Kwenye huu mjadala napendelea sana kuwa msomaji tu. Lakini hii posti umeandika utumbo hadi uzalendo umenishinda. Umeandika sijui manyege, unawaita wenzio viruka njia, mara wametukana wazazi, haya maneno yako yanathibitisha vipi uwepo wa Mungu au usahihi wa Quran!?
Ile post yako ndefu pale juu haiwezi kuachwa bila kupingwa.
Unasema Quran ndiyo imekuja na nadharia ya vitu kama dunia kuwa mviringo na eti chanzo cha vitu ni maji!!, Mbona huu ni uwongo wa mchana kweupe!!!??, Quran imekuja takriban miaka 600 baada ya Yesu, mbona kuna wanafalsafa na wanasayansi waliowahi kuishi kabla ya Yesu walishakuja na hizi nadharia??, kutojua hili, ni uthibitisho kuwa wewe unaeaccuse wenzio kuwa hawana elimu ndio huna elimu na inawezekana umekaririshwa Quran tu ndio maana ukaamini kuwa ndio ya kwanza kuja na hizo nadharia.
Mwanafalsafa Thales aliyeishi miaka 624 hadi 546 Kabla ya Yesu ndiye aliyeleta nadharia kuwa chanzo cha vitu vyote ni maji, Yeye alifanya utafiti na kugundua kuwa kuna kitu kinachounganisha vitu vyote pamoja na kutofautiana kwa vitu hivyo, akagundua kuwa kitu hicho ni maji na akafikia hitimisho kuwa maji ndiyo chanzo cha kila kitu.
Hata hivyo, nadharia hiyo ilipingwa na mwanafunzi wake aliyeitwa Anaximander, yeye alithibitisha kuwa chanzo cha vitu ni lazima kisiwe na mipaka wala ukingo, contrary to water, akahitimisha ni ni HEWA na wala sio maji.
Wanafalsafa wengine wengi, wakiwemo Democritus na Leccippus wamelifanyia kazi hili na kupendekeza chanzo cha vitu ni ATOM.