Historia ya Wimbo wa Taifa wa Tanzania na mtunzi wake

Me siamini. Maana neno Tanzani limepatikana baada ya muungano
 
Alitunga huo wimbo wa Taifa mwaka gani?
Na vipi kuhusu bendera ya Taifa nani aliyedesign?
 
Kumbe tune siyo yetu tulifanya kucopy kuna haja ya kuwa na wimbo wetu kama taifa
 
Nadhani uliweke hili clear mkuu... ni wimbo wa msanii wa South afrika sio wa taifa la South africa (hadi 1997)....maana wao wameanza kuutumia mwaka 1997 ilihali sisi ulishakuwa wa taifa.

Asante kwa maelezo.
 
Ninavyofahamu mimi ni kuwa wimbo huu mwanzo ulikuwa ni wa kwaya kwenye makanisa ya waafrika huko SA na lilipoanza vuguvugu la kisiasa, wimbo huu ukaanza kutumiwa na vyama vya kisiasa kabla na baada ya mikutano ya kisiasa[kabla ya kupigwa marufuku]
 
Kwa nini tuige au kuazima wakati watunzi wazuri tunao tu? BTW asante sana kwa info.
Slow learner;

Binadamu wote ni sawa na Africa ni moja, ulifundishwa hii jargon? bado unafikiria M-south siyo ndg yako? kwa nini mnapenda tuige sana wazungu kuliko waafrica?

Angetunga mzungu aaah! ungeona ana maana, mmesharogwa nyie!

Yaani tokea Africa Magharibi ya ikweta mpaka Mashariki yake towards South tunapashwa kuwa nchi moja tu, lazima tigane tuzidi kupendana.
 
Ha ha para ya mwisho ndio umemaliza kabisa kamanda. Ubarikiwe
 
Kuwa na wimbo unique wa taifa sio tija kwa sasa. Labda tuanze na elimu inayoendana na mazingira yetu, elimu kwa ajili ya taifa letu, Tena kwa lugha yetu kama wachina, warusi, wajerumani, wafaransa n.k, Nyimbo haiwezi kutuletea maendeleo yoyote.
 
Wanahistoria mfu kabisa...Wimbo wetu huu ambao una beti mbili umechanganywa zaidi ya nyimbo tatu. Ubeti wa kwanza ni maneno ya Kizulu na Ngoni ingawa ata na Boers wapo . Ayo maneno yalitumiwa sana na Chama cha Ukombozi cha Afrika Kusini SANC badae ANC.

Ubeti wa pili unaosema Tanzania umetokana na makabila mawili ambayo yaliwai kudai Uhuru na Taifa lao kutoka kwa Ujerumani na badae Waingereza. Wahaya asa wale waziba na wayoza walitaka Taifa lao huru wakawa na bendera na huo wimbo ambao kuna maneno mpaka leo yamechukuliwa.

Ulianza hivi.

Omukama Lugaba bera eiyanga lyaitu

Bera abantu baryo na abatwazi ba Buhaya.

Nimeishia apa..ili ukitaka zaidi ebu tembelea Idara ya PSPA pale UDSM au History apo apo UDSM lakini pia unaweza kumuuliza Bashiru ambae ameshiriki utafiti huu.
 
Naomba jibu maana huu wimbo huu. Nani kautunga na una maana gani?
 
Mtunzi alikuwa Muitaliano wa Shirika la Waconsolata wa Kanisa Katoliki pale Tosamaganga, Padre Musso!
 
Alikuwa Padre Musso, Muitaliano wa Shirika la Consolata la Roman Catholic! Ali-edit pale Tosamaganga Mission ambayo sasa ni Sekondari ya Tosamaganga na ya kwanza kabisa kusajiliwa Tanzania iliwa na usajili wa S.01
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…