Hitimisho la Kesi: Licha ya hukumu kutolewa, hakuna official statement niliyokabidhiwa mahakamani

Mkuu hapa mbona kama umenishtua, heb nirud kuisoma tena ile hukumu nione kama kuna hiyo kitu ya kuitwa decree.
Lakin the strange thing ni kwamba lasf week nimekabidhiwa talaka already na nimeambiwa kuwa natakiwa kwenda Rita nikiwa na risiti nilioandiiiwa mahakamani baada ya kufanya malipo ya serikali (nilifanya kwa simu baada ya kupewa controll number).
Au ndio kusema siku hiz taratibu zime change?? Maana sijaambiwa kitu mahakaman kuhusu kwenda Rita na hiyo decree zaid ya hiyo risiti ndio walinisisitiza. Pia waliambia (mahakamani) kuwa nisii laminate talaka kabla ya kwenda Rita maana kuna vitu wataviandika nyuma ya talaka.

Nitakujuza acha nisome kama hukumu ina hiyo decree
 
Pole. Hukumu haijachapwa hiyo. Hukumu ikitokabutapewa DIVORCE DECREE,
Ukishapata decree usisahau kuisajili RITA
DOohhh..haya mambo mbona magumu namna hii?
Kwann kuna tofauti ipi kati ya hukumu na mwenendo wa kesi?

Na mbona nimepewa hatibya Talaka?
 
DOohhh..haya mambo mbona magumu namna hii?
Kwann kuna tofauti ipi kati ya hukumu na mwenendo wa kesi?

Na mbona nimepewa hatibya Talaka?
Mwenendo wa case ni recordings zote za kwenye file. Yaani documents, ushahidi mliotoa, recordings za hakimu etc. hiyo haikuhusu sana (japo Kuna wakati hasa kwenye rufaa ni muhimu). Hukumu (judgment) ndo maamuzi ya hakimu. Hii inakua na details zote kuhusu case pamoja na hukumu husika na sababu za hukumu. In your case kutoa au kutokutoa talaka.

Document ya mwisho ambayo ni ya msingi zaidi inaitwa Decree. Hiyo ndo talaka yenyewe Sasa. Ni kama summary ya hukumu.
 
Why wamenipa hati ya Talaka sasa mkuu,nisaidie ufafanuzi
Usinambie hii ngoma bado ngumu na mimi najua am done!! πŸ˜‚
 
Hii case nafaikiri imefatiliwa na watu wengi Sana mpaka sasa imetazamwa na watazamaji 20k
Niseme tu kuwa humu nimefunguliwa vitu vingi sana ambavyo sikuvijua before na nimesaidika sana. Maana it was my first time kushtakiwa na kupelekwa mahakaman.
Humu nimekutana watu ambao wamenishauri mambo mengi kisheria wengine mpaka ku exchange contacts Pm na kunisaidia maelekezo mengi mnoo ambayo sikua najua ningetakiwa kufanya nini kwenye hii scennario.

Am grateful kwakwel
 
Good to hear Mkuu.

Hakika JF naweza kusema ni familia kubwa Sana .

Pia na sisi tunakushukuru Sana kwa kukiweka kisa chako cha Ndoa, kwani kimekuwa na funzo kubwa Sana .

Na ukifatilia wasomaji wengi wa kisa hiki ni guests ambao hata hawana I'd means tatizo ni kubwa Sana katika jamii.
 
Ahahahah..sikutegemea kama tungeendelea na huu muendelezo maana imagine toka uzi ukihusu sijapewa hukuma mpaka leo nimeweka copy ya Talaka. 😁
 
Mkuu hili kwangu ni jipya umepewa hati ya talaka kabla ya hukumu!

Sasa mahakamani mlienda tena kufanya nini? Hiyo Ngoma imeisha. Hiyo hati ndo decree.....
Ndio maana nikauliza au taratibu now days zime change?
Maana nikisoma ule mwenendo wa kesi, is like ndio hukumu yenyewe. Nitaipandisha hapa labda unaweza pata idea.
 
Bro chukua mkeo mrud nyumban huo ndio ushauri wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…