Historia ya Wanyakyusa kufahamika zaidi kuliko Wasafwa ambao ni wazawa halisi wa Jiji la Mbeya

Dah umezunguka mzee Hadi chimala. Kumi Bora unapakumbuka ?
Aise sana mbeya nimeizunguka sana maana nlipomaliza la saba nkatupwa mbeya...
Chimala nlisoma shule ya msingi pale
Nimakaa sana kwa mzee mmja maarufu wanamuita mjerumani alikuwa kama mzungu fulani
Nkarudi dar form 1 tena nkatupwa mbeya mjini kule nako nkakaa kwa mzee mmja tulimpa jina la gaddafi
Unajuwa zamani utotoni nlikuwa mtukutu sana,aise hizo familia nlizopelekwa ilikuwa si mchezo yaani kazi kazi
Ila mkoa wa mbeya ulinijenga sana aise.....
Kuzunguka mbeya nlizunguka maana mzee hyo alikuwa na chai maharage sasa kila jumamosi ilikuwa lazima na mm niingie mzigoni kama konda kuchukua hela za abiria
So mkoa ule nlitembea kiaina
Tulikuwa tunaenda mpaka santilia huko milimani

Ova
 
Huu uzi umenifanya niwakumbuke wababe wa zamani hapo mbeya mjini
Wakina dr zimwi na akina fike [emoji1]

Wanyakyusa,walikuwa wanapenda sana huu usemi" we dogo hebu njoo"

We dogo ,we dogo [emoji1]

Ova
 
Kwa sasa sisi Wanyakyusa na Wasafwa ni kitu kimoja, tunaoana na kuheshimiana. Tumekuwa ndugu na tunachangamana kila maeneo, milimani na mabondeni.
 
Daah we mwenyeji. Mjerumani alishakufa na eneo lishauzwa kwa tajiri mmoja hivi amejenga Sana pale. Pia mji umeamia kule mlimani viwanja viliunzwa Kama njugu
 
Daah we mwenyeji. Mjerumani alishakufa na eneo lishauzwa kwa tajiri mmoja hivi amejenga Sana pale. Pia mji umeamia kule mlimani viwanja viliunzwa Kama njugu
Yah nlikaa pale,nakumbuka walikuwa wasabato kindakndaki aise
No soda no chai ,vyakula chemshachemsha....
Pale nlijifunza kazi nyingi sana kuanzia kilimo mpaka kuendesha vyombo vya moto
Sema sasa mjerumani aka mzee Charles kesi alizokuwa analetewa kila siku haziishi maana kila siku mm nlikuwa na misala
Sema licha ya kuwa na misala kazi pale nlikuwa napiga sana
Yah nlisikiaga paliuzwa
Ila kukaa mbeya kulinijenga sana sana

Ova
 
Ndio ndio. Wasabato kanisa wamejenga kubwa Zaidi
 
Daah we mwenyeji. Mjerumani alishakufa na eneo lishauzwa kwa tajiri mmoja hivi amejenga Sana pale. Pia mji umeamia kule mlimani viwanja viliunzwa Kama njugu
Alafu Kyle kutoka nyumbani kwa mjerumani kama unakwenda mlimani
Alikuwopogi mama mmj mganga anaitwa hidaya,ilikuwa ukikaa usiku unasikia ngoma znapigwa watu wanaimba na kulia [emoji1]
Kuna siku nlijiuliza tukasema Acha twende usiku huko ilikuwa saa saba usiku,tulitoroka nyumbn pale kwenda kule...aise kufika tulikuta watuuu
Wakatustukia wacha watufukuze,kesi ikaletwa kwa mzee tena pale [emoji1]
Nlipokuja ondoka hapo chimala wazee wa kiburushi walifurahi sana
Maana walikuwa wanaona kama nawaharibu watoto zao....
Ila ilipopita kama mwaka hivi ahhh aise wenyewe wakaanza kunimiss
[emoji1] huko
Na pia nliishi pia kwenye zile kota za FAO igurusi,napo hko familia nliyokuwa nakaa nayo wakanitimua
[emoji1]
Ila mbeya nlipapenda sana

Ova
 
Wanyakyusa ni wavivu na wana kiburi na majivuno sio rahisi kukuza mji. Ila kuupaisha ujulikane hilo wanaweza sana tu.

Wasafwa mpaka kesho wanaogopa kuchangamana, huko ituha wako kibao waliohamia miaka hiyo wakidhani ni mbali na mji. Lakini sasa hivi lami imewafikia mpaka mlangoni. Wageni wanajazana hapo ituha, mijengo inaangushwa kila leo.
Wengine kama ilivyo kawaida wanahama wanakimbilia milimani zaidi, na akihama anauza kila kitu anaenda kuanza upya huko milimani .

Hawapendi kuchangamana, walau kizazi hiki cha sasa ila pia bado wasafwa kuchangamana ni tatizo kubwa. Bado wanakimbilia kujenga milimani wakae peke yao. So muda mrefu ituha itamilikiwa na wageni.
Hata viongozi wao tu sio wasafwa, aisee hili kabila.
 
Upo deep dogo ww ni wa soko matola, forest au isanga???
 
Isyonje ya zamani kulikua na baridi makete isubiri, naona mabadiliko hali ya hewa saivi pa kawaida sana

Isyonje kwenye cabbage kama tako la kajala 🤠
 
Huu uzi umenifanya niwakumbuke wababe wa zamani hapo mbeya mjini
Wakina dr zimwi na akina fike [emoji1]

Wanyakyusa,walikuwa wanapenda sana huu usemi" we dogo hebu njoo"

We dogo ,we dogo [emoji1]

Ova
Hadi leo hadi kesho imekua tabia
 
Mkuu Ngonde hata leo ipo.
Ndonde area ni eneo la Unyskyusani linalotokea Kaskazini ya Malawi, Kyela yote na sehemu za Rungwe.
Ingawaje leo ukitamka mnyakyusa wa Ngonde utaeleweka kuwa unamaanisha mnyakyusa wa sehemu tambarare za Kyela na Malawi Kaskazini.
Wanyakyusa wa milimani Tukuyu, Busokelo na huko Mwakaleli wanajulikana kama ni wa Kumwamba(milimani).

Wanyakyusa wa Ngonde na wale wa Kumwamba, kitabia wako tofauti ingawaje lugha ni moja.
Wale wa Ngode ni wepesi kujidai, kujiamini na ni waongeaji sana.
Wanawake wa Kyela wengi ni "weupe" na wanapendeka.
Wanyakyusa wa Kumwamba wengi ni weusi na ni wakulima wa ndizi sana.
Wale walio mipakani na makbila ya wasafwa, wakinga, wapenja, waandali, wengi wamechanganya damu. Hawa kitabia ni watu wafanyakazi kweli kweli, hawana utani na akiamini kitu ambacho anaona ndiyo ukweli, si rahisi kumchanganya akili.

Kwa ujumla, wanyakyusa wote huamini ukweli na wako very loyal.
Ila kiujumla huwezi kumdharau mnyakyusa, hata kama ni masikini hana kitu.
Kwa ujumla, wanyakyusa nawa eneo lote la nyanda za juu kusini, ni wapambanaji na hawaogopi ku risk maisha yao.
Wakoloni waliwahi sema ,they are fierce fighters.
Kitu cha ziada, wanawake wa kinyakyusa ni wachakarikaji kuliko wanaume.
Na ukimzingua au kumdanganya katika mapenzi anaweza kukukung'uta.
 
Hio sifa ya mnyakyusa hapendi dharau kwa kiasi flani kulingana na ninavyowajua wanyakyusa huwa inatumika sana na wanawake wa kinyakyusa kuficha ile tabia ambayo ni maarufu kwa baadhi yao kuwa na viburi na kutaka usawa na wengine hata ubabe mbele ya wanaume, hata wewe umekiri wazi hio point ya mwisho kwamba wapo wenye nguvu za kushushia vipigo wanaume. kwa upande wa wanaume umkute anasema hapendi dharau ni nadra sana maana mwanaume wa kinyaki huwa anacheza na mazingira tu, akiona sehem flan haifai anajiweka pembeni.

Kwenye elimu wanyakyusa wanaupiga mwingi tu na wapo maofisini wanakula mema ila kwenye suala la upambanaji kwenye biashara kwa wanyakyusa nikiwa kama mwenyeji niliyeishi hapa Mbeya bado wapo level za kawaida mno, wengi hata biashara wanafanya kwa nidhamu ndogo ya pesa hasa kwenye kushindwa kujibana, ni kawaida kumkuta mama wa kinyakyusa anauza maparachichi lakini ana wigi la bei na anakula chipsi mayai anashushia na pepsi yake, mambo ya kujibana bana wakati kipo kwao ni ngumu, Na hapa wote ni mashahidi hata Mwanjela tu hapo walio tawala na kukua (domainating and growth) ni wakinga na wageni, wanyakyusa wapo ndio lakini unakuta wapo pale pale (stagnant) biashara ile ile, na hii ni sababu kujibana kwao ni ngumu, hata wafanya biashara wengi hupambania watoto wao wasome kwa lengo la kuajiriwa, huko ndio wanaona kwenye uhuru.

wanawake wa kinyaki ni wachakalikaji kuliko wanaume, hii kwakweli nami nimeisikia ila sijathibitisha, maana nao wanaume wanapambana ila nao wanawake wanapambana pia, sijajua kigezo ni kipi hasa kilitumika ila naweza kusema labda ni kwamba kuna jamii nyingi hasa za huku kusini na pwani mwanamke anategemea zaidi kutafutiwa ila kwa wanyakyusa tunavyoona wanachakalika basi ndio watu wanashangaa na kukuza hii ishu sana hadi wengine wanaanza kusema kwamba wanawake wanapiga kazi sana kuzidi wanaume.

Kuhusu wanyakyusa hadi wapewe title ya fierce fighters bado sijajua hilo, Kwa wahehe mkwawa mziki wake ulikubalika, kwa wachaga mangimeli nae alileta resistance si haba, kina Mirambo nao wajerumani walipelekewa moto kimtindo, wakurya hao walitumika kwenye majeshi ya wakoloni, huko Singida nako naskia kuna sehem wakoloni walishindwa kabisa kutawala. Ila kwa wanyakyusa sijawai kusikia hilo, nachojua wajerumani waliingia unyakyusani kwa resistance ndogo waliweza kuwamudu ndani ya muda mfupi tu ila wamishenari walijenga shule, makanisa, mahospitali, n.k.
 
Acha maneno mengi weka bei ya kg moja ya kitimoto hapo mbeya!!
 
Inasemekana mwenye Hotel ya silver stone tunduma ni mswafwa

Kuhusu madon mbeya toka kitambo ni wakinga hata hapo block t walijaa sana

Hivi eland Hotel bado ipo hapo block t

Ova
Hata kama Wakinga ndiyo matajiri wa Mbeya mbona wanaishi maisha duni kuliko maskini Msafwa.

Yule mwenye Paradise Hotel pale Soweto anaitwa Kasisi, alikuwa anaishi nyumba ya tope kule Ilemi hata haikuwa na umeme.

Nashauri Wasafwa waishi kama Wasafwa kuliko kuishi kama matajiri lakini utajiri wa masharti
 
Elimu pia iliwapitia kushoto

Ova
Kwa taarifa yako Chief SECRETARY wa kwanza wa Tanzania huru baada ya Mwingereza kuondoka alikuwa anaitwa Dickson Nkembo, Msafwa kutoka Tarafa ya Iwindi. Utasemaje Wasafwa hawakusoma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…