Hivi dume Zima unakaaje kwenye nyumba ya kupanga hata chumba kimoja kimekushinda

Unashangaa mtu kuamka na boksa kwenye hiyo nyumba, kwa taarifa yako na wewe ukija hovyo hovyo kwenye hizo nyumba unaweza ukadinywa vilevile.
 
Cha umuhimu hapa duniani ni kupata makazi bora either ya kwako binafsi au ya kulipia
 
Ila mda mwingine ukiwaza, inasikitisha sana Aise... Chumba kimoja unashindwa kujenga kweli?? πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜….
Kaka, kila mtu ana speed yake… usijali, tunajenga maisha yetu kwanza kabla hatujajenga ukuta!
 
Kaka, kila mtu ana speed yake… usijali, tunajenga maisha yetu kwanza kabla hatujajenga ukuta!
Ni kweli mkuu, pambaneni sana ili mjenge, maisha ya kupanda ni changamoto sana.. 🀝🀝🀝
 
Kuna kauwendawazimu flani ka'kifisadi umekapata baada ya kupata mafanikio haramu(jichunguze mwenyewe uhalali wa kipato chako), pia ni mshamba usiye na staha na hujui maisha, sasa kamekulevya umeanza kufuru.

Kuna mtu aliyestaarabika na bila sababu anapendq kuishi kwa mtu?

Kuna watu wana mijengo yao lakini wamepanga kwa sababu kadha wa kadha!

Kuna wafanyakazi wa rika zote wamepanga kutokana na mazingira ya kazi lakini wameacha miji yao na familia zao mbali.

Topic yako ungespecify na kudifferentiate kuelekeza matusi yako kwa watu wenye kipato kizuri lakini wamejisahau kujenga makazi yao na kudekeza starehe za kichwa cha chini na 'ubwao', ungelieleweka.

Kutoa kejeli ya ujumla kwa wapangaji wenye heshima zao ni kumchokoza beya!
 

Huku ndiko kuwashwa washwa sasa.

Wahindi wanakaa nyumba za NHC kwani umewazidi nini?
 
Kama unaamini kujenga nyumba ya kuishi ndiyo kufanikiwa bado uko nyuma sana shekhe
Na wenye ndoto ya kujenga wakiamini ndiyo kufanikiwa huishi kwa tabu sana hutumia nguvu nyingi sana kufanikisha hilo jambo
Miaka mitano mtu anajenga ukimpiga mahesabu unakuta amezika milioni hamsini, sitini
Ingekuwa unawekeza sehemu kidogo kidogo kwa hiyo miaka mitano ungekuwa na uwezo wa kujenga nyumba zaidi ya hizo tena za uhakika na uhakika wa biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…