Hivi anavyofanya Rais Samia ndio kuua upinzani

Hivi anavyofanya Rais Samia ndio kuua upinzani

Hamnaga akili nyingine zaidi ya kuua upinzani? Ukifa wewe unapata nini au mumeo anacheo huko ccm??
Tujadili Sera na vitu vya maana kwa ustawi wa nchi na watu wake acheni upumbafu
Wanafikiri mtu akiwa mpinzani basi si mtanzania tena au pengine anakuwa shetani. Ni akili zilizooza kabisa
 
Upinzani hauwezi kufa hata kwenye familia upinzani unakuwepo sio lazima uuone wazi wazi..

Upinzani huanzia kwenye fikra sio yote asemayo baba ndio ya mdomoni itakua sawa na moyoni ..wanaweza kufanya ila wasifanye kwa moyo na ufanisi ukawa duni huo ni upinzani pia
 
Tokea Rais Samia aingie madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Naona kila anachofanya anapata sifa kutoka kwa watu wengi hasa wa upinzani.

Kwa maono yangu hivi anavyofanya mama ndio kuua upinzani, sio kuwakamata na kuwatisha na kuwabambikia kesi na kuwafunga, mama akiendelea hivi mpaka 2025 upinzani utakua na wakati mgumu hasa kwenye nafasi ya Urais.
Wewe ulitaka afanyaje labda? Aendelee kukandamiza wapinzani?
 
Hapa home wife alikuwa kwa DIKTETA....Sasa leo mimi namsapoti MAMA.....zamu kwa zamu
 
Mafanikio ya Samia ni habari mbaya sana kwa Lisu maana 2025 hana chake tena.

Ccm itaendelea kupeta

Bavicha wote sasa hivi wanashangilia ccm
 
Mwendazake na Samia wote ni ccm kenge wewe
Punguza jazba twende pole pole.

Nikweli Samia Na Magufuli Wote Ni CCM nakubali Ila Vipi Kuhusu Mitazamo Yao Inafanana Au Ni Tofauti?.
 
Tokea Rais Samia aingie madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Naona kila anachofanya anapata sifa kutoka kwa watu wengi hasa wa upinzani.

Kwa maono yangu hivi anavyofanya mama ndio kuua upinzani, sio kuwakamata na kuwatisha na kuwabambikia kesi na kuwafunga, mama akiendelea hivi mpaka 2025 upinzani utakua na wakati mgumu hasa kwenye nafasi ya Urais.
Mama ni civilized educated na matured kelele za bawaba hazimnyimi usingizi.
Chura hawamzui kunywa maji
 
Kutenda haki sio kuua upinzani. Sasa tutaenda kwenye ushindani wa hoja na sera ambao ni msingi wa femokrasia ya vyama. Tunaondokana na siasa za kibabe na kibeberu.
Kwa hoja na haki ccm saa nne asubui chali
 
Naona kila anachofanya anapata sifa kutoka kwa watu wengi hasa wa upinzani.
Lkn anatengeneza upinzani kwa "push gang". Na ndiyo maana unasema anapata sifa -hasa upinzani-. Maana yake baadhi ya wanaCCM mnamchukia sana.
 
Tokea Rais Samia aingie madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Naona kila anachofanya anapata sifa kutoka kwa watu wengi hasa wa upinzani.

Kwa maono yangu hivi anavyofanya mama ndio kuua upinzani, sio kuwakamata na kuwatisha na kuwabambikia kesi na kuwafunga, mama akiendelea hivi mpaka 2025 upinzani utakua na wakati mgumu hasa kwenye nafasi ya Urais.
Hapo anawafufua wanyonge wenye mawazo mbadala.
 
Mama hauwi upinzani bali anajiua mwenyew na chama chake. Hawa watu hawana jema, jinsi uwabebavyo ndio jinsi uumiavyo. Jk aliwapa uhuru wa kufanya mambo yao na aliwabeba katika mambo fulani lkn mwisho wa siku kuwabeba kwake kuligeuka kaa la moto kwa yeye mwenyewe. Huruma yake kwao iliwafanya wamwite dhaifu, mpenda sifa nk. Kwa sasa mama anaona raha kushangiliwa kama alivyoanza kushangiliwa JK mwaka 2005 wakati anaingia lkn mwisho wa siku sifa hizo zikageuka majuto kwake. Ngoja siku atagusa masilahi yao ya kisiasa na kimaisha. "Ukicheza na mbwa sana ujiandae kufuatwa msikitini". Tuvute subira kidogo tuone baada ya mwaka mmoja hali ya siasa hapa nchini itakuaje ila atapoanza kushambuliwa asije kutumia nguvu kubwa kuwatuliza, maana atakuwa amewapa mwenyew njia ya kufanya hivyo.
Kwa hiyo wewe uliktakaje?
 
nyani wala mahindi na kisa cha mkulima,aliyekuwa akiwafukuza.

walilaani sana pilika za mwendazake juu yao,kumbe alisaidia hata wasikike wapo.

huyu mama ndio mbaya maana hatumii nguvu kuyeyusha upinzania kabisa.anajua aguse wapi,nyumbu walipuke kwa shangwe.
Anaweza yeye akabaki 2025 ila ule msitu ulochipukizwa katikati ya Dodoma utavunwa zaidi ya nusu.yao
 
Anaweza yeye akabaki 2025 ila ule msitu ulochipukizwa katikati ya Dodoma utavunwa zaidi ya nusu.yao
hiyo nafasi ya kufyeka wanaipata wapi wako wanademka tu saa hizi,walilia nafasi ya kufanya siasa bila kubanwa wanayo na wanaimba mapambio ya kumtukuza mama.
 
Tokea Rais Samia aingie madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Naona kila anachofanya anapata sifa kutoka kwa watu wengi hasa wa upinzani.

Kwa maono yangu hivi anavyofanya mama ndio kuua upinzani, sio kuwakamata na kuwatisha na kuwabambikia kesi na kuwafunga, mama akiendelea hivi mpaka 2025 upinzani utakua na wakati mgumu hasa kwenye nafasi ya Urais.

..Mnakosea sana kufikiria " kuua " upinzani.

..Watu wenye mawazo mbadala hawawezi kupotea ktk ardhi ya Tz au hapa duniani.

..Rais Samia au CCM haiwezi kutatua changamoto zote ktk maisha ya Watz.

..Kutokana na UKWELI huo hakuna uwezekano wa kutokuwepo chama au kikundi cha watu kitakacho-propose namna bora au tofauti ya kushughulika na matatizo ya Watz.

..Mama Samia anaweza kuajiri Watz wote walioko mtaani. Lakini anaweza kutokea "mpinzani" akajenga hoja kwamba mishahara ni midogo, au mazingira ya kazi siyo mazuri,...na wananchi wakamchagua wakavutiwa na hoja zake.

..Again, upinzani hauwezi kufa, au kukosa hoja, unless Watz wameacha kufikiri.
 
Back
Top Bottom