Historia ya Wanyakyusa kufahamika zaidi kuliko Wasafwa ambao ni wazawa halisi wa Jiji la Mbeya

Kwa taarifa yako Chief SECRETARY wa kwanza wa Tanzania huru baada ya Mwingereza kuondoka alikuwa anaitwa Dominick Nkembo, Msafwa kutoka Tarafa ya Iwindi. Utasemaje Wasafwa hawakusoma?
Nimekubali

Ova
 
Wasafwa wanapenda kukaa milimani
Wasafwa walikuwa ni watu waoga Sana walikuwa wakiona hata gari wanakimbia!
Lakini mleta uzi huu bado hujatuambia asili ya wanyakyusa je wametokea wapi?

Ova
Hakuna Msafwa muoga, wasafwa ni maskini jeuri tu. Futa hii
 
Mbeya ya wanyakyusa .....sema tu Kuna kipind wakoloni walituteka na kutupeleka Malawi .......

Then wasafwa waka dominate hapa mbeya town......but after decolonization bhanyambala ( wanaume )... tukarudi
Huo ni uwongo ambao hautasaidia hata kizazi chako kujuwa historia ya Wanyakyusa.

Wabantu wote ni migrants kutoka Congo desert na Niger Congo basin. Ila nani alitangulia kufika Mbeya mjini ndiyo issue. Wanyakyusa ni mchanganyiko wa movement ya Wapogoro kutoka Morogoro na Makabila yakiyokuwa yanamkimbia Chaka Zulu kutoka South Africa. Sehemu yao ya kwanza ku settle ni Rungwe na Kyela.

Wasafwa migration yao ni kutoka Niger/Congo basin, waliingilia Sumbawanga kutokea Congo desert wakaacha kundi moja linaitwa Wanyika na kuja ku settle Mbeya.

Kwa hiyo jamii ya kwanza kufika Mbeya ni Wasafwa wala siyo Wanyakyusa. Wasafwa wapo Mbeya Jiji, Mbeya Rural, Chunya, Mbarali na sehemu ya Mbozi. Wapo vilevile Tarafa ya Isongole iliyopo Rungwe kama kilometre 20 za kwanza baada ya mpaka wa Mbeya /Rungwe
 
Majina ya koo za kisafwa ndo kama yapi wakuuu...huwa siwajui kabisa....
 
Ni sawasawa na mji wa mbalizi na kabila la Wamalila.

Ila Wamalila nao hawajulikani kisa ni uchache wao
Wamalila siyo kabila bali ni lahaja tu. Sawa na kusema Wanyamanyafu siyo Wasafwa. Kabila hujitambulisha kwa lugha, eneo la kijiografia, utamaduni wa kuoa na kuzikana.

Wamalila wameamua tu kujitambulisha kwa lahaja yao kama kabila lakini ni jamii ya Wasafwa tu. Kwa Wasafwa kuna lahaja zifuatazo:- Waporoto, Waguruka, Wambwila, Wasongwe, Wayole, Wasoha etc

Kama na hao wengine wangeamua kujitambulisha kilahaja basi hakutakuwa na kabila la Wasafwa
 
Mbilinyi ni wakinga original hao.
Mbilinyi kama una maanisha Sugu ni Mpangwa. Ila mama yake ndiyo Mkinga na kalelewa na mama yake Mbeya ndiyo maana Wakinga wanamuona damu yao
 
Majina ya koo za kisafwa ndo kama yapi wakuuu...huwa siwajui kabisa....
Kuna majina yanayoanza na Mwa...
kama ilivyo kwa Wanyakyusa mfano Mwakalila, Mwashoma, Mwanjali, Mwakwenda, etc. Lakini kuna ambayo hayaanzi na Mwa kama Ndele, Mbwiga, Mbwette, Mbanga, Shelela, Mbonile, Mlekani, Malijani, Nkembo, Mboma, Sambwe etc
 
Enzi hizo mzee wangu alikuwa ananunua maeneo kule ituha ilikuwa wasafwa tupu lakini sasa hivi kumekuwa mji na wasafwa hawapo tena.
Ituha wamejaa wasafwa mkuu, ni kwao kule na ni wengi ila wageni tayari washafanya uvamizi.
Kama kawaida yao, baadhi washauza maeneo wamekimbilia milimani.
 

Asante mleta mada kwa hoja zako nzuri sana, ila kuna masuala kadhaa ningependa kuyaweka sawa ama kuyafafanua katika kunogesha mjadala.
  1. Wasafwa ni moja ya makabila machache ambayo yali resist ukoloni (kutawaliwa na wageni wa kizungu) kwa nguvu zote. Kumbuka ukoloni uliambatana na ujo wa elimi na huduma za kisasa za afya, kwa mantiki hii shule zilichelewa sana Usafwani kutokana na kupinga ukoloni tofauti na Unyakyusani. Shule ya kwanza ya misheni nadhani ni Irambo (1920s) tofauti na Rungweama Makete (wilaya jirani) ambako misheni ziliwahi kutokana na wao kutoupinga ukoloni. Hata hivyo, baadhi ya Wasafwa walisoma katika shule hizi ambazo zilikuwa nje ya wilaya ya Mbeya. Kuliweka sawa hili, Ikumbukwe kwamba katibu mkuu Kiongozi wa kwanza enzi za Mwalimu (Nkembo) alitokea Uswafwani.
  2. Wasafwa ni watu wakarimu sana kwa wageni (mpaka leo), suala la kuchangamana na wageni kwao sio ishu kubwa. Wasafwa kiasili ni wakulima na wafugaji, sasa maeneo yao ya kilimo yalipovamiwa wakasogea pembezoni mwa mji ambapo kuna ardhi ya kutosha kuweza kulima na kufuga ili kujikimu kimaisha. Suala hili kwa mtazamo wa wageni linaonekana ni kukimbia mji, sio kweli. Baada ya mfumo wa maisha kubadilika, wamechangamana na wageni mjini Mbeya na maisha yanaendelea. Nikilinganisha na baadhi ya makabila yanayosifika kwa kubagua wageni (yanajulikana) kimsingi Wasafwa sio wakabila kabisa.
  3. Wasafwa ni watu wa kujituma sana kwenye kufanya kazi na kusaka fursa nje ya nyumbani kwao kama ilivyo kwa Wakinga. Hili linadhihirishwa na kusambaa kwao kusaka maisha maeneo mbalimbali. Wapo kwa wingi wilaya za Handeni, Muheza, Korogwe (Tanga) na wilaya za Hai na Siha mkoani Kilimanjaro. Wapo kwa wingi pia wilaya za Nkasi, Sumbawanga (Rukwa) na mkoani Katavi katika kusaka fursa. Hii trend si ya miaka ya hivi karibuni, ni ya miaka mingi sana hapo nyuma.
  4. Wasafwa ndio kabila pekee mkoani Mbeya ambalo kiasili lipo katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya isipokuwa wilaya ya Kyela tu. Naongelea kuanzia Kanyegere, Ntokela, Ndaga kuja Isyonje (Rungwe), Sonyanga kuja Ilongo, Igalako, Ruiwa nk (Mbarali), Chalangwa kwenda Ifumbo nk (Chunya) na wilaya zao za asili ambazo ni Mbeya mjini na Vijijini.
  5. Kuhusu siasa, nakubaliana na mleta mada, si wengi wamejikita katika kusaka nafasi za za juu kisiasa, kunahitajika mwamko sana.
Hitimisho
Ikumbukwe kwamba waliowahi kupata elimu ukanda huu waliwabagua sana Wasafwa kwa kuendeleza ukabila na ubaguzi katika suala la ajira hata kwa Wasafwa wasomi (mada hii ipo hapa JF), si ajabu baadhi ya Wasafwa walibadili ama kurekebisha majina yao ili kupata nafasi za ajira, maana wangetumia majina yao halisi wasingepata. Hili linajulikana toka kitambo sana. Unyanyasaji wa aina hii pia wafanyiwa sana watu wa Pwani kutoka kwa wageni wahamiaji.
Tuendelee kujadiliana!
 
Huyo mzungu alikuwa basha wako siyo maku wewe
 
Kiujumla Mbeya ni kwetu, lakini Mbeya hawana mwamko kabisa wa kujenga nyumba nzuri na mipango miji inayoleweka.
 
Mkuu nakubaliana kwa kiasi na maoni yako.
Ikumbukwe kuwa kabila la wasfwa na wahehe wamefanya kazi kubwa sana kutokea enzi za machifu kama Merere kuondoa au kukinga utumwa kuingia Mbeya.
Wasafwa walikuwa na jeshi kubwa sana lililowazuia waarabu kupita nyanda(plains) za kuanzia Mbarali, Kapunga na Chimala.
Ndio maana utakuta nyanda za juu kusini kuelekea Mbozi, huwezi kukuta influence kubwa za waarabu, na hata wazungu.
 
Ni kweli unachokisema, nmekaa Mbeya sana muda nilipata kuambuwa unachokisema! Afu masafwa ni wazuri sana ni ma Black Beauty kuliko ndugu zao...
 
Hebu nipe majina 10 ya Wasafwa ambayo ambayo distinctly unajua huyu sio Mnyakyusa.
 
Sijui kwanini wanyakyusa wanajisikia sana na kupenda kujisifia ilihali ukimwangalia unaona kabisa ana kipato na maisha ya chini sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…