anadai na kuafiki kuwa Nyerere alikuwa na haki ya kutumiavyombo vya dola dhidi ya Waislam kwa kuwa kama asingefanya hivyo nchi ingekuwana mamlaka mbili, yaani ya Waislam na ya serikali. Kwa ajili hii aliamuakuivunja EAMWS ili ëkulinda umoja wa kitaifaí. Halikadhalika ipoëKwikima Reportí (1968)[1]ambayo imeeleza kwa ufasaha tatizo la EAMWS, chanzo chake na mchango wa serikalikatika kuhujumu umoja wa Waislam. Taarifa hii inafaa kutumika leo kama dira yakuelewa tatizo la Waislam wa Tanzania kama ilivyokuwa wakati ule ilipotolewakwa mara ya kwanza. Taarifa ya Kwikima inaeleza jinsi TANU, serikali na Waislamwachache katika TANU walivyodanganyika kudhani kuwa katika kuisaidia serikalikuivunja nguvu EAMWS walikuwa wanatimiza uzalendo na maslahi ya taifa. Rejeahizi tano ni muhimu kwa wanafunzi wa historia ya siasa Tanzania; na kwa mtafitiyeyote anaetaka kujua chanzo cha chuki baina ya Waislam na serikali na chanzocha hisia kali za kidini zinazoikumba nchi yetu kuanzia miaka ya 1980. Rejeazote hizo za vitabu, makala za utafiti na taarifa mbalimbali, ingawazimeandikwa na waandishi tofauti na kwa muelekeo tofauti zote hizi zinadhihirishakitu kimoja ñ kuwepo kwa njama zinazoendelea kwa zaidi ya karne moja dhidi yaUislam na Waislam, kwanza zilikuwa zikifanywa na wakoloni walioitawalaTanganyika na sasa zinafanywa na Wakristo wananchi kuhakikisha kuwa Uislamhaupati nguvu."