Ogah,
Unanionea mimi bure bila sababu. Uminita mimi mamluki nikakuwekea habari uisome na uamue nani mamluki badala ya kunipa jibu unakuja na hamaki nyingi zaidi.
Sijachoka nakuwekea tena ile ile na safari hii uwanja uko wazi kwa mwanaukumbi yeyote aseme kwa hakililah nani ni mamluki:
"Hivi sasa kuna vitabu viwilivilivyoandikwa na Wakristo wenyewe vinavyothibitisha kuwa Wakristo wametumianyadhifa zao katika serikali kuuhujumu Uislam na Waislam. Jan P van Bergenkatika kitabu chake, Development and Religion in Tanzania,(1981) [1]ametoboa siri kuhusu uadui aliokuwa nao Rais Mstaafu, Nyerere dhidi ya Uislamna Waislam. Kitabu kinaeleza kwa ufasaha jinsi Nyerere wakati alipokuwamadarakani alivyokuwa akifanya mikutano ya siri na viongozi wa Kanisa kuwekamikakati ya kuupa nguvu Ukristo. Katika mikutano hiyo Nyerere aliwahakikishiaviongozi wa Kanisa kuwa anaaunga mkono Ukristo. Kitabu hicho kinaeleza jinsiNyerere alivyotimiza ahadi yake hiyo kwa Kanisa kwa kuhakikisha kuwa anawapaWakristo nafasi za juu katika serikali na chama. Kitabu hiki kilikuwa kinauzwaCatholic Bookshop, Dar es Salaam. Lakini ilipokuja kudhihirikia Kanisa kuwakitabu hiki kilikuwa kinatoa habari nyeti na siri za Kanisa kuhusu njama dhidiya Waislam, kwa haraka sana kikaacha kuuzwa. [1] Hadi hivi sasa kitabuhicho ni marufuku kuletwa tena Tanzania.Kitabu cha pili nicha Dr John C. Sivalon, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi1985 (1992). [1]Kitabu hiki kinaeleza njama ndani ya serikali kuuhujumu Uislam. Sivalonanafichua kuwa kuanzia mwaka 1961 baada ya Tanganyika kupata uhuru, Kanisalilikuwa na hofu mbili. Hofu ya kwanza ilikuwa umoja wa madhehebu za Kiislamkati ya Sunni, Bohora, Ismailia na Ithnasheri. Hofu ya pili ilikuwa kuhamishwakwa makao makuu ya EAMWS kutoka Mombasa kuja Dar es Salaam. Kanisa lilikuwalinahofu kuwa mali walizokuwanazo Waasia Waislam zikitiwa katika harakati zaWaislam ambao walikuwa na nguvu kubwa katika uwanja wa siasa zitaathiri maslahi ya Ukristo katika Afrika yaMashariki. Kwa ajili hii Kanisa likatanganza kuwa Uislam ni adui wake naikaanza mikakati ya hujma dhidi ya Uislam ili kuudhoofisha." [1]
Mohamed