Hivi anavyofanya Rais Samia ndio kuua upinzani

Hivi anavyofanya Rais Samia ndio kuua upinzani

Tokea Rais Samia aingie madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Naona kila anachofanya anapata sifa kutoka kwa watu wengi hasa wa upinzani.

Kwa maono yangu hivi anavyofanya mama ndio kuua upinzani, sio kuwakamata na kuwatisha na kuwabambikia kesi na kuwafunga, mama akiendelea hivi mpaka 2025 upinzani utakua na wakati mgumu hasa kwenye nafasi ya Urais.
Anayo fanya SSH ndo upinzani walikua wanataka Haki,Usawa na Utu, upinzani unakufaje au ndio una imarika baada ya uovu kufichuliwa?
 
Mama hauwi upinzani bali anajiua mwenyew na chama chake. Hawa watu hawana jema, jinsi uwabebavyo ndio jinsi uumiavyo. Jk aliwapa uhuru wa kufanya mambo yao na aliwabeba katika mambo fulani lkn mwisho wa siku kuwabeba kwake kuligeuka kaa la moto kwa yeye mwenyewe. Huruma yake kwao iliwafanya wamwite dhaifu, mpenda sifa nk. Kwa sasa mama anaona raha kushangiliwa kama alivyoanza kushangiliwa JK mwaka 2005 wakati anaingia lkn mwisho wa siku sifa hizo zikageuka majuto kwake. Ngoja siku atagusa masilahi yao ya kisiasa na kimaisha. "Ukicheza na mbwa sana ujiandae kufuatwa msikitini". Tuvute subira kidogo tuone baada ya mwaka mmoja hali ya siasa hapa nchini itakuaje ila atapoanza kushambuliwa asije kutumia nguvu kubwa kuwatuliza, maana atakuwa amewapa mwenyew njia ya kufanya hivyo.
Ulilelewa vibaya kuaminishaa kua upinzani ni uadui
 
Ulilelewa vibaya kuaminishaa kua upinzani ni uadui
Anaeamini kuwa upinzani au siasa ni uadui ni yule aliekimbilia ulaya kuomba watanzania tuwekewe vikwazo na kunyimwa misaada kwa sababu zake za kisiasa, bila kujali kwamba vikwazo hivyo vitaweza kuathiri watanzania wengi wakiwemo ndugu zake na wapinzani wenzake. Kitendo cha kulishwa bure ulaya, kuishi bure ulaya na kuongea utumbo wake bure katika nchi za ulaya kilimfanya asahau kabisa ndugu zake na wanachama wake ambao vikwazo hivyo vingewaathiri pakubwa.
 
Punguza jazba twende pole pole.

Nikweli Samia Na Magufuli Wote Ni CCM nakubali Ila Vipi Kuhusu Mitazamo Yao Inafanana Au Ni Tofauti?.
Bavicha ni mwendo wa kusifu na kuabudu ccm tu
 
Bavicha ni mwendo wa kusifu na kuabudu ccm tu
Kwa sasa bavicha ni ccm B, bila shaka mwaka 2025 ccm na chadema watajiunga dhidi ya chama cha Zito ambacho ndo kitasimama kama chama cha upinzani.
 
Back
Top Bottom