Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

jamani mmemshukia sana mzee mohamed said .... vijana nadhani kwa sasa mumuwache apumzike kwa amani. nadhani atakuwa amejifunza kuwa watu wapo makini na hawadanganyiki kamwe. hayo mengine ni kibinadamu tu anakosea... msameheeni wajameni. tumeona mchele ni upi na chuya ni zipi. miaka hii ni ngumu kuwadanganya vijana hata ukitaa kupitia wenye dini au kabila....wanakuruka na kukufanya ujisikie mnyonge na mpweke.
Mtu...
Mbona unanipitishia hukumu ya kunionea.
Mimi kweli wa kujifundishwa historia hii ya wazee wangu?

Kuwa nisamehewe kuwa nadanganya nk. nk.

Inakuwaje unataka kuninyang'anya haki yangu niliyoipata kwa jasho langu?

Mimi naweza kusimama kwa hoja na hao wote na waongezeke mara mbili.

Wala usidhani natupa maneno tu ya kutupa.

Huu mwaka wa kumi na zaidi nipo hapa hajanishinda mtu mwisho huishia matusi nikafunga mjadala na sababu ya kufunga ni kuwa siwezi kujibu matusi naweza kujibu hoja.

Wewe nani na kwa ujuzi upi uliokuwanao katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na historia ya Mwalimu Nyerere unitolee mimi hukumu?

Mimi nimesoma Nyaraka za Sykes zinakwenda nyuma kutoka 1929 hadi 1961 uhuru unapatikana.

Kila aliyehusika katika kupigania uhuru wa Tanganyika yumo humo.

Hakuna mtafiti yeyote aliyefunguliwa nyaraka hizi ila mimi.

Kama hamuutaki ukweli huu sawa hakuna wa kukulazimisheni mnaweza kuendelea kuamini historia rasmi hakuna tatizo.

Hii nchi huru una rukhsa ya kuamini upendacho.

Kitabu changu kipo kinasomwa toka 1998 si hapa tu bali vyuo vyote vinavyosomesha historia ya Afrika na baadhi ya vyuo hivyo nimealikwa kuzungumza.

Hawa Northwestern University, Chicago, Evanston Illinois ndiyo wanaongoza duniani katika African History.

Screenshot_20220331-173703_Photos.jpg
 
Hoja zako hazina mashiko MS. Kitabu kitakuwa kimedoda kimauzo mzee. Inabidi ufanye jitihada za ziada watu angalau wafahamu bado kipo sokoni. Lakini pamoja na jitihada zako zote miaka nenda, miaka rudi, kitabu bado hakiuziki. Publishers watakuwa wamepata hasara.
Gold...
Siwezi kuingia katika ubishi huo.
 
Gold...
Siwezi kuingia katika ubishi huo.
Why not mzee MS? Tupatie idadi ya mauzo tokea kitabu kichapishwe tafadhali. Hii siyo siri kati yako na publisher(s). Maana kama kitabu ni “best seller” kama unavyodai., basi litakuwa ni jambo rahisi sana kutupatia takwimu za mauzo ya hicho kitabu chako pendwa tokea kichapishwe.
 
Haya yote ya nini ndugu yangu?
 
Nearly Ten Year back you still rumbling..........
All fake self proclaimed themselves so called "JF Intellectuals" have sunk in their own vomit.....
Kudos Mohamed Said
 
Nearly Ten Year back you still rumbling..........
All fake self proclaimed themselves so called "JF Intellectuals" have sunk in their own vomit.....
Kudos Mohamed Said
Tek...
Hili jambo jepesi sana kueleweka.
Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika walioitafiti na kuandika wamefanya makosa.

Haya makosa mimi nimeyaona na nimejua kuwa hapa yapo makosa.

Tuchukulie kuwa waliofanya makosa yale hawakukusudia yamefanyika kwa upungufu wa kibinadamu.

Tuchukulie hivi kuwa makosa haya ni kwa bahati mbaya.

Mimi nimejua kuwa historia ya TANU imekosewa kwa kuwa hicho chama kimeasisi na wazee wangu kwa ajili hii basi ni historia yangu naijua kwa kuwa historia hii nimeishinayo toka niko mtoto hadi napata akili zangu nasoma chuo kikuu.

Chuo Kikuu ndiyo nakutana na historia ambayo siyo kabisa.

Nimeandika kitabu na kuiweka sawa historia yote ya uhuru kuanzia kuasisi kwa African Association (AA) 1929 hadi kufika kuundwa kwa TANU 1954.

Bahati nzuri nyaraka za kusaidia kuelewa historia hii zipo na wahusika wakuu walikuwa hai na wameeleza kila kitu kama kilivyokuwa.

Nimeandika kitabu na kitabu kimechapwa.

Katika hali kama hii cha kutegemewa ni ''critique,'' za kawaida kwani hakuna kazi ya mikono ya binadamu inayoweza kuwa kamili isiwe na makosa.

Kinyume chake nimejengewa uadui kwa kuandika kitabu ambacho kimewarejesha wapigania uhuru ambao hawakutajwa katika historia iliyotangulia.

Huko nje mambo ni tofauti wao maswali wanayoniuliza ni inawezekana vipi historia ya nchi ikageuzwa?

Wako wapi wasomi wa vyuo vikuu Idara ya Historia wakati haya yanatokea?
Maswali mengi, mengi, mengi naulizwa.

Wanataka kujua wanahistoria wamefanya nini baada ya kusoma historia ya uhuru kama nilivyoiandika.

Nawaeleza kuwa baadhi ya walimu wanawakataza wanafunzi wao kufanya rejea kwenye kitabu changu.

Wananiuliza kwa nini wanafanya hivyo?
Ilmuradi wanashangaa.

Angalia hiyo picha ya Dome Budohi na mimi tumepiga Nairobi ipo katika kitabu cha Abdul Sykes.

Kadi ya TANU ya Dome Budohi ni No. 6 na ni mmoja wa viongozi walioingia katika uongozi wa TAA pamoja na Julius Nyerere, Abdul Sykes, Kassela Bantu kwa kuwataja wachache katika uchaguzi wa April 1953.

Dome Budohi alikuwa ni jamaa akijuana vyema na wazee wangu katika 1950s wakati wa harakati za kuunda TANU.

Mwaka wa 1955 alikamatwa kwa tuhuma za kuwa Mau Mau akarejeshwa kwao Kenya na kufungwa Lamu.

1648785888729.png
 
Tek...
Hili jambo jepesi sana kueleweka.
Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika waioitafiti na kuandika wamefanya makosa.

Haya makosa mimi nimeyaona na nimejua kuwa hapa yapo makosa.

Tuchukulie kuwa waliofanya makosa yale hawakukusudia yaefanyika kwa upungufu wa kibinadamu.

Tuchukulie hivi kuwa makosa ni kwa bahati mbaya.

Mimi nimejua kuwa historia ya TANU imekosewa kwa kuwa hicho chama kimeasisi na wazee wangu kwa ajili hii basi ni historia yangu naijua kwa kuwa historia hii nimeishinayo toka niko mtoto hadi napata akili zangu nasoma chuo kikuu.

Chuo Kikuu ndiyo nakutana na historia ambayo siyo kabisa.

Nimeandika kitabu na kuiweka sawa historia yote ya uhuru kuanzia kuasisi kwa African Association (AA) 1929 hadi kufika kuundwa kwa TANU 1954.

Bahati nzuri nyaraka za kusaidia kuelewa historia hii zipo na wahusika wakuu walikuwa hai na wameeleza kila kitu kama kilivyokuwa.

Nimeandika kitabu na kitabu kimechapwa.

Katika hali kama hii cha kutegemewa ni ''critique,'' za kawaida kwani hakuna kazi ya mikono ya binadamu inayoweza kuwa kamili isiwe na makosa.

Kinyume chake nimejengewa uadui kwa kuandika kitabu ambacho kimewarejesha wapigania uhuru ambao hawakutajwa katika historia iliyotangulia.

Huko nje mambo ni tofauti wao maswali wanayoniuliza ni inawezekana vipi historia ya nchi ikageuzwa?

Wako wapi wasomi wa vyuo vikuu Idara ya Historia wakati haya yanatokea?
Maswali mengi, mengi, mengi naulizwa.

Wanataka kujua wanahistoria wamefanya nini baada ya kusoma historia ya uhuru kama nilivyoiandika.

Nawaeleza kuwa baadhi ya walimu wanawakataza wanafunzi wao kufanya rejea kwenye kitabu changu.

Wananiuliza kwa nini wanafanya hivyo?
Ilmuradi wanashangaa.

Mohmed Said,

Mambo yaliyokuwa yanafanyika zama za Nyerere ni ufichwaji wa majina ya wazalendo wa Kiislamu au wenye majina ya kiislamu kuandikwa katika vitabu vya historia ya nchi hii kama wapigania uhuru nadhani sababu ni hii; Waisilamu ni wengi sana katika kupigania uhuru ukilinganisha na idadi ya Wasiokuwa Waisilamu ikizingatiwa kuwa wasiokuwa waisilamu walikuwepo na wal "enjoy" maisha katika utawala wa Kikoloni na hawakuona umuhimu wa kupigania uhuru ili kulinda starehe zao kwa maana hiyo ingeandikwa historia inayojumuisha majina ya wapigania uhuru, majina ya Waisilamu yange "overwhelm" majina ya watu wengine na labda ingeonekana Waisilamu ndio waliopigania Uhuru wa nchi hii kwa wingi--- kitu ambacho hawakutaka kijulikane kwa maslahi wanayoyajua.

Juu ya yote, Kipindi Mwalimu anajiuzulu/anang'atuka alipata kusema juu ya mchango wa Wazee wa kiislamu aliokuwa nao katika harakati za kudai uhuru na dua na kafara wazee hao walizomfanyia Mwalimu ili apate nguvu katika kudai uhuru na bila shaka sababu kuu ya wazee hao kumjumuisha Mwalimu katika harakati za uhuru ni ili isijekuonekana kwamba hao Wazee wa kiislamu walikuwa ni wapigania dini na sio wapigania uhuru. Imekuwa ni vizuri sana kwamba Wengi wa wazee hao ni miongoni mwa wazee wako au ni miongoni mwa watu uliohusiana nao na umeweka ushahidi hai usiokuwa na shaka hii ni kama "ngoma imempata ajuaye kuicheza", kudos Mzee.

Tunashukuru sana Mzee wetu kutufundidha historia iliyofichwa juu ya wapigania uhuru wa KIISLAMU na kama yupo mtu anayewajua wapigania uhuru wengine wasiokuwa Waisilamu au wasiokuwa na dini naye anayoruhusa kutuhadithia habari zao ili historia ihifadhiwe kwa ajili ya vizazi vyetu.

Leo hii ukiwauliza Watanzania wengi juu ya historia ya jina "TANZANIA", na kuhusu nani aliyebuni hilo jina majibu utakayopata ni vichekesho vikubwa, kwasababu historia hii ndogo ya jina TANZANIA imefichwa kwasababu hizo hizo kwamba aliyebuni jina hilo ni Muisilamu.
 
Mokaze,
Ahsante sana ndugu yangu.
 
Huko nje mambo ni tofauti wao maswali wanayoniuliza ni inawezekana vipi historia ya nchi ikageuzwa?
Mohamed, mbona unachanganya wasomaji?
Huko nje unaeleza ni historia ya Nchi, hapa nyumbani unatueleza kitu tofauti, soma hapa chini kauli yako

''Mohamed Said said:
Syll...
Mimi nakuhadithieni historia ya nyumbani kwetu nimeandika kitabu cha historia ya jamii yangu ambayo kabla haikuwapo.''

Wako wapi wasomi wa vyuo vikuu Idara ya Historia wakati haya yanatokea?
Wanataka kujua wanahistoria wamefanya nini baada ya kusoma historia ya uhuru kama nilivyoiandika.
Si akina Shivji wameandika wakaja kukuhoji baada ya hapo ''ukanuna' hawakuandika ulivyotaka. Ukadai 'wamepotosha'' au umesahau
Nawaeleza kuwa baadhi ya walimu wanawakataza wanafunzi wao kufanya rejea kwenye kitabu changu.
Wananiuliza kwa nini wanafanya hivyo?
Ilmuradi wanashangaa.
Wanakila sababu ya kushangaa kwasababu hukuwaeleza ukweli.

Wao wanajua ni historia ya Tanganyika kumbe wewe unajua ni ya 'nyumbani kwetu nimeandika kitabu cha hostoria ya jamii yangu ambayo kabla haikuwepo''

Mohamed, Wanafunzi watafanya vipi reference ya '' historia ya nyumbani kwako'' kwa mujibu wako. Kuna kosa gani kwa wahadhiri ambao pengine leo wanakusoma na kubaini historia pendwa au ngano hii inahusu Familia.

Mag3
 
Mohamed, mbona unachanganya wasomaji?
Huko nje unaeleza ni historia ya Nchi, hapa nyumbani unatueleza kitu tofauti, soma hapa chini kauli yako

''Mohamed Said said:
Syll...
Mimi nakuhadithieni historia ya nyumbani kwetu nimeandika kitabu cha historia ya jamii yangu ambayo kabla haikuwapo.''

Si akina Shivji wameandika wakaja kukuhoji baada ya hapo ''ukanuna' hawakuandika ulivyotaka. Ukadai 'wamepotosha'' au umesahau

Wanakila sababu ya kushangaa kwasababu hukuwaeleza ukweli.

Wao wanajua ni historia ya Tanganyika kumbe wewe unajua ni ya 'nyumbani kwetu nimeandika kitabu cha hostoria ya jamii yangu ambayo kabla haikuwepo''

Mohamed, Wanafunzi watafanya vipi reference ya '' historia ya nyumbani kwako'' kwa mujibu wako. Kuna kosa gani kwa wahadhiri ambao pengine leo wanakusoma na kubaini historia pendwa au ngano hii inahusu Familia.

Mag3
Nguruvi...
Kuwa historia hii ni historia ya nyumbani kwetu ndicho kitu kinachofanya historia hii iwe tofauti na zote zilizopata kuandikwa kuanzia Kimambo na Temu (1969), Uloto (1971), Chuo Cha CCM Kivukoni na Shivji at.al (2020).

Msome Daisy hapo chini.
Utangulizi nimeandika mimi:

''Aisha ‘’Daisy’’ Sykes Buruku ni binti ya Abdulwahid Sykes mmoja kati ya wazalendo 17 waliounda chama cha TANU kilichopigania uhuru wa Tanganyika.

Daisy kama anavyofahamika zaidi kwa jina hili, ni msichana wa kwanza Mwafrika kusoma Shule ya Wasichana ya Aga Khan mwanzoni mwa miaka ya 1950 na msichana wa pili kuingia Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki, Dar es Salaam mwishoni mwa miaka ya 1960.

Daisy amefahamiana na wazalendo wengi mmoja wapo akiwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na machifu mashuhuri kama Mangi Mkuu Thomas Marealle waliokuwa wakifika nyumbani kwa baba yake wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Katika kuadhimisha miaka 50 ya kifo cha baba yake, Daisy ameandika makala haya kukumbuka siku zile zilizojenga haiba ya baba yake na ya wazalendo walioshiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kwa miaka mingi Daisy amekuwa akiishi na kufanya kazi nje ya Tanzania.''

Daisy anaeleza:

''Lakini kile ambacho kimeathiri fikra zangu na kubakia na mimi katika kumbukumbu zangu ni kufika pale nyumbani kwa uongozi wa juu wa Waafrika kabla ya uhuru, machifu kutoka makabila mbalimbali ya Tanganyika na viongozi wa vyama vya wazalendo vilivyokuwa ndiyo vinainukia, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi Waafrika katika wa serikali ya kikoloni.

Kutokana na hadhi hii ya baba yangu na umaarufu wake na kule kupenda kukirimu watu, nikawa si mgeni kwa machifu mashuhuri na nikawa nawahudumia walipokuwa mara nyingi wakija nyumbani.

Wageni hawa mashuhuri waliokuwa wakija nyumbani ni pamoja na Mangi Mkuu Thomas Marealle, Machifu Abdiel Shangali, John Maruma kutoka Moshi, Adam Sapi Mkwawa kutoka Iringa, Kidaha Makwaia kutoka Usukuma, Abdallah Fundikira, Harun Lugusha kutoka Tabora, Humbi Ziota kutoka Nzega, Michael Lukumbuzya kutoka Ukerewe na Patrick Kunambi kutoka Morogoro na wengine wengi.

Hawa machifu kwa kawaida walikuwa wakija na wake zao, wanawake warembo ambao hawakuacha kunifanya mimi kuwashangalia.

Nakumbuka katika machifu wale, alikuwapo chifu mmoja na wa pekee mwanamke - Mwami Theresa Ntare kutoka Kasulu Kibondo.

Katika hali kama hii iliyokuwa tabu kufahamika, tukiwa watoto tulipata kujua maisha ya jamii nyingine, lugha zao, utamaduni wa makabila mengi ya Tanganyika kabla ya watu wengi kutoka sehemu nyingine za pwani hawajajua chochote kuhusu watu hawa.

Nilibahatika kukutana na katika utoto wangu na lile tabaka la Waafrika waliokuwa watumishi wa serikali, kundi dogo makhsusi lililokuwa linakua na liliopembuka kwa elimu zao kutoka Chuo Cha Makerere, Uganda na vyuo vingine.

Hiki ndicho kilikuwa kizazi kipya cha Watanganyika wasomi waliohusika na kuasisi siasa fikra ya uhuru itakayopelekea Waafrika kujitawala - Hamza Mwapachu, Zuberi Mtemvu, Mzee John Rupia, Steven Mhando, Dunstan Omari, Dossa Aziz kwa kuwataja wachache.

Kulikuwa pia na tabaka jingine la watu maarufu kutoka Zanzibar kama Ahmed Rashad Ali and Abdul Razak Abdul Wadud ambao walikuwa kama sehemu ya familia yetu.

Siwezi kumsahau Maloo, Mburushi kutoka Congo ya Mashariki ambae alikuwa anakaa nyumbani na baba kwa muda mrefu sana kiasi tuliamini ni mmoja katika familia ya Sykes.

Lakini aliyeshika nafasi ya juu kabisa katika fikra zangu nikiwa mtoto alikuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na ni kupitia kwake ndipo tukapata kujua kwa mara ya kwanza kuwa kuna kabila linaitwa, ‘’Wazanaki.’’

Kila alipokuwa anakuja nyumbani kwetu kuja kwake kulikuwa jambo maalum kulikosababisha minong’ono watu wakizungumza kwa sauti za chini wakipeana taarifa kuwa, ‘’Nyerere anakuja au keshafika.”

Kwangu mimi hii ilikuwa ishara ya kutimiza kazi yangu kwani siku zote nilikuwa nikiambiwa kutengeneza kifungua kinywa cha chai na mayai kila alipokuja nyumbani akitokea Shule ya Mt. Francis, Pugu alipokuwa akisomesha.''

Daisy anaendela kueleza:

''Nakumbuka katika akili yangu ya kitoto kumuona Mwalimu Nyerere akiishi nyumbani kwetu kwa muda katika nyumba yetu ya Mtaa wa Stanley baada ya kuacha kazi wakati marafiki zake wa karibu baba na Dossa Aziz walikuwa wanamtafutia nyumba ya kuishi.

Nyumba yetu ya Stanley kwa kuwa ilikuwa kwenye makutano ya barabara mbili ilikuwa na mjengo wa kipekee kwa nyakati zile.

Nyumba kubwa na yenye vyumba kadhaa ilikuwa upande wa Mtaa wa Stanely na upande wa Mtaa wa Sikukuu ilikuwa nyumba nyingine inayojitegemea ikiwa na sebule na chumba cha kulala hapo hapo.

Ingawa upande huu wa nyumba ilikuwa na nafasi ya kutosha ilikuwa vigumu kwa wanaume wawili wakubwa kuishi pamoja.

Naamini baba yangu mdogo Abbas ambaye alikuwa akiishi kwenye nyumba ile ikabidi ahame aende kweye nyumba yetu nyingine Mtaa wa Kipata au ajibane nyumba kubwa ili Mwalimu Nyerere apate utulivu na faragha katika nyumba ile.

Mwalimu Nyerere na Hamza Mwapachu ni watu walionivutia sana mimi kwa kiwango cha juu kwa namna walivyokuwa wakilitamka jina langu, ‘’Daisy,’’ kwa lafidhi yenyewe ya Kiingereza kama wanavyozungumza Wazungu na hii ikalifanya jina hili langu la utani linigande na liwe ndilo jina langu halisi.

Nikiwa mtoto nakumbuka sana vipi baba akishughulishwa na kutaka kuona kuwa Mama Maria na watoto wake hawakosi chochote kuyafanya maisha yao kuwa mepesi, ya starehe na furaha akihakikisha chakula kinapelekwa dukani kwa Mama Maria kila siku katika duka lake dogo lilikuwapo Mtaa wa Livingstone kona na Mtaa wa Mchikichi, hiki kikiwa kielelezo chake kikubwa kabisa cha huruma na ukarimu wake.

Ilikuwa katika kipindi hiki cha mimi kuanza kupata akili katika kukua kwangu ndipo nilipokutana na wanawake wazalendo waliokuwa wanaochipukia katika uongozi wa Tanganyika, wanawake kama Bi. Lucy Lameck kutoka Moshi, Mary Ibrahim na akina mama wa Kiislam kama Bi. Titi Mohamed, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Hawa bint Maftah, hawa kutoka Dar es Salaam, wote hawa kwangu mimi walikuwa bibi zangu.

Kitu cha kufurahisha ni kuwa hawa akina mama wa Kiislam wote walivutwa katika siasa na Bibi Chiku bint Kisusa, maarufu akijulikana kama Mama Sakina.

Alikuwa Mama Sakina ndiye aliyewapa hawa wanawake wa Kiislam niliowataja hapo juu utambulisho na wakaja kuwa watu maarufu.

Baba yeye ndiye alikuwa kiongozi wa mikakati hii yote kwa sababu bila yeye kuwatia hima kwa kutumia ushawishi wake ingekuwa vigumu kuweza kuwatia hawa wanawake katika kuwahamasisha wanawake wenzao wa Kiislam na wao watoke majumbani kuja mstari wa mbele katika mikutano wakiimba na kutoa vibwagizo vya kuunga mkono TANU na kudai uhuru.

Hili jambo lilikuwa jipya, jambo ambalo katika utamaduni wetu kwa wakati ule halikutarajiwa na ni kinyume katika utamaduni wetu kwa wanawake wa Kiislam kulifanya katika siku zile.

Nimesikia mazungumzo mengi wakati baba na wenzake walipokuwa wakijadili majina na shughuli ambazo hawa akina mama walikuwa wahusishwe ili kuleta mvuto wa kisiasa katika mikutano yao ya TANU.

Nakumbuka vizuri sana jinsi baba alivyokuwa karibu sana na Mwalimu Sakina na ndugu yake Mwalimu Fatna (wote hawa watoto wa Mama Sakina), na jinsi alivyowaleta ndugu hawa karibu na Mama Maria na hawa wakamjulisha Mama Maria Nyerere kwa mama yao na mashoga zake Bi Hawa Maftaha, Bibi Titi Mohamed na Bi Tatu binti Mzee.

Hawa wanawake ndiyo waliomsaidia Mama Maria kufungua hilo duka lake dogo pale Mtaa wa Livingstone kona na Mchikichi, mahali ambako Mama Maria alishinda kutwa nzima akiuza duka lake.

Nikiwa mtoto nakumbuka kwenda kwenye dula lile kila siku mchana kupeleka chakula kwa Mama Maria, ambako hapakuwa mbali kutoka nyumbani kwetu.

Kwa kuwa baba alikuwa anataka ratiba hii yake ya chakula ifuatwe sawasawa kwa wakati wake, wakati mwingine hii ilikuwa changamoto kubwa sana kwa mama yetu, Bi. Mwamvua bint Mashu.''

Bwana Mag,
Ikiwa wewe au yeyote yule ana ukweli zaidi wa huu na aulete hapa barzani tuusome.

Hakika haya yote ni ya nyumbani kwetu wala hatuoni aibu kujifakharisha na historia hii.

Jirani na nyumba hii ya Abdul Sykes ipo nyumba ya bibi yangu na ipo hadi leo ingawa nyumba yote mbele ni maduka.

Si mbali na hapo ilikuwa nyumba ya Mzee Kubhe, Tewa Said Tewa na nyumba ya Ramadhani Fundikira.

Katika historia hii hakika mimi niko nyumbani kwetu.

1648928804103.png

Kulia ni Mama Sakina Bi. Chiku bint Said Kisusa, mke wa Shariff Abdallah Omar Attas, Bi. Titi Mohamed na wa kwanza kushoto ni Bi. Tatu bint Mzee na Julius Nyerere huyo katikati Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wanamsindikiza Mwalimu safari ya kwanza UNO Februari, 1955. Sina majina ya hao akina mama wengine.

Daisy is very informative. Haswa baada ya kusoma kipande hicho juu...itabidi nikanunue Kitabu, kinaonekana kina Hadithi nzuri ya jamii yake na pamoja na kutoa wasifu ulioheshimika. Walakin wake hakutoa uelewa wake wa Kwanini"Watanganyika" na Machifu wa "Makabila" ambayo alikuwa hajawai kuyasikia walitaka kukata minyororo ya Wakuja....Waarabu na Wazungu! Kwani kupigania Uhuru huo wa Kisiasa ulikuwa ni katika kupigania na kuondoa minyonyoro hasi (Wazungu na Ukristo, Waarabu na Uisilamu) ya wakati huo kwa "Watanganyika" ambao mimi naamini kwa dhati ndio ilikuwa adhma ya Wote hao waliotajwa...iwe ni Aliyesilimika na aliye Okoka. Wote walikuwa na adhma moja...Ukoloni na Ukoloni mamboleo na minyonyoro yake yaondolewe. Mengine yatabaki hivyo, Hadithi a
 
Kitu kimoja nilicho na hakika nacho kwa asilimia 100% ni kwamba wale wote wenye mapenzi ya kweli kwa taifa letu la Tanzania wanasita sana kuchangia hii hoja inayofinyangwafinyangwa na huyu anayejiita Mohamed Said. Bila kumung'unya maneno nayaita madai ya Mohamed Said la kutoa elimu ya historia ya kweli ni porojo hatari iliyojaa uchochezi ambayo lengo lake hasa ni kuleta uhasama wa kidini miongoni mwa wananchi. Sijui anachotegemea kufaidika nacho kwa kupanda hii mbegu ya hatari ambayo nina hakika mtu kama Mohamed Said anajua fika madhara yake.

Mohamed Said ni kama kipofu ambaye baada ya kusimuliwa na wazee kwamba tembo ni mnyama mkubwa kuliko wanyama wengi anapata nafasi ya kumpapasa tembo. Kwa bahati mbaya anaupapasa mguu wa tembo na si mwili wote halafu katika imani yake anadai anao uwezo wa kutoa somo kuhusu umbo la mnyama tembo na ushuhuda wake, kuwa tembo ni kama gogo la mti mkubwa, ndio ukweli na anayesema tofauti hajui kitu. Watu wote wanaolalamikiwa na Mohamed Said kuwa walisahauliwa, wengi wao walikuwa wakazi wa Dar es Salaam eneo la Gerezani.

Kabla ya uhuru Tanganyika iligawanywa katika majimbo makuu manane na katika majimbo yote hayo, jimbo la pwani kwa ujumla lilikuwa moja ya majimbo yaliyokuwa nyuma kimaendeleo kiuchumi, kielimu na kisiasa na hiyo ni licha ya kuwa makao makuu ya serikali ya kikoloni yalikuwa Dar es Salaam. TAA ilianzishwa na watumishi wa serikali (civil servants) na kwa wakati wote kazi kubwa ya TAA ilikuwa ni kulalamika ikidai haki ya wafanyakazi bila upendeleo na hasa ubaguzi wa rangi katila utumishi kubwa ukiwa uonevu dhidi ya wazawa, mtu mweusi.

Jimbo la Ziwa ni moja ya majimbo yaliyokuwa mbele kiuchumi, kielimu na kisiasa na kama kuna kitu kinaweza kudaiwa kuwa kilisahaulika katika harakati ya kupigania uhuru ni mchango wa Jimbo la Ziwa (Bukoba, Mwanza, Mara na Shinyanga) Jimbo la Ziwa ndilo lililoongoza kwa idadi ya watu, idadi ya makabila, idadi ya mali asili na idadi ya machifu ambao nafasi yao ilikuwa kubwa tu katika kuhamasisha watu. Moja wa watu ambao mchango wao nitautaja kidogo tu ingawa alifanya jitihada kubwa labda zaidi ya wazee wa Mohamed Said ni Paul "Kishamapanda" Bomani.

Historia ya harakati za uhuru ni zaidi ya porojo za Mohamed Said, watu walipigania uhuru kama Watanganyika na bila kubaguana kikabila, kidini wala kijinsia. Ndio maana mimi sitaki kabisa kuwa na majibizano na huyu Mohamed Said moja kwa moja ila kwa kuwa hoja ileletwa JF, akae tayari kupewa somo kuhusu umbile zima la mnyama tembo na sio mguu moja wa tembo alioupapasa. Hapa mimi nitaongea sana kuhusu mchango wa Jimbo la Ziwa na baadaye kuonyesha jinsi maadui wa nchi yetu wanavyowatumia kidini watu kama huyu Mohamed Said.

Baadaye nitaeleza jinsi Mkoa wa Mara yenye makabila karibu hamsini yalivyoweza kushirikiana bila mfarakano na kuitikia mwito wa Mwalimu Nyerere katika hizo harakati za kudai uhuru. Je mwamko wa wakazi wa jimbo la Ziwa ulikuwaje na mapokezi gani aliyapata kila wakati Mwalimu aliporudi kwenye hili jimbo ambalo idadi ya wakazi wake kwenye miaka ya 50s ilikuwa mara tatu ya majimbo mengi Tanganyika kama Pwani. Pia nitaonyesha ni wakati gani walianza kuyasikia hayo majina anayodai Mohamed Said ya wazee wa Gerezani Dar es Salaam !
Tembo [emoji848][emoji848] GEORGE MARCUS
 
Daisy is very informative. Haswa baada ya kusoma kipande hicho juu...itabidi nikanunue Kitabu, kinaonekana kina Hadithi nzuri ya jamii yake na pamoja na kutoa wasifu ulioheshimika. Walakin wake hakutoa uelewa wake wa Kwanini"Watanganyika" na Machifu wa "Makabila" ambayo alikuwa hajawai kuyasikia walitaka kukata minyororo ya Wakuja....Waarabu na Wazungu! Kwani kupigania Uhuru huo wa Kisiasa ulikuwa ni katika kupigania na kuondoa minyonyoro hasi (Wazungu na Ukristo, Waarabu na Uisilamu) ya wakati huo kwa "Watanganyika" ambao mimi naamini kwa dhati ndio ilikuwa adhma ya Wote hao waliotajwa...iwe ni Aliyesilimika na aliye Okoka. Wote walikuwa na adhma moja...Ukoloni na Ukoloni mamboleo na minyonyoro yake yaondolewe. Mengine yatabaki hivyo, Hadithi a
Syll...
Historia ya uhuru wa Tanganyika ina raha sana kuisoma na ndiyo maana kitabu hiki tunakwenda toleo la tano.

Unaweza ukamsoma ndani ya kitabu hicho hapo chini:

1648932573327.png
Daisy Sykes Buruku, ‘'The Townsman: Kleist Sykes,’' in Iliffe (ed) Modern Tanzanians, Nairobi, 1973, pp. 95-114.

Hii ni sura katika kitabu hicho na aliindika mwaka wa 1968 kwa msaada wa baba yake kutokana na mswada wa kitabu alioandika babu yake Kleist Sykes kabla hajafariki mwaka wa 1949.

Hii ilikuwa Seminar Paper aliyopewa kuandika na mwalimu wake wa Historia John Iliffe, Daisy alipokuwa mwanafunzi University of East Africa, Dar es Salaam, (East Africana seminar paper ya A.D. Sykes ''The Life of Kleist Sykes,'' University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15).
 
Mohamed, mbona unachanganya wasomaji?
Huko nje unaeleza ni historia ya Nchi, hapa nyumbani unatueleza kitu tofauti, soma hapa chini kauli yako

''Mohamed Said said:
Syll...
Mimi nakuhadithieni historia ya nyumbani kwetu nimeandika kitabu cha historia ya jamii yangu ambayo kabla haikuwapo.''

Si akina Shivji wameandika wakaja kukuhoji baada ya hapo ''ukanuna' hawakuandika ulivyotaka. Ukadai 'wamepotosha'' au umesahau

Wanakila sababu ya kushangaa kwasababu hukuwaeleza ukweli.

Wao wanajua ni historia ya Tanganyika kumbe wewe unajua ni ya 'nyumbani kwetu nimeandika kitabu cha hostoria ya jamii yangu ambayo kabla haikuwepo''

Mohamed, Wanafunzi watafanya vipi reference ya '' historia ya nyumbani kwako'' kwa mujibu wako. Kuna kosa gani kwa wahadhiri ambao pengine leo wanakusoma na kubaini historia pendwa au ngano hii inahusu Familia.

Mag3
Nyerere akiijuwa wapi dar wakuja yule, a likaribishwa kwa / na Waislam. Hilo nalo kwako gumu kulielewa? Au mlimkaribisha nyinyi kule misheni kota?
 
Jambo la kwanza hii lugha ya "kupigania" uhuru sio sahihi sana kwa mazingira ya jinsi Tanganyika ilivyoupata uhuru wake. Sisi uhuru wetu ulikuwa ni wa mazungumzo zaidi na wakoloni wetu jinsi ambavyo tungeendesha nchi yetu baada ya uhuru, lugha ya kufaa zaidi ni kutafuta uhuru.

Pili hakuna mtu anayeijua historia ya nchi hii atapinga kwamba Waislamu walikuwa na mchango katika kuutafuta uhuru wa nchi hii, Waislamu walikuwa sehemu ya nchi hii wakati uhuru unatafutwa, wameendelea kuwa sehemu ya nchi na wataendelea kuwa sehemu ya nchi hii kwa muda mrefu vivyo hivyo Wakristo.

Jambo linalopingwa na ambalo halitakubalika ni kutaka kuiwasilisha na kuitafsiri historia ya nchi hii kwa mrengo wa wazee wako tu kama madereva waliotufikisha kwenye uhuru na wengine wote waliobaki walikuwa abiria ambao walikuwa hawajui hata wanaelekea wapi. Huu ni upotoshaji mkubwa, kwa akili za kawaida tu kujadiliana na wakoloni au mabeberu wa kizungu mezani ilihitaji watu wenye elimu nzuri na wewe unafahamu vizuri kundi gani la jamii lilikuwa na elimu nzuri wakati huo.

Jambo lingine huonyeishi dhahiri sababu gani hasa zilimfanya Mwl aliwafute "wazee wako" katika historia, kama ni kweli Nyerere aliwafuta wazee wako ambao wengi kama sio wote ni wa mrego mmoja basi aliwafutwa kama sehemu ya "power struggle" ndani ya chama chake na pia ni sawa tu na ambavyo aliwafuta maswahiba wake wengine nje ya chama wakiwemo wasomi, waandishi, vyama vya upinzani, matajiri mabepari n.k Siuoni msingi wa malalamiko yako kuhusu hawa "wazee wako" tu.
Mjadala huu ulitakiwa uishie hapa kwa maelezo yako!
 
Mjadala huu ulitakiwa uishie hapa kwa maelezo yako!
Kila...
Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kwa hakika ilikuwa imeandikwa na watu wakaamini yale yaliyoandikwa kuwa ndiyo ukweli wenyewe.

Hivi ndivyo ilivyokuwa toka uhuru upatikane mwaka wa 1961.

Mwaka wa 1998 ndipo kikatoka kitabu cha Abdul Sykes.

Kitabu kilikuwa cha historia ya TANU lakini kilikuwa kinaeleza historia ambayo haikuwa inafahamika na wengi.

Wapo waliofurahishwa na historia hii sababu ikiwa ilikuwa nyepesi kufahamika na ilijaa historia za wazalendo wengi.

Wapo waliofadhaishwa na kitabu hiki na sababu kubwa ilikuwa historia hii ilifanya historia zote zilizopata kuandikwa kabla waandishi wake waonekane hawakuwa na ufahamu wa kutosha wa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Hapa ndipo ulipozuka mjadala ambao unaendelea hadi dakika hii ninapoandika.

Wapo wanaouliza maswali kutaka kujua zaidi.

Wapo wanaokuja si kwa lingine ila kusukumwa na ghadhabu kwa nini historia hii imeandikwa?

Kwa nini tusibakie na historia yetu?

Wengi wa hawa wanaishia kumtukana mwandishi.

Kitabu cha Abdul Sykes kipo huu mwaka wa 24 na kinakwenda chapa ya tano.

Vitabu vilivyotangulia vyote vimekufa vimeishia toleo moja.

Toleo la kwanza kwa Kiswahili (2002)

1649089860684.png
 
Stories za binamu yako "Daisy", nazo tuzitambue kama sehemu ya Historia za nchI?
 
Stories za binamu yako "Daisy", nazo tuzitambue kama sehemu ya Historia za nchI?
Huyu Mohamed Said analo tatizo kubwa, Tuliosoma zamani wakati wa mkoloni tulisoma kitabu cha zamani cha historia kilichoitwa Watanganyika.

Ndani ya hicho kitabu makabila yote yaliyojulikana kama Watanganyika wazawa yaliorodheshwa,

Tanganyika haikuwa na Wazulu, Wamanyema, Wanubi wala wengi wa hao wanaodaiwa na mohamed Saidi kwamba eti ndio walipigania uhuru wa Tanganyika.

Shame on you Mohamed Said, uongo wako hakika umebuma na umebakia kutapatapa tu kama mfa maji. Kwa lugha ya FaizaFoxy, nasema unanchekesha.
 
Mag3,
Ikiwa unaniona nina tatizo sawa.

Wapo wanaoniona sina tatizo na ni watu wa maana kiasi hunipa kazi nikaandika na wakachapa niandikayo (Cambridge Journal of African History, Oxford University Press nk.).

Ukiwa unaiona natapatapa wako wanaoniona nimetulia na wanakuja hadi nyumbani kwangu kunifanyia mahojiano.

Back
Top Bottom