Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,984
Sweke34,
Ukoloni haukuwa unafanyakazi kwa namna hiyo hawakuutazama Uislam kwa jicho lilelile walilotazama Ukristo. Sasa ikiwa nitatoa mchango wa Uislam katika via hivi nitakuwa nauogopa ukweli. Hebu soma hiki kipande hapa chini:
"Vita vya Maji Maji vilipoanza kusini yaTanganyika mwaka 1905 kwa nia ya kuwafukuza Wajerumani kutoka Tanganyika, zilesehemu zenye Wakristo wengi zilikataa kujiunga na vita na badala yakewakajiunga na majeshi ya Wajerumani na kupigana bega kwa bega na dhidi ya wazalendo.Hii ilitokana na sababu ya kuwa uasi dhidi ya dhulma wa Wajerumani ulianzakatika maeneo yenye Waislam wengi na vita vikachukua sura ya vita vya Kiislamudhidi ya Wazungu ambao dini yao ni Ukristo. Kwa kuwa wamishonari walikuwawashirika wa wakoloni, walichukuliwa kama maadui na hivyo ikawa vituo vyaovinashambuliwa na wapiganaji wa Maji Maji. Kutokana mashambulizi haya, Wakristowalivichukua Vita Vya Maji Maji kama vita dhidi ya Ukristo. Harakati za MajiMaji zilishindwa na Wajerumani walifanya fisadi kubwa dhidi ya wananchi naviongozi wao. Jambo hili liliacha kovu kubwa katika fikra za wananchi na kwaupande wa Wakristo ambao walinusurika na ghadhabu ya Wajerumani, wengi waowakajiweka mbali na aina yoyote ya kupinga ukoloni. Kufuatia historia hii Waafrika waliokuwakusini ya Tanganyika sasa wakiwa chini ya utawala wa Waingereza na kuwa chiniya himaya ya wamishonari walipupazwa kiasi kiasi kwamba waliogopa siasa. Baadaya Waafrika kushindwa vita kwa silaha kali za Wazungu sasa Kanisa likaona ndaniya fadhaa ile fursa yao kutawala sehemu hiyo kwa kutoa vishawishi kama vileshule na hospitali. Kwa hiyo Wamishionari na Waingereza walionekana kamamabwana wema wenye kuwajali raia zao kinyume na serikali katili na ya kidhalimu ya Wajerumani. Vuguvugu la siasakama ilivyokuwa Vita vya Maji Maji, lilianza katika maeneo ya Waislam kufuatiamfumo ule ule kama ilivyokuwa katika upinzani wa ukoloni wa Wajerumani.Wakristo katika Jimbo la Kusini waliiona TANU kama walivyoviona Vita Vya MajiMaji, kama harakati nyingine za Waislam zilizowa zinakuja tena kwa mara ya pilikuvuruga amani na utulivu. TANU ilipoanza ikawa inavuma kuwa safari hii Waislamwalikuwa wamemua kuanzisha vita dhidi ya Waingereza kama walivyoanzisha vita naWajerumani."
Ikiwa sitafanya uchambuzi kama historia ilivyokuwa kwa kuogopa ukweli na kutaka kuwafurahisha watu historia hii itapotea.
Mohamed
Sheikh Mohamed,
Ni kweli utaendelea kuutaja uislamu kama ambavyo na sisi tutaendelea kukukatalia kwamba hao wazee walipokuwa wanapigana, hawakusukumwa na uislamu wao bali uafrika wao na utanganyika wao.
Kwakuwa umeamua kumpigia back pass sweke, ngoja na mie nikurudishie back pass.
Askari wa kimanyema, kinubi na kizulu (waislamu) walishirikiana na wazungu wajerumani (wakristo) kupambana na mwafrika mwenzao mkwawa (muislamu) na hatimaye kushinda vita na kupelekea mkwawa kujinyonga.
Kwahiyo hapa tuseme waislamu walikuwa wanapigana dhidi ya uislamu ama muislamu mwenzao? hapana, ni dhahiri kwamba waafrika(niwaite mamluki) walikuwa wanatumikia mabwana zao kwa ajili ya maslahi yao binafsi. Na hawakupigana kwa mgongo wa uislamu bali walitumikia utumishi wao kwa mjerumani.
Sasa ilipofika zamu ya waingereza kuitawala tanganyika, hawa wamanyema, wanubi na wazulu (waislamu) hawakuwa na previledge walizokuwa wakipata enzi za mjerumani kwahiyo waliunganisha nguvu na wenyeji wao katika kupigana na muingereza. Walipigana kama watanganyika na si waislamu! pamoja na kwamba walikuwa na imani ya uislamu lakini hawakusukumwa kwenda kupigania uhuru kwa sababu ya uislamu wao bali utanganyika wao na uafrika wao.
Askari hao hao wa kizulu, kinubi na kimanyema(waislamu) ndio hao hao walitumika na mkoloni kupambana na bushiri pangani (muislamu). Je hapo kulikuwa na agenda ya uislamu? hapana, walikuwa wanawatumikia mabwana zao wajerumani! Tukifika mahali pa kutenganisha uislamu na utanganyika tutakwenda pamoja vizuri sana, short of that itakuwa ni kuyumbishana tu.