Historia ya Wanyakyusa kufahamika zaidi kuliko Wasafwa ambao ni wazawa halisi wa Jiji la Mbeya

Historia ya Wanyakyusa kufahamika zaidi kuliko Wasafwa ambao ni wazawa halisi wa Jiji la Mbeya

Hakuna kilichoharibika wakae wanyakyusa ama wasafya yote ni sawa,hakuna aliyewafukuza wasafya ni wao wenyewe na ubinafsi wao .by the Way "survival for the fittest"
 
Mimi nikajua unataka kutuambia kuwa wanyakyusa ni watu wa Zimbabwe. Au nikajua unataka kusema kuwa Yale maendeleo makubwa ya mkoa mbeya yameletwa na Wasafwa na siyo Wanyakyusa kama tujuavyo. Kumbe ni historia ya machifu na uhuru
 
Ni sawasawa na mji wa mbalizi na kabila la Wamalila.

Ila Wamalila nao hawajulikani kisa ni uchache wao
 
Mbeya n mkoa wenye makabila mengi kuna wamalila pia wamesaulika kabisa
 
Maana ya neno MBEYA unaipata kwenye lugha gani?

Ha ha ha!
Kuna wanyakyusa Malawi-wanaitwa wa Ngonde, Zambia na hata Zimbabwe.
Namfahamu jamaa akiitwa Ngonde kwa jina la UKOO na ni msafwa, ana ndugu Malawi, anazungumzia NGONDE Empire mara nyingi nikikutana naye, anasema ilikuwa kubwa na hata sasa ipo kubwa isipokuwa kutokana na mambo ya lugha sijui Lahaja, Rejesta, jin linatoholewa, mara Gonde, Gondwe, Ngonde n.k

Historia inasemaje kuhusu wamisionari na mkoa wa Mbeya? Isije kuwa kama Wachaga, Wahaya na Umisionari, wameingilia huko, wakawapa madini wakwanza, basi wakajiona viiiiichwa, kumbe ni hali ya kutangulia tu.
 
Wasafwa wazee wa kulima viazi.
Sema wasafwa wa hapo karibu na Kiwira (Mbeye 1, Ntokela n.k ) wanapwaya sana kwenye usafi na wamama wana bass nzito kama wanaume! Ila wana roho nzuri sana kwa wageni!
 
WASAFWA NDIO WAZAWA HALISI WA JIJI LA MBEYA, KILITOKEA NINI MPAKA WANYAKYUSA WA NJE YA JIJI KUFAHAMIKA NDIO WENYEJI?

Yani hii Tanzania nzima ukiuliza Mbeya inakaliwa na kabila gani fasta mtu anakujibu wanyakyusa lakini ukweli ni kwamba wasafwa ndio wenyeji, mtu wa nje anaweza asijue hii mbeya wakinga ndio wenye maendeleo kiuchumi na ndio wafanyabiashara wakubwa wanaomiliki maduka mengi, mahoteli, viwanda, makampuni, n.k. lakini ukimuuliza mwenyeji wa hapa mbeya ni nani, atakujibu fasta tu kwamba ni wanyaki, kilotokea nini hadi ikawa hivi?

ni kwamba nchi ilipopata uhuru kulikuwa kuna wageni wengi walianza kuja na kuhamia hapa jijini kwenye makao makuu ya mkoa m wa Mbeya, wageni hawa kwa kiasi kikubwa walikuwa ni wanyakyusa ambao ni wazawa wa wilaya za Rungwe na Kyela zilizopo ndani ya mkoa wa Mbeya, shida ikaja kwamba wasafwa wakiona wageni walikuwa hawataki kuchangamana nao walikuwa wanahamisha makazi kwenda sehem ambayo wapo peke yao, wanyakyusa walizidi kujaa hapa mjini na ikawa usumbufu kwa wasafwa kuhama hama ikafikia kipindi wengine wakaanza kukimbilia milimani waishi kivyao vyao.

matokeo yake hapa mjini makabila ya ziada yaliyokuja kama wanyiha, wandali, wakinga, wahehe, wangoni, wabena, n.k. wao wakawa wanajua huu mji ni wa wanyakyusa maana wasafwa wengi walikimbilia milimani ikawa vigumu kuwajua wao ndio wenye mji.

Laiti wasafwa wangebaki kwenye huu mji huenda wangekuwa na maendeleo sana kuzidi hata wanyakyusa, mji huu ulikuwa ndio makao makuu ya mkoa wa Mbeya lakini hii bahati wakaichezea na ni ngumu kurudi tena. wasafwa waliletewa hivi vitu vizuri hapa mjini ila wakavikimbia.

-hapa mjini serikali ilijenga shule nyingi ila wasafwa walizikimbia

-ajira nzuri enzi hizo zinahitaji elimu hata za shule ya msingi au form 4 zilikuwepo mjini wao zikawa zinawapita

-mji ulianza kujaa na kukawa na fursa za biashara ambazo wasafwa wangeweza kupata pesa lakini kujitenga kwao kukaliacha soko wazi kwa wageni.

-madaraka, vyeo na teuzi serikalini za kuongoza mji huu wakawaachia wageni ambao nao walitumia bahati hii kuwekana maofisini na kupeana vyeo.

-viwanja vingi waliviacha ama kuviuza na kukimbilia milimani kusiko hata na huduma za jamii, n.k.

-baadhi ya wasafwa waliorudi hapa mjini ama waliobaki maeneo ya karibu wakaanza kujitambulisha ni wanyakyusa kwa kuogopa aibu na wengine kufikia hatua ya kufuta majina ya ukoo ili kuepukana na aibu, hii tabia hadi sasa inaendelea.

Ni historia yenye kusikitisha ila ina funzo kubwa sana, mkataa kwao hugeuka mtumwa.

Mwisho kwa kuhitimisha naweza kutoa ushauri kwa wasafwa kwamba historia haiwezi kubadilika itabaki kwajili ya kujifunza lakini mnachoweza kubadilisha ni muda wa mbele (future) kwa maamuzi mnayoweza kuanza kuyatekeleza sasa ili angalau mrudishe hadhi, mapendekezo yangu kwenu:

- wasafwa mzingatieni sana elimu pambanieni na ikibidi mjinyime watoto wasome.

- mjipanue na kutafuta fursa mpya za kibiashara na kujiajiri, Mbeya ni jiji lina watu wengi wenye mahitaji mengi muangalie ni sehemu zipi mnaweza kuchota pesa.

- muwe na bidii ya kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa na uongozi kwenye huu mji wenu, mpambanie nafasi za kupaza sauti ya kero zetu wageni wa mbeya na zenu wazawa halisi wa mbeya.

-msaidiane na kubebana ili walio chini nao wawe na maendeleo, roho za umimi na ubinafsi haziwezi leta maendeleo.

-mjivunie asili yenu ya usafwa, kuna baadhi ya wasafwa hufuta majina yao ya ukoo na wengine kukana kabila lao, huu ni ujinga, jivunie kabila lako, nyumbani ni nyumbani kwa jirani sio kwako.

bila kufanya haya hakuna kitachobadilika..
Wasafwa nao wajitutumue kujitangaza tamaduni zao.

Wasitegemee watu kutoka nasaba nyingine kuwabeba. Wajibebe
 
Inasemekana mwenye Hotel ya silver stone tunduma ni mswafwa

Kuhusu madon mbeya toka kitambo ni wakinga hata hapo block t walijaa sana

Hivi eland Hotel bado ipo hapo block t

Ova
Naona ni wazi kabisa Mbeya hujaenda miaka, Mbeya imebadilika sana mkuu, hio erland hotel ilishakufa walijenga tawi la karibu la chuo kinaitwa teku. kwa sasa hapa Mbeya kuna hoteli kama Tughimbe, Desderia (ya sugu), Mdope, usungilo, n. k hizi zote nilizotaja wamiliki ni wakinga.

hotel hio ya silver stone sijajua maana ipo mkoa mpya wa Songwe, mambo yalivyobadilika kwa sasa siwezi shangaa nayo ikawa ni tbt zilizopendwa
 
Back
Top Bottom