Ndoa ya kwenye Biblia ni kivuli cha ndoa halisi ya Mungu Na mwanadamu.Yesu alisema huwezi kuwatumikia mabwana wawili, Na akasema mtu huwaza yaujazayo moyo wake.
Ndoa ni kumwamini Kristo , refer Ufunuo 19 Ndoa ya mwanakondoo..
Uzinzi unaoongelewa kwenye Vitabu vya kinabii ni juu ya watu wa Mungu kushirikiana Na shetani.
Yeremia 31:31-32
[31]Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
[32]Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema BWANA.
Kwahiyo ndoa halisi ni kumwamini kristo
Warumi 7:1-6
[1]Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu wakati anapokuwa yu hai?
[2]Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume.
[3]Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine.
[4]Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda.
[5]Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao.
[6]Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko.
Aliyewaunganisha Mungu ,mwanadamu asiwatenganishe
Mathayo 19:4-6
[4]Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
[5]akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
[6]Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
Na hapa ndio inaelezea ndoa isiyotenganishika
1 Wakorintho 6:17
[17]Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
Bikira safi ni wale waliomwamini kristo ,hawa wajashirikiana Na Shetani yani hawajafanya uzinzi Na shetani
2 Wakorintho 11:2
[2]Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
Harusi yatimia
Ufunuo wa Yohana 19:7-8
[7]Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.
[8]Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.
Mke mmoja ilikuwa ni kivuli ,
Wakolosai 2:16-17
[16]Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
[17]mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
Torati ni kivuli tu,sura yenyewe ni Yesu
Waebrania 10:1
[1]Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.
Musa alimwinua nyoka jangwani watu wamtazame ,Na Yesu alipokuja akasema kile ni kivuli ila picha halisi ni yeye atainuliwa msalabani ..
Yohana 3:14-16
[14]Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;
[15]ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.
[16]Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Yesu alipofufuka ndio anasema kuwa manabii wote walisema habari zake yeye , ndoa nayo ilikuwa ni picha ya kuungwa Na Roho kwa njia ya kumwamini kristo
Luka 24:44-45
[44]Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.
[45]Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.
Biblia ni kitabu kinachomhusu Yesu Na ujumbe wake wa ukombozi