Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Lazima uwe taahiri kuchagua kuwa kama CUF ya Lipumba au ACT ya Zito. CCM wangependa sana vyama vyote viwe hovyo kama ulivyovutaja ili wavitumia kadiri wanavyotaka.Pole sana ndugu yangu, kumbe hujui tofauti ya vyama vya siasa na vikundi au vyama vya wanaharakati (activists). Goja nijaribu kukuelewesha:
Vyama vya siasa hufanya kazi kwa utaratibu niliouelezea hapo juu kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi pamoja na mila, desturi na maadili ya wananchi.
Kama likitokea jambo linaloelekea kutokuwa na masilahi ya taifa, hususani hili la mkataba wa IGA; chama hufanya kwanza utafiti wa kina wa kisayansi wakitumia watalaamu wao mahili. Baada ya hapo vikao vya chama (CC na NEC) hukaa kuchambua kwa makini utafiti huo na kutoa tamko la chama lililosheheni weledi mkubwa kuhusu jambo hilo pamoja na maoni na mapendekezo ya utatuzi wake. Vyama vya siasa huwa havikurupuki. Upinzani wa kisiasa siyo sawa na mchezo wa ngumi wa kurushiana makonde. Upinzani wa kisiasa ni wa kushindanisha nguvu za hoja na siyo hoja za nguvu.
Vikundi ama vyama vya wanaharakati havina sheria wala kanuni na taratibu za kufanya kazi yao. Wao hufanya kazi kwa matukio. Havifanyi utafiti. Wao wakisikia jambo lo lote lililofanywa au kukusudiwa kufanywa na serikali, hulirukia na kuishambulia serikali kwa nguvu kubwa bila hata uthibitisho wa kile walichokisikia. Huropoka maneno makali na mabaya kwa serikali na kwa viongozi wa serikali yakiwamo matusi na maneno mengine machafu. Hushambulia serikali ndani ya nchi na nje ya nchi na taasisi za kimataifa hususani European Union, World Bank na kadhalika. Lengo ni kuichafua nchi na kuitishia iwekewe vikwazo vya kimataifa kwa kile serikali ilichofanya. Wanaharakati hawatambui kwamba nchi yetu ni sovereign state yenye uhuru wa kuendesha mambo yake. Hawa wanaharakati hupeleka haraharaka mambo yetu BBC na Al Jazera na kadhalika. Wanaamini Tanzania inatawaliwa na mabeberu wa Ubiligiji, Ujerumani, USA na EU.
Chama cha chadema kiko kundi hili la wanaharakati. Hakina tofauti yo yote na vikundi vingine vya wanaharakati hususani kile cha Sauti ya Watu kinachoendeshwa na Maria Sarungi ambacho Dr Slaa kajiunga. Raisi Salmia kawaelekeza wanachotakiwa kufanya cha siasa. Sidhani kama wamemuelewa. Maamuzi ni ya kwao, waendelee kuwa chama cha wanaharakati au wajirekebishe na kurudi kuwa chama cha siasa kama vile chama cha Zitto Kabwe au kile cha Prof. Lipumba. Wakiendelea kuwa wanaharakati wasitegemee kupata ha mbunge mmoja 2025.
Umaweweseka sana Dr Ujinga. Hujajikomboa kifikra na kinafsi. Wanachofsnya CHADEMA ni sahihi kabisa, ndivyo vyama vya siasa kwenye nchi za kidemokrasia vinavyofanya.
Baada ya kashfa ya viongozi wa Serikali, wote kutoka upande mmpja wa Jamhuri, kuhusika katika kuwezesha uporwaji wa bandari za Tanganyika, CHADEMA Baraza Kuu walikaa, na miongoni mwa maazimio ilikuwa ni kuwaeleza wananchi kilichotendeka, na athari yake kwa Taifa na vizazi vijavyo. Na hicho ndicho kinachoendelea. Wewe endelea kuwaeleza wananchi uzuri wa huo mkataba, CHADEMA wataendelea kuwaeleza wananchi juu ya ubaya wa huo mkataba mbaya kabisa kwa Taifa letu.