Hivi haiwezekani viongozi wakashughulika na kero bila microphone?

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
25,522
Reaction score
40,795
Kwa Sasa Tanzania imekuwa ni fashion kwamba ili Kiongozi aonekane anafanya kazi vizuri, ni lazima atumie microphone anapotembelea au kukagua miradi ya serikali. Na mara nyingi kwenye hizo microphone Kuna maspeaker ya kuwafanya wananchi wasikie Kiongozi anaongea nini. Mara nyingi wananchi hushangilia sana Kiongozi anapofoka na kukaripia wahusika wa miradi au viongozi wa serikali eneo husika. Kwa maana nyingine, kwa Tanzania ili uwe Kiongozi mzuri dharilisha sana viongozi walioko chini yako na uwakebehi hadharani au mbele ya video huku Mic ikiwa on na wananchi wanashangilia. Fanya hivyo tu, urais ni wako.

Sikatai kutumia microphone, ila naona ni kama haisaidii kutatua matatizo na kero za wananchi. Hivi Kiongozi akikagua mradi mwenyewe akiongozana na wataalamu na wahusika bila microphone na maspeaker na hata bila kuchukuliwa video kazi haitafanyika?. Na pale anapoona Kuna shida akakaa na wale viongozi kule ofisini na aidha kuwapa maelekezo au kuwaadhibisha kwa mujibu wa Sheria, mambo hayataenda?. Lakini kuwadhihaki na kuwakebehi viongozi wenzako hadharani kwa maneno ya kejeli na dharau sio uongozi mzuri.

Niulize swali Moja tu, tangu hii fashion ya kutumia microphone imeanza kutumika na viongozi, Kuna mabadiliko?. Mambo ni Yale Yale. Ukiindoka ukarudi kesho yake shida ni zilezile , kwa sababu tiba sio kutumia mic ili kushangiliwa na wananchi au kuonekana unafanya kazi, bali shida ni namna ya kuondoa hizo KERO za wananchi kwa mfumo Mmoja . Na sio kusubiria Kiongozi aje mpanda afokee watu halafu aende Tena Mwanza afokee watu nk. Ndipo KERO zitatuliwe.

Suluhisho sio mic bali suluhisho ni viongozi kuumiza kichwa ili kuja na mfumo unao saidia kutatua KERO za wananchi pasipo kutumia mic na kufokea watu. Weka mfumo utakaoweza kutatua KERO za Ardhi kuanzia Namanga Arusha mpaka Tunduma Songwe. Tutengeeze mfumo bora na sio usanii na maigizo ya mic wakati KERO zinabaki palepale.
 
Wanaona aibu kwakua hawajiamini.
 
"mi nataka kutrendi tu,
Mi nataka kutrendiiii!...", G nako.
 
Back
Top Bottom