Hivi CHADEMA wamemuelewa kweli Rais wetu? Kwamba hicho wanachozunguka kukihubiri ni ukiukaji wa malengo ya kuruhusu mikutano ya hadhara

Lazima uwe taahiri kuchagua kuwa kama CUF ya Lipumba au ACT ya Zito. CCM wangependa sana vyama vyote viwe hovyo kama ulivyovutaja ili wavitumia kadiri wanavyotaka.

Umaweweseka sana Dr Ujinga. Hujajikomboa kifikra na kinafsi. Wanachofsnya CHADEMA ni sahihi kabisa, ndivyo vyama vya siasa kwenye nchi za kidemokrasia vinavyofanya.

Baada ya kashfa ya viongozi wa Serikali, wote kutoka upande mmpja wa Jamhuri, kuhusika katika kuwezesha uporwaji wa bandari za Tanganyika, CHADEMA Baraza Kuu walikaa, na miongoni mwa maazimio ilikuwa ni kuwaeleza wananchi kilichotendeka, na athari yake kwa Taifa na vizazi vijavyo. Na hicho ndicho kinachoendelea. Wewe endelea kuwaeleza wananchi uzuri wa huo mkataba, CHADEMA wataendelea kuwaeleza wananchi juu ya ubaya wa huo mkataba mbaya kabisa kwa Taifa letu.
 
Endelea kuota. Ndoto ya mwendawazimu haijawahi kuwa na athari.

Ifute au mshauri Rais aifute hiyo CHADEMA mara moja ili tujue ni rahisi kiasi hicho.
 
HAKI ya KIKATIBA kufanywa kuwa huruma ya Mwenyekiti wa CCM inanikumbusha kiburudisho cha DUMB and DUMBER
 
Dr. Akili tumia akili japo kidogo. Lengo chama chochote cha siasa ni kuchukua mamlaka ya dola. Chama chochote cha upinzani duniani kote utafuta udhaifu wa serikali ya chama kilichopo madarakani ili kukidhoofisha ili kisichagulike.

Kuwapangia wapinzani kitu Cha kufanya au kuongea ni utoto ktk siasa. Hapa kwetu hatujafikia viwango vya ukosoaji ukinganisha na nchi nyingine.
 
Chawa OP
 


Hapa unafanya siasa nyepesi.

Maswali haujibu unabaki kuuzunguka mbuyu.

Jitahidi kusimamia hoja unapoileta mezani.



Kuhusu Lissu kuwa kibaraka wa wazungu, Serikali ya Tanzania iliyopo madarakani sasa ni kibaraka wa nani?

Kuna nchi na kiongozi Afrika hii ambae sio kibaraka wa nchi za Magharibi? Yupi?



Nakuuliza tena, ina maana msajili wa vyama vya siasa hajui tofauti ya wanasiasa na wanaharakati?

Mbona hata Onyo hajawapa hao CHADEMA kuacha harakati wafanye Siasa kwa mujibu wa sheria na miongozo ya vyama vya Siasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…