Historia Yangu yenye kujaa ukakasi na uhusiano wangu na Member huyu wa JF

Historia Yangu yenye kujaa ukakasi na uhusiano wangu na Member huyu wa JF

1970 kazaliwa bimkubwa wangu nae kapishana mwaka mmoja na mzee.....humu ndani unaweza kubishana na baba yako mzazi kabisaa
Huyo ni dogo tu kama anabisha aprove hapa ...Hakuna mtu ana miaka 50 na kuendelea akawa analeta content za kukejeli dini isiyokuwa yake..Anajifanya muislamu wa mchongo.

Huyo ni wale vijana waozurura huko ughaibuni kama chimakeke🤣🤣hawana impact kazi kushangaa.
 
Nimezaliwa mwaka 1970, na kupata Elimu yangu ya Msingi hapa hapa Dar Es Salaam na Sekondary Nje ya Dar Es Salaam katika shule zinazomilikiwa na Makafir. Kiukweli ilikuwa changamoto kidogo kutokana na Mzee wangu kuwa ni mtu anayeshika sana Dini.

Kwa wale watu walioishi Kimanga, Mji Mpya watakuwa wanaufahamu Msikiti wa Ngunde. Mzee wangu alikuwa hakosi kuswali pale swala zote tano. Nakumbuka hata kipindi kile Sheikh Shariff Majini amekuja Kimanga mmoja ya watu ambao walisupport sana ile mihadhara alikuwa mzee wangu.

Mimi nmecheza mpira Uwanja wa Twiga nikichezea Twiga na akina Omary, Mluguru, Galabu n.k kwa wenyeji wa maeneo hayo watakuwa wanakumbuka.

Sheikh Shariff alifanya sana mihadhara ule Uwanja wa Twiga. Nilikuwepo kipindi hicho sehemu za mbele kabisa. Akina Mazinge watakuwa wananikumbuka pia sababu nlikuwa mtu wa imani sana. Mwaipopo na Abubakar. Hawa hawawezi nikumbuka.

Mzee wangu alikuwa ni mmoja ya wazee wenye kauwezo flani yale maeneo tukiwa na nyumba nzuri miaka hiyo yenye fensi. Na tulifanikiwa kwenda shule tofauti na wenyeji wengi ambao waliishia darasa la 7 au hawakumaliza shule. Sekondary O Level nlisoma ya Serikali na A level nikaenda ya Makafir.

Mimi nlikaa na wahuni... Ile mitaa ilikuwa na wahuni sana. Tukicheza mnanda, mchiriku n.k mpaka kipindi imekuja anzishwa team ya Begeju baada ya Twiga kuvunjika. Begeju ikawa ina wahuni wavuta bhangi na Twiga ya wastaarabu. Ilikuwa hizi teams zikikutana moto lazima uwake.

Leo hii nimefikaje hapa JF? Na wengi wananiona kama si Muislamu (nakubaliana nao) na huwa natamani sana niweze kuwa Mkristo ingawa bado sijaweza kuwa sababu ya aina ya maisha ambayo nimezoa na imani iliyonikuza. Huwa nawaambia watu mimi Role Model wangu kwa tabia zangu zote ni Muhamad. Huwa sitanii.

Lakini Elimu ilinisaidia sana kufunguka na kusoma kwa kureason hivi vitabu. Nlianza kusoma Biblia kwa lengo la kupata mistari ya kupotoshea Wakristo na kuwananga. Badala yake ikaanza kunifundisha vitu ambavyo vilianza kunifanya nione kuna maeneo mengi sikuwa sawa katika imani yangu ya awali.

Mzee wangu alikuwa anajua kuyaita majini na kuongea nayo. Alikuwa analetewa hata watu awapige kisomo na alikuwa na mambo mengi sana ambayo mimi yalikuwa yananitatiza. Lakini all in all alikuwa swala 5 na muislamu kweli kweli. Aliwachukia sana Wakristo na mara nyingi alikuwa akisema alitamani waondolewe wote Duniani. Hii ilikuwa inanishangaza. Nlisoma shule ya Wakristo. Tena RC. Nakumbuka ambavyo waliheshimu sana imani za sisi waislamu wachache.

Hatukuzidi 13 pale shuleni. Lakini walihakikisha hatulishwi nguruwe na vyombo ambavyo vinatumika kupikia Nguruwe havichanganywi na vya ujumla. Walitupa darasa la kuswalia. Walituheshimu sana. Mimi hili lilinipa shida. Sababu nlitamani tuchukiane wao hawakutuchukia wala kututenga. Walikuwa nasi vizuri tu. Ilinifanya nitake kujifunza Biblia. Sikujua ambayo ngekutana nayo huko mbele. Huwa najuta sana kwa uamuzi huo wa kusoma Biblia mpaka leo


Nitaendelea...
Ina maana Samia akimaliza uongozi wake 2030 una 60..
 
Makafiri, 😩😩

Hili limeniliza sana,

Hili limeniumiza mno,

Katika nyuzi nilizoumia, huu umeniumiza,,

Hivi hizi dini, Yaan unatamani mkristo asiwepo kisa kutokufuasa Allah?

ama waislamu wasiwepo kisa hawaamini kwenye neema na wokovu ? Aseeh binadamu tuna shida mahali

cc Kiranga Infropreneur min -me

Haya tunaoamini kwenye Imani

Uislamu umekamilika Mash'Allah 😍 cc Poor Brain Busu la Kenge kipenzi chetu Hussain Ali akiutetea 🥺 💔,
Haya kwenye neema na wokovu cc Setfree Meneja Wa Makampuni

Haya kwenye jopo la udaku

trudie Mrs none Binti wa zamani
Kuna jamaa mmoja kule kani tag kwenye uzi wa uuzaji wa nguruwe aiseee leo nimejua kukasirika
 
Aaah hata waislam Kuna makafiri usitushekenge wewe
tapatalk_1495297805963.jpg
 
Back
Top Bottom