Hivi hakuna namna Yanga wanaweza kukata rufaa FIFA?

Yanga mmekula kodi yetu. bure bure tu tunaomba mrudi nyumbani kabla hatujaanza kuwadai
 
Hapana; refa ndiye mwamuzi wa mwisho. Muda mfupi kabla mchezo haujaanza nilipata maono kuwa refa atainyima Yanga ushindi wa wazi; ndipo kiherehere kikaanza kunisumbua. Niliandika kwenye post hii hapa:

 
Mkiambiwa angalieni na mechi za nje hamuelewi.

Arsenal alifungwa goli ambalo macho yaliona mpira umetoka var ikasema haujatoka.

Juzi spurs kakataliwa goli ambalo macho yaliona mpira umevuka mstari ila var ikagoma.

Na haina kukata rufaa.
 
Labda ukute Malinzi ndiye anaongoza FIFA
 
Yanga mmekula kodi yetu. bure bure tu tunaomba mrudi nyumbani kabla hatujaanza kuwadai
Hakuna cha kuonewa,Malengo yao yalikua ni makundi kwisha,CAF wanaangalia na malengo yako.
 
Wanajua goal lile limetughalimu kiasi gani watanzania hisia zetu kwa kukosa kusonga mbele kwa kukataa goal la wazi kabisa
 
Hiyo ni kama kwenda kupinga matokeo ya uchaguzi ze hegi 🐼
 
mbona EPL wanapokwa pointi wao wanatumia kanuni ipi au mpira wa Africa unasheria zake? umesahau ile ya simba kuchezesha mchezaji asiye stahiki? bado yanga wakipanga karata vzr wanaweza wakapindua meza kibabe, staki kuamini kuwa VAR inakuwa ARV
 
Inawezekana refa alipewa maelekezo ahakikishe nani anashinda, sioni sababu kwanini refa hakutaka kabisa kuisogelea VAR wakati ilikuwepo, alijua wazi ingemuumbua hivyo kumlazimisha kwenda kinyume na maelekezo aliyopewa na wakubwa zake.

Mourinho aliwahi kuisifia VAR ya Afrika, ila kwa lile tukio la jana naamini hata naye atakuwa hana hamu tena.
 
Watalalamika tu na baada ya malalamiko kuonekana ni sahihi wataadhijiwa VAR officials, kesi inafungwa.
 
Mlikataa msamiati wakufa kiume leo mmeuona,kuvuka robo cafcl sio vyepesi hivyo swine
 
Matokeo ya mpira hata uonewe vipi hayajawahi kubadilishwa na rufaa,kinacho badilishwa na rufaa labda kadi nyekundu. Tuvumilie ndio mpira huo, tuombe Mungu kuwe na goal line technology, ila matokeo ndio yamesha simama na haya badiliki.

VAR yenyewe ya EPL mara kibao waamuzi wanatoa maboko, ila matokeo hubakia vilevile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…