Historia ya uundwaji wa Mikoa Tanzania

inauma sana, alafu kuna nyegere wanasema wanatetea legacy ya mwenda zake, hivi wanajua tulivyopigwa na huyu jamaa.?
 
Hakuna ubaya kugawa mikoa kama itarahisisha kupeleka huduma za kijamii karibu zaidi kwa wananchi, cha muhimu kusiwe na upendeleo tu, bado Morogoro na Tabora kuna uhitaji wa kuigawa zaidi ili kuwasogezea huduma wananchi.
Sababu za kisiasa hizi.kwa nini hizo huduma zisipelekwe huko waliko sasa
 
Sisi sote ni watanzania tena huru kwahiyo tujitahidi sana tunapotoa hoja zetu au maoni yetu tuhakikishe hatukandamizi kabila au dini ya mtu..
 
Pole sana, Tanganyika wakati tunapata uhuru ilikuwa na Majimbo tisa, siyo manane kama unavyotaka kudanganya. Yalikuwa majimbo manane kabla ya mwaka 1959. Ilipofika mwaka huo Jimbo la Ziwa liligawanywa na kupata jimbo la Ziwa magharibi na kufanya nchi kuwa na majimbo tisa hadi uhuru wa Tanganyika mwaka 1961. Aidha, mwaka 1974 wakati wa utawala mwl Nyerere iliundwa mikoa ya Lindi baada ya kugawa mkoa wa Mtwara, Dar es Salaam baada ya kugawa mkoa wa Pwani Rukwa baada ya kuchukua Mpanda toka Tabora na Sumbawanga toka Mbeya.
 

Na mikoa ya Iringa, Rukwa na Ruvuma iliundwa mwaka gani? Na hakuna mkoa unaoitwa Sumbawanga!
 

Upo sahihi kabisa!
 
MWAKA 1966 NYERERE aliunda mikoa 15 nayo ni:-
1. Kilimanjaro
2. Arusha
3. Pwani .
4. Dodoma
5.Tanga
6. Kigoma
7. Mara
8. Mbeya
9. Morogoro
10 .Mwanza
11. Ruvuma
12.Shinyanga.
13. Singida
14 Tabora
Tuambie nani aliiunda mikoa ya;
  1. Iringa
  2. Dar
  3. Mtwara
  4. Lindi
  5. Rukwa
  6. Kagera
 
Na mikoa ya Iringa, Rukwa na Ruvuma iliundwa mwaka gani? Na hakuna mkoa unaoitwa Sumbawanga!
Mkoa wa Rukwa makao makuu Sumbawanga. Wakati unaundwa mkoa huu mwaka 1974 walichukua wilaya ya Mpanda iliyokuwa mkoa wa Tabora na wilaya ya Sumbawanga iliyokuwa mkoa wa Mbeya ukaundwa mkoa wa Rukwa na makao Makuu ya mkoa huo yalikuwa Sumbawanga.
 
Ukiona limwanasiasa linapigania kugawa nchi Jua Halina uwezo!!! JKn angeweza kufanya butiama mkoa!!!! BWM angeweza kufanya masasi mkoa!!! JK angeweza kufanya chalinze mkoa!!! Hawajufanya
 
Ukiona limwanasiasa linapigania kugawa nchi Jua Halina uwezo!!! JKn angeweza kufanya butiama mkoa!!!! BWM angeweza kufanya masasi mkoa!!! JK angeweza kufanya chalinze mkoa!!! Hawajufanya
 
Tufanye kila kijiji kiwe mkoa
 
Tukisema kila kanda itumie resources zake vipi
 
Kama jambo haliathiri maendeleo ya jamii na wanajamii hata kama watasema kila wilaya iwe mkoa it's ok. Hatujengi nchi jirani tunajenga Tanzania..
 
Bado hoja yako haina mashiko, kwa nini usipiganie maendeleo yapelekwe wilayani na kwenye kata ambako ndiyo jirani na watu? Asilimia 85 ya watanzania wako vijijini, hivyo huduma muhimu ziwafuate huko badala ya wao wazifuate huko mikoa ni. Mimi naweza kwenda likizo kijijini Moshi na nikamaliza likizo yote bila ya kwenda Moshi mjini kwa sababu huduma muhimu pale Kijijini na kwenye kata zinapatikana.
 
Naona kuna sababu za kisiasa zaidi(udhibiti)kuliko maendeleo juu ya umegaji wa mikoa.
 
Hii mbinu ya divide and rule ccm wanaitumia kwelikweli!
 
umenogesha jukwaa na kuendeleza nilichoandika, sasa nakukubali sema lugha umetumia ya mbagala magengeni.
 
Mimi nashangaa huwezi sikia Marekani wanayagawa majimbo yao.Sababu ya kugawa mikoa zimekaa kisiasa zaidi yaani wagawe kisha watawale.Eti huduma ziwe karibu na wananchi wakati gharama za uendeshaji zinaongezeka hii ni akili mufilisi kabisa.Kwa taarifa yenu wazungu wanafurahia sana tunayoyafanya.
Jimbo la Texas la marekani ni kubwa sawa na nusu ya Tanzania lakini maendeleo yapo.
Waafrika tutazidi kutwaliwa tu.Hivi mnafikikiri kwanini wazungu hawataki United States of Africa? aliyokuwa anaitaka Ghadhafi na ndio maana wakamuua.Mtoa post ahsante kuona hilo na post yako nzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…