Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Kumbe sio mimi pekeyake ninayeona hivyo.
Mzee na Mheshimu ana staa walakin
Syll...
Mimi nakuhadithieni historia ya nyumbani kwetu nimeandika kitabu cha historia ya jamii yangu ambayo kabla haikuwapo.

Vipi mtu ataniambia kuwa hiyo siyo historia yetu?

Bahati mbaya au nzuri Nyerere ni sehemu ya historia hii.

Ingewezekana mimi ningemtoa katika historia hii nisingemtaja lakini historia hii itakuwa na upungufu mkubwa.

Angalia picha hiyo hapo chini.

Huyo kulia ni Mama Sakina mimi namwita bibi mwanae mmoja Mustafa alikuwa rafiki ya baba yangu.

Huyo kushoto ni Bi. Tatu bint Mzee akiishi Kirk Street (Mtaa wa Lindi) mbele ya mtaa huu ni Mtaa wa Kipata niliozaliwa mimi.

Bi. Tatu bint Mzee ni rika moja na mama yangu kwa hiyo Bi. Tatu mimi ni mama yangu.
Nimezaliwa na watu hawa na nimeishinao.

Sasa uongo uko wapi hapo?
Kuwa hawakuijenga TANU wala kupigania uhuru?

Jiulize wamefika vipi kuwa na Nyerere wanamsindikiza safari ya kwanza UNO 1955 na kumfanyia dua ya kumuaga katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?

1648619287946.png
 
Unaweza kututajia hao watu unao wasema kiongozi wangu ?
Hivi kwa akili yako unaamini huyu mzee hajui michango mikubwa ya Watanganyika lukuki Tanganyika nzima wasiyo Waislamu? Kwanini hawatambui katika simulizi zake na badala yake amebakia kumwaga majina ya Waislamu pekee?
 
Wewe wataje yeye amewataja anao wajua yeye, usiumize kichwa sana.

Au kwanini walio andika Historia ya uhuru hawakuwataja wazee wake ambao yeye anasema wameshiriki katika hilo suala...?
 
Syll...
Mimi nakuhadithieni historia ya nyumbani kwetu nimeandika kitabu cha historia ya jamii yangu ambayo kabla haikuwapo.

Vipi mtu ataniambia kuwa hiyo siyo historia yetu?

Bahati mbaya au nzuri Nyerere ni sehemu ya historia hii.

Ingewezekana mimi ningemtoa katika historia hii nisingemtaja lakini historia hii itakuwa na upungufu mkubwa.

Angalia picha hiyo hapo chini.

Huyo kulia ni Mama Sakina mimi namwita bibi mwanae mmoja Mustafa alikuwa rafiki ya baba yangu.

Huyo kushoto ni Bi. Tatu bint Mzee akiishi Kirk Street (Mtaa wa Lindi) mbele ya mtaa huu ni Mtaa wa Kipata niliozaliwa mimi.

Bi. Tatu bint Mzee ni rika moja na mama yangu kwa hiyo Bi. Tatu mimi ni mama yangu.
Nimezaliwa na watu hawa na nimeishinao.

Sasa uongo uko wapi hapo?
Kuwa hawakuijenga TANU wala kupigania uhuru?

Jiulize wamefika vipi kuwa na Nyerere wanamsindikiza safari ya kwanza UNO 1955 na kumfanyia dua ya kumuaga katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?

View attachment 2168905
We mzee una mental illness kwa sababu ya udini na ubinafsi..ila pole sana mana hiyo historia yako itabaki chumbani kwako haitokuja fundishwa popote pale ndani au nje ya nchi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe wataje yeye amewataja anao wajua yeye, usiumize kichwa sana.

Au kwanini walio andika Historia ya uhuru hawakuwataja wazee wake ambao yeye anasema wameshiriki katika hilo suala...?
Wazee wako walitajwa? Kila mtu akianza kudai wazee wake wamesahaulika kutajwa kwenye vitabu vya historia itakuwa ni useng.e mtupu. Una hoja za kitoto. Pumbaav!
 
Usini quote tena wee fala. Nenda kabishane na wenzako wa uswahilini.
 
Mohamed anatakiwa achukuliwe afungwe Kwa kosa la uchonganishi Na uchochezi Na uhaini
 
We mzee una mental illness kwa sababu ya udini na ubinafsi..ila pole sana mana hiyo historia yako itabaki chumbani kwako haitokuja fundishwa popote pale ndani au nje ya nchi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Jiwe...
Kuniita mwendawazimu umenikumbusha kisa kilichotokea wakati mimi kijana niko kazini.

Palitokea tatizo kazini baina yangu na mkubwa wangu.

Majalada muhimu ya wateja yalikuwa hayaonekani hivyo nikaandikiwa barua kali nijieleze vinginevyo nitachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Mimi na mkubwa wangu tukatakiwa tujieleze mbele Mkurugenzi wa Idara.

Mkubwa wangu akaeleza kazi aliyonikabidhi na jinsi nilivyoshindwa kuikamilisha na kupoteza majalada yenyewe.

Ilipofika zamu yangu nikaeleza kwanza kuwa kuwa mimi katika umri wangu ulimi wangu haujagusa ulevi wa aina yeyote kwa hiyo akili yangu haijapata kupoteza fahamu hata dakika moja.

"Huyu mkubwa wangu ana tatizo la kumbukumbu hawezi kuhifadhi vitu akilini kwa ajili ya pombe.

Kazi nimekamilisha na nimemkabidhi lakini lipo tatizo hapa la kusahau kwa kuwa wakati mwingine anakuwa hayuko sawa anakuwa pombe haijamtoka.

Yeye kaniandikia barua kutaka kuniharibia maisha yangu mimi ninachoomba tupekue ofisi yake tutafute hayo majalada."

Ofisi ilipekuliwa.

Majalada yalionekana yakiwa nimeyamekamilisha siku nyingi nyuma tena yametupwa ovyo pasipostahili.

Siku ile Mkurugenzi wa Idara alishuhudia uozo uliokuwa ofisini kwa mkubwa wangu.

Barua niliyoandikiwa ilifutwa.

Kilichofuatiwa mimi nikapewa uhamisho kwenda idara nyingine kwani ilikuwa fedheha nisingeweza kufanyakazi chini ya bwana yule.

Mimi akili zangu zimetimia.
Mkubwa wangu ana tatizo la akili.

Kuhusu historia.

Labda hufahamu nimeshiriki katika kuandika Dictionary of African Biography, Oxford University Press New York (2011).

Nimeshiriki kuandika vitabu vya historia shule ya msingi Afrika ya Mashariki, Oxford University Press, Nairobi (2007).

Kote huko kazi zangu zimechapwa na zinasomwa.

Kwa kuhitimisha ipime akili yako jinsi unavyoweza kunitukana kuwa mimi mwehu bila kujali chochote na ipime akili yangu nilivyokujibu.
 
Tuma maombi BAKWATA waruhusu simulizi/hadithi zako ziwe sehemu ya mafundisho kwenye Madrassah.
 
Usini quote tena wee fala. Nenda kabishane na wenzako wa uswahilini.
Acha mihemko katika mambo ya kielimu. Unaleta uzwazwa na ushabiki wa kitoto.

Siku nyingine usirudie tena kuandika ujinga ukiwa huna hoja.
 
Wazee wako walitajwa? Kila mtu akianza kudai wazee wake wamesahaulika kutajwa kwenye vitabu vya historia itakuwa ni useng.e mtupu. Una hoja za kitoto. Pumbaav!
Wewe si ndiyo ulie anza kulia lia kwamba kuna watu unawajua wengi mno wamepigani uhuru, sasa kama unashindwa kuwataja, uliandika ili ufurahishe nafsi yako ?

Anae dai ujue ana ushahidi wa hilo, unapo amua kumpinga umpinge kwa hoja.

Dogo, matusi hayana uwezo hata wa kubadili herufi moja,sasa naona unapoteza muda kutukana.

Sasa kama ni hoja ya kitoto, inakuwaje unashindwa kuikosoa na kuiweka sawa, bali hata swali dogo la kuwataja kumi tu unao wajua unashindwa. Siyo kila mjadala uchangie, mingine ni bora kuwa msomaji na kupata faida.

Huwa siitiki mpaka niitike au unakuwa kama mwanamke mjamzito, visirani mia.

Shukrani.
 
Tuma maombi BAKWATA waruhusu simulizi/hadithi zako ziwe sehemu ya mafundisho kwenye Madrassah.
Gold...
Kuna wakati yapata sasa imepita miaka 30 kilitengezwa kitabu cha kusomesha Islamic Knowledge.

Historia hii imo ndani ya kitabu hicho kama sura na wanafunzi wanaisoma.

BAKWATA wala hawakutuma maombi kwangu kutaka idhini yangu.
 
Gold...
Kuna wakati yapata sasa imepita miaka 30 imepita kilitengezwa kitabu cha kusomesha Islamic Knowledge.

Historia hii imo ndani ya kitabu hicho kama sura na wanafunzi wanaisoma.
Jambo jema sana mzee. Hadithi zako zibaki humo humo ambapo zina nafasi, na siyo kwenye mainstream Tanzanian society.
 
Hapa nchini kitabu kinasomwa sana na JF imesaidia sana kukitangaza kitabu hiki kuanzia 2002 tulipofanya tafsiri ya Kiswahili hadi leo kitabu kimechapwa mara nne.

Wasomaji wakifika maduka ya Ibn Hazm kununua kitabu hiki huuliza kitabu cha Sykes.

Allah ana maajabu yake 1988 gazeti lililomtaja kama mwasisi wa TANU lilikusanywa lote.

Leo kitabu cha Abdul Sykes kinauzwa madukani na vyombo vya habari vinakuja nyumbani kunihoji kuhusu mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

View attachment 2169265
View attachment 2169270
View attachment 2169271
 
Tutajie kumi tu.
Kisai,
Ile historia ya Mwalimu mwaka wa 1952 anafika nyumbani kwa Abdul Sykes kaongozana na Kasella Bantu na Mwalimu anajulishwa kwa Abdul ni historia muhimu sana.

Nyumbani kwa Abdul Sykes Mwalimu kapokelewa na Mama Daisy na mwanae Daisy na Abbas Sykes wakati ule kijana mdogo.

Hii ni "milestone" katika historia ya Mwalimu na halikadhalika katika historia ya akina Sykes kama waasisi wa harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Sasa hapa rudi nyuma hadi 1929 wakati Kleist Sykes anaasisi African Association (AA).

Nyerere alikuwa na miaka 7 Abdul ana miaka 5.

Anzia hapa fungua nyaraka na kumbukumbu alizoacha Kleist akieleza Waafrika wa Tanganyika walikuwaje miaka hiyo fika hadi hapo mwaka wa 1952 wazalendo hawa wawili walipokutana wote wakiwa wanachama wa TAA.

Mimi nimebahatika kumjua Abdul Sykes, Mama Daisy, Daisy na Abbas Sykes na nimeisoma historia ya TAA kutokea 1929 hadi 1952 na kuisoma historia hii kuanzia 1952 hadi uhuru unapatikana 1961.

Katika hawa waliompokea Nyerere 1952 Ally Sykes ndiye niliyeishinae katika maisha ya kila siku hadi alipofariki 2013.

Hata Nyerere hawezi kusema kuwa anaijua TAA na TANU kumshinda Ally Sykes.

Mimi nimejifunza historia hii yote kutoka 1929 hadi wanaunda TANU 1954 kutoka kwa mzalendo huyu.

Kadi ya TANU ya Julius Kambarage Nyerere ni No. 1 kaandikiwa na Ally Sykes, kadi no 2 ni mwenyewe Ally Kleist Sykes na kadi no. 3 ni Abdulwahid Kleist Sykes.

Nimeziona kwa macho yangu barua za kusajili TANU nyingine "notes," zilizoandikwa kwa mkono kutoka kwa Zuberi Mtemvu kwenda kwa Ally Sykes, uchapaji wa kadi nk. nk.

Tuifute historia hii tubakie na historia gani?
 
Hii kauli huwa naisikia sana, sijui watu wameihakiki kwa namna gani. Uongo ukijirudia unakuwaje ukweli ?
Ni msemo ukimaanisha kuwa uongo ukirudiwa rudiwa mara nyingi hugeuka kuwa 'ukweli''
Haina maana uongo huo ni ukweli bali watu watauamini uongo huo na kuamini uongo kuna upa uhalali wa ukweli.

Mathalan, uongo wa kwamba Abdul Sykes alimpokea Mwalimu Dar es Salaam umerudiwa rudiwa sana kiasi kwamba watu wanaamini kuwa Abdul alimpokea Mwalimu. Kule kuamini ndio kunafanya uongo huo uonekane ukweli lakini haina maana ni ukweli, ni uongo uliorudiwa sana ukaonekana ukweli.
 
Nguruvi...
Hakuna tatizo ndugu yangu watu watapima kama mimi ni muongo.
 
Mohamed hili si suala la kupima ni suala la ukweli. Nyerere alikuwepo na Abdul Sykes alikuwepo

Hoja kwamba Abdul Sykes alimpokea Mwalimu unajenga fikra za Mwalimu kutoka Butiama na kufikia kwa Abdul Sykes. Je, hicho ndicho kilichotokea? Kama si hivyo ni kipi?

Mwalimu alikuwa Mwanafunzi Makerere. Kwa nyakati hizo siasa za Afrika Mshariki zilikuwa za pamoja na Mwl alitambua uwepo wa AA ya Kleist na Mwl Matola na TAA ya akina Abdul Sykes.

Mwalimu alikwenda Tabora kufundisha akawa katibu wa tawi la Chama, tawi kubwa nchini kwa siasa za nyakati hizo. Huyu katibu hakujuana na viongozi wa makao makuu japo kwa barua?

Mwl akahudhuria mkutano mkuu wa chama 1948. Mwl alikuja kama 'mzamiaji' au alialikwa?
Kama alialikwa nani alitoa Mwaliko! Katika mkutano Mwl hakujitambulisha anatoka wapi?

Mwl akaenda Scotland, aliporudi akaja Dar es Salaam kufundisha shule ya Pugu
Kwa mujibu wa Mohamed Said, Mwl alitambulisha kwa Abdul Sykes na siku nyingine alilala Temeke kwa rafiki yake. Hadi hapo Abdul alimpokeaje Mwl Dar es Salaam?

Kwa mujibu wa Mohamed Said Mwalimu aliishi nyumbani kwa akina Abdul Sykes akipikiwa Mayai ! hakuna ubishi katika hilo, lakini hilo halimfanyi Abdul awe amempokea!

Kama kuna makosa katika maelezo hayo hapo juu, Mohamed atufafanulie Abdul Sykes alimpokeaje Mwl.
 
Back
Top Bottom