Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kazi ya kuunganisha raia waliifanya kina Nyerere miaka ya Awamu ya kwanza yeye kazi yake ilikuwa kuifungua nchi ili marais wanaofuatia wapate urais wa kukuza uchumi.Hakuna lolote lililojificha kuhusu ubaya wa Magufuli katika kufanya mambo kama haya.
Magufuli hakuwa kiongozi wa kuwaunganisha raia; ilikuwa ni kama raha kwake kuona mifarakanyo ndani ya jumuia!
Huu ni ujinga uliopita kiasi. Tangu lini ugawaji wa mikoa au wilaya unafanywa kwa kutumia kigezo cha kuhesabu makabila? Mtu mzima ovyo, mkabila mkubwa!unagawa mikoa minne iwe mkoa wa CHATO, hao watu wa Chato REgion watakuwa wahaya, wasukuma ama warwanda?
Kubomoa misingi yote ya watu kuwa na mahusiano mazuri kati yao wewe unayaita "kukuza uchumi"?Mbona unapenda sana kujidhalilisha na mawazo ya namna hii!Kazi ya kuunganisha raia waliifanya kina Nyerere miaka ya Awamu ya kwanza yeye kazi yake ilikuwa kuifungua nchi ili marais wanaofuatia wapate urais wa kukuza uchumi.
Kuundwa mikoa mipya kadri muda unavyokwenda zipo faida zake. Sisi wa Ngara tunaijua faida ya mkoa wa Chato. Utakuwa karibu kwetu kulinganisha na mwendo wa kuitafuta Bukoba mjini.
Ukiiongelea mikoa ukiwa Dar huwezi kuelewa hii mikoa mipya inakwenda kuongeza kitu gani kipya. Ni mpaka uwe mwenyeji wa sehemu husika ndio utaelewa.
Inaongezeka mikoa, lakini lugha ya taifa inabakia ile ile kiswahili na muingiliano wetu wa kimakabila ni ule ule wa siku zote.
Ni shida sana, ilivyoletwa kigamboni na ubungo watu hawakulalamika, Ila kuundwa Chato itakuwa ni ukabila!!
Wengi huwa wanaongea wasichokijua kwa undani, from Kakonko mpaka Ujiji ni masaa 5, from Kakonko to Chato almost masaa 2 na nusu, sawasawa na watu wa ngara, mtu anatoka Kabanga anaenda Bukoba mjini kwa shida ya kimkoa watu hawaoni haya!
Moa wa Shinyanga ilikuwa si mkubwa sana by then lakini namna ulivyokuwa umekaa ilikuwa shida wakaamua kuugawa, Arusha pia ikazaa manyara, Rukwa ikazaa katavi, mikoa iliyobaki ni Tabora na Morogoro, mtu yuko Malinyi na ulanga anakuja Morogoro mjini safari ya masaa zaidi ya 8, ndani ya mkoa mmoja.
Katika kuundwa mikoa tunaamini serikali unaona umuhimu wake ndio maana wanaona waongeze eneo kiutawala
Haiwezekani Ndio maana kuupata mkoa wa Chato inabidi wilaya tano ziunganishwe.Kama ni hivyo kila wilaya iwe mkoa sasa
Haiwezekani Ndio maana kuupata mkoa wa Chato inabidi wilaya tano ziunganishwe.
Hivi bila kugawa mikoa huduma hazisogei!?? Manyara imetengwa na Arusha nini cha maana kimefanyika!??Hakuna ubaya kugawa mikoa kama itarahisisha kupeleka huduma za kijamii karibu zaidi kwa wananchi, cha muhimu kusiwe na upendeleo tu, bado Morogoro na Tabora kuna uhitaji wa kuigawa zaidi ili kuwasogezea huduma wananchi.
Ndio maana sisi "tusio na dini " ytunasema Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Yesu lihimidiwe!Yan magu angekua Rais kwa miaka 10 na ili mingine ndungai na kundi lake waliotaka aongezewe hii nchi ingekua kitu cha ajabu sana
ambapo JIWE na wenzake waroho wa madaraka ndio walikuwa wanatupeleka huko.Ukweli kabisa Majimbo yalituunganisha na kuwa wamoja kwani Jimbo moja lilikuwa na Makabila zaidi ya matatu. Sasa hii mikoa ukiitaja tu haraka haraka unapata hisia ya Kabila fulani hapo.
Hili swali linatakiwa waulizwe warogho wa madaraka, yaani hii nchi kuna vichaa wachache wanatupelekesjha, :Hivi bila kugawa mikoa huduma hazisogei!?? Manyara imetengwa na Arusha nini cha maana kimefanyika!??
SUKUMA GANG walikuja kwa nguvu sana , Saa hii "remote ya Msoga " inasambaratisha huo mtandao wa SUKUMA GANG.Ndo vizur , ifikie hatua tuje tugawane kila mtu chake , ili kudhalilishana kikabila kupungue ..... Ili tuone ukanda gani utaumia , mana sasa inaonekana hii nchi ni ya watu Fulani , wakikosekana serikalin wanaumia
Wananchi walipiga kelel kuomba Mkoa? Pumbav kabisa!Ombi la kuwa na Mkoa wa Chato tulilisikia wakati wa Msiba wa JPM na halikuwasilishwa na Serikali bali Wananchi. Kama ni zuri au baya, tuwaachie wataalam wa Serikali waamue. Otherwise ni umbea na kueneza chuki.
pwani , moro na Tabora igawiwe ili nini?Binafsi nisingekuwa na tatizo kama mikoa mipya ingetokea Morogoro, Tabora au Pwani.
Tena Morogoro unapatikana mkoa huko wa Kilombero, Ifakara, Malinyi, Mbingu, Ngeta, Mlimba...wala hauibi wilaya wala eneo la mikoa mingine.
Hakuna mgogoro wakati wa ugawaji wa mipaka. Kunakuwa na migogoro ya ardhi katika hili zoezi la umegaji ardhi.
Ila Chato aisee hapana! Hii nchi yetu sote
Everyday is Saturday............................... 😎
jiwe aliwachukia sana, sijui walimtenda nini,Ningeshangaa kama ungemaliza kuandika uzi wako bila kuwataja Watu wa Kilimanjaro[emoji23][emoji23]
Alikuwa na wivu wa kike yule jamaajiwe aliwachukia sana, sijui walimtenda nini,
Wacha tugawane cake ya taifa ifikie na makabila wasiotegemea kuushika urais.pwani , moro na Tabora igawiwe ili nini?
Upumbavu tu na kutengeneza nafasi za kisiasa.
mimi ningekuwa mwansiasa nikiingia madarakani narudisha mikoa inakuwa 10 tu na ukabila unakufa.
Leo ukigawa mkoa wa kilimanjaro, unapata mkoa wa Pare na Chagaa, kesho upare watadai hawa waSame na hawa mwanga, watagawana tena, ni upumbav tu.