Hivi CHADEMA wamemuelewa kweli Rais wetu? Kwamba hicho wanachozunguka kukihubiri ni ukiukaji wa malengo ya kuruhusu mikutano ya hadhara

Hivi CHADEMA wamemuelewa kweli Rais wetu? Kwamba hicho wanachozunguka kukihubiri ni ukiukaji wa malengo ya kuruhusu mikutano ya hadhara

Pole sana ndugu yangu, kumbe hujui tofauti ya vyama vya siasa na vikundi au vyama vya wanaharakati (activists). Goja nijaribu kukuelewesha:

Vyama vya siasa hufanya kazi kwa utaratibu niliouelezea hapo juu kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi pamoja na mila, desturi na maadili ya wananchi.

Kama likitokea jambo linaloelekea kutokuwa na masilahi ya taifa, hususani hili la mkataba wa IGA; chama hufanya kwanza utafiti wa kina wa kisayansi wakitumia watalaamu wao mahili. Baada ya hapo vikao vya chama (CC na NEC) hukaa kuchambua kwa makini utafiti huo na kutoa tamko la chama lililosheheni weledi mkubwa kuhusu jambo hilo pamoja na maoni na mapendekezo ya utatuzi wake. Vyama vya siasa huwa havikurupuki. Upinzani wa kisiasa siyo sawa na mchezo wa ngumi wa kurushiana makonde. Upinzani wa kisiasa ni wa kushindanisha nguvu za hoja na siyo hoja za nguvu.

Vikundi ama vyama vya wanaharakati havina sheria wala kanuni na taratibu za kufanya kazi yao. Wao hufanya kazi kwa matukio. Havifanyi utafiti. Wao wakisikia jambo lo lote lililofanywa au kukusudiwa kufanywa na serikali, hulirukia na kuishambulia serikali kwa nguvu kubwa bila hata uthibitisho wa kile walichokisikia. Huropoka maneno makali na mabaya kwa serikali na kwa viongozi wa serikali yakiwamo matusi na maneno mengine machafu. Hushambulia serikali ndani ya nchi na nje ya nchi na taasisi za kimataifa hususani European Union, World Bank na kadhalika. Lengo ni kuichafua nchi na kuitishia iwekewe vikwazo vya kimataifa kwa kile serikali ilichofanya. Wanaharakati hawatambui kwamba nchi yetu ni sovereign state yenye uhuru wa kuendesha mambo yake. Hawa wanaharakati hupeleka haraharaka mambo yetu BBC na Al Jazera na kadhalika. Wanaamini Tanzania inatawaliwa na mabeberu wa Ubiligiji, Ujerumani, USA na EU.

Chama cha chadema kiko kundi hili la wanaharakati. Hakina tofauti yo yote na vikundi vingine vya wanaharakati hususani kile cha Sauti ya Watu kinachoendeshwa na Maria Sarungi ambacho Dr Slaa kajiunga. Raisi Salmia kawaelekeza wanachotakiwa kufanya cha siasa. Sidhani kama wamemuelewa. Maamuzi ni ya kwao, waendelee kuwa chama cha wanaharakati au wajirekebishe na kurudi kuwa chama cha siasa kama vile chama cha Zitto Kabwe au kile cha Prof. Lipumba. Wakiendelea kuwa wanaharakati wasitegemee kupata ha mbunge mmoja 2025.
Lazima uwe taahiri kuchagua kuwa kama CUF ya Lipumba au ACT ya Zito. CCM wangependa sana vyama vyote viwe hovyo kama ulivyovutaja ili wavitumia kadiri wanavyotaka.

Umaweweseka sana Dr Ujinga. Hujajikomboa kifikra na kinafsi. Wanachofsnya CHADEMA ni sahihi kabisa, ndivyo vyama vya siasa kwenye nchi za kidemokrasia vinavyofanya.

Baada ya kashfa ya viongozi wa Serikali, wote kutoka upande mmpja wa Jamhuri, kuhusika katika kuwezesha uporwaji wa bandari za Tanganyika, CHADEMA Baraza Kuu walikaa, na miongoni mwa maazimio ilikuwa ni kuwaeleza wananchi kilichotendeka, na athari yake kwa Taifa na vizazi vijavyo. Na hicho ndicho kinachoendelea. Wewe endelea kuwaeleza wananchi uzuri wa huo mkataba, CHADEMA wataendelea kuwaeleza wananchi juu ya ubaya wa huo mkataba mbaya kabisa kwa Taifa letu.
 
Everybody knows this except you and likes. Rais kawapa onyo, hamukumuelewa kwa sababu katumia lugha ya kiungwana ambayo kwenu ni ngumu kuielewa. Angalikuwa Jiwe angaliwaambia kwa lugha mnayoijua na kuwapiga ban ya kufanya mikutano ya hadhara mara moja, mkashitaki huko kwa mabeberu wenu.

Mkiendelea na huo uanaharakati wenu hata raisi huyu atawachoka na kuwapiga ban kufanya hiyo mikutano, na ana uwezo wa kukifuta hiko chama mkashitaki kwenye hiyo mnayoiita dunia. Hakuna anayewaogopa. Bahati nzuri Mr Mbowe ameshajirekebisha kwa kiwango kikubwa, hata katibu mkuu wenu. Amebakia hasa Bw. Tundu Lissu, yeye anaweza kudhibitiwa pekee yake.
Endelea kuota. Ndoto ya mwendawazimu haijawahi kuwa na athari.

Ifute au mshauri Rais aifute hiyo CHADEMA mara moja ili tujue ni rahisi kiasi hicho.
 
4-Dumb-and-Dumber-Laughing-Gif.gif
HAKI ya KIKATIBA kufanywa kuwa huruma ya Mwenyekiti wa CCM inanikumbusha kiburudisho cha DUMB and DUMBER
 
Rais aliruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ili vikatangaze sera za vyama vyao kwa wananchi ili kuwavutia kuwaunga mkono kwenye harakati za kushika dola kwenye chaguzi zijazo.

Chama cha siasa ni sera yake na si vinginevyo. Rais aliruhusu ruzuku ya Serikali kwa Chadema iliyokuwa imegomewa ya bilion mbili (inasemekana) kwa mwezi kuanza kutolewa.

Cha ajabu Chadema wamekuwa wanazunguka kila mahali wakipinga serikali kwa kila kitu inachokifanya, wakikashifu, kudhalilisha na hata kuwatutana na kuwatezwa viongozi wakuu wa serikali ikiwamo raisi wa nchi, kuchochea vurugu na uvunjaji wa amani. Wamekuwa wakitishia kwamba watakiwasha hapa ndani na duniani kote kwani waungwa mkono na dunia aka mabeberu wa dunia ie EU, USA etc.

Wamekuwa wakidandia masuala hususani ya maboresho ya katiba ya nhi, mkataba wa bandari zetu na DP World na uboreshaji wa hifadhi ya Ngorongoro na kuyafanya kuwa ndiyo sera yao wakati kuna vyombo halali vinavyo shughulikia mambo haya.

Leo Rais kasema na kutoa maelekezo, sidhani kama hawa chadema wamemuelewa. Watapinga maelekezo haya kama kawaida yao. Ikumbukwe kwa mila zetu, tamaduni zetu na sheria zetu, maelekezo ya mkuu wa nchi ni maagizo na ni amri. Hawa jamaa watayapinga na kumteza aliyeyatoa. Ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu.
Dr. Akili tumia akili japo kidogo. Lengo chama chochote cha siasa ni kuchukua mamlaka ya dola. Chama chochote cha upinzani duniani kote utafuta udhaifu wa serikali ya chama kilichopo madarakani ili kukidhoofisha ili kisichagulike.

Kuwapangia wapinzani kitu Cha kufanya au kuongea ni utoto ktk siasa. Hapa kwetu hatujafikia viwango vya ukosoaji ukinganisha na nchi nyingine.
 
Rais aliruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ili vikatangaze sera za vyama vyao kwa wananchi ili kuwavutia kuwaunga mkono kwenye harakati za kushika dola kwenye chaguzi zijazo.

Chama cha siasa ni sera yake na si vinginevyo. Rais aliruhusu ruzuku ya Serikali kwa Chadema iliyokuwa imegomewa ya bilion mbili (inasemekana) kwa mwezi kuanza kutolewa.

Cha ajabu Chadema wamekuwa wanazunguka kila mahali wakipinga serikali kwa kila kitu inachokifanya, wakikashifu, kudhalilisha na hata kuwatutana na kuwatezwa viongozi wakuu wa serikali ikiwamo raisi wa nchi, kuchochea vurugu na uvunjaji wa amani. Wamekuwa wakitishia kwamba watakiwasha hapa ndani na duniani kote kwani waungwa mkono na dunia aka mabeberu wa dunia ie EU, USA etc.

Wamekuwa wakidandia masuala hususani ya maboresho ya katiba ya nhi, mkataba wa bandari zetu na DP World na uboreshaji wa hifadhi ya Ngorongoro na kuyafanya kuwa ndiyo sera yao wakati kuna vyombo halali vinavyo shughulikia mambo haya.

Leo Rais kasema na kutoa maelekezo, sidhani kama hawa chadema wamemuelewa. Watapinga maelekezo haya kama kawaida yao. Ikumbukwe kwa mila zetu, tamaduni zetu na sheria zetu, maelekezo ya mkuu wa nchi ni maagizo na ni amri. Hawa jamaa watayapinga na kumteza aliyeyatoa. Ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu.
Chawa OP
 
Jiwe alikataa katiba mpya na alipiga marufuku hiyo mikutano ya hadhara na mliufyata.


Wewe unaona kutawaliwa na Moshi au Mwanza au Bagamoyo ni sawa?





Sera za vyama vya siasa, sheria za nchi, tekinolojia na hata imani na mahubiri ya dini mbali mbali hazijaweza na hazitaweza kukomesha wizi wa aina yo yote tangia mwanzo wa dunia. Katika bustani ya Adeni, ibilisi alimshawishi Eva kuiba lile tunda la Mungu na alifanya hivyo, akaliiba, akakamatwa na kuadhibiwa yeye na Adamu wake. Tangia hapo wizi unaendelea kwa ushawishi wa ibilisi, wanaokamatwa huadhibiwa, wengi hawakamatwi na dini zinahubiri adhabu yao wataikuta huko ahera watakapoenda.



Nimekudokeza tu mfano rahisi wa mbinu moja wapo inayoweza kutumiwa kama chadema hawaweki mawakala thabiti wa kusimamia upigaji kura na uhesabu kura kwenye hivyo vituo. Mbinu ziko nyingi tu duniani za kuibiwa kura ukizembea. Huo ni mfano tu (abstract) wa great thinker, usiuchukulie kama ni wa ukweli na kwamba mimi ndiyo shahidi. Kwanza mimi si mwanachama wa chama cho chote cha kisiasa.

Ulisikia na kuona huko Kenya kwenye chaguzi zao walivyolalamika kura zao kuibiwa juu kwa juu kwa njia ya kidijitari za mtandao wakati wa transmission za data kwenda National Election Commission. Walifikishana hadi Mahakama ya juu lakini ikawa ngumu kuthibitisha wizi huo wa mtandao beyond reasonable doubt.

Bila shaka ulisikia huko USA wakilalamika jinsi Russia ilivyobadili electronically kura za Mama Clinton na kumwezesha rafiki yao Trump kuwa rais wa USA.

Leo umemsikia mwanaharakati wa kimataifa, Bw. Tundu Lissu alivyotorokea USA/ Belgium kutokea Ngorongoro hadi Nairobi International Airport baada ya alichotumwa kufanya huko Ngorongoro Crater na Tanzania kwa ujumula kusitishwa na jeshi la Wambura. Ameenda kutoa ripoti ya kile alichoweza kukikusanya hapa Tanzania. Huyu mtu nyie mnamuita ni mwanasiasa. Wenye akili wanamuita ni mwanaharakati na jasusi wa nchi za ulaya na Amerika. Ni kibaraka wa hao wazungu wanaotaka kumsimika awe raisi wa Tanzania kwa masilahi yao.


Hapa unafanya siasa nyepesi.

Maswali haujibu unabaki kuuzunguka mbuyu.

Jitahidi kusimamia hoja unapoileta mezani.



Kuhusu Lissu kuwa kibaraka wa wazungu, Serikali ya Tanzania iliyopo madarakani sasa ni kibaraka wa nani?

Kuna nchi na kiongozi Afrika hii ambae sio kibaraka wa nchi za Magharibi? Yupi?



Nakuuliza tena, ina maana msajili wa vyama vya siasa hajui tofauti ya wanasiasa na wanaharakati?

Mbona hata Onyo hajawapa hao CHADEMA kuacha harakati wafanye Siasa kwa mujibu wa sheria na miongozo ya vyama vya Siasa?
 
Back
Top Bottom