Hivi hakuna njia nyingine ya kupunguza Vitambi/Mafuta mwilini?

Hivi hakuna njia nyingine ya kupunguza Vitambi/Mafuta mwilini?

ngongoti2000

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2017
Posts
2,236
Reaction score
2,142
Wataalam

Nimekuwa nikijiuliza hivi imeshindikana kweli kufanya surgery ya kuondoa mafuta toka kwenye tumbo? Mi naona jinsi yalivyojirundika sehemu moja tumboni kama mnavyotuaminisha kupitia michoro yenu nk ni kazi rahisi zaidi kama imewezekana kuzalisha mwanamke kwa kisu? Badala ya sijui kukata utumbo nk???au kuna kitu sijui hapa wataalam?

Nimehangaika sana kupunguza kitambi changu lakini sasa nimekata tamaa baada ya kubugia madawa mbalimbali ya kienyeji, herbal, food suplements, diet, kuacha kula wanga, mafuta, sukari na nyama nyekundu......Yote haya nimefanya lakini wapi......yaani kuna madawa nikinywa naharisha mafuta mpaka nasikia kizunguzungu...lakini kitambi kinabaki pale pale hata sijui yale mafuta huwa yanapungua kutokeaga wapi.....

Hii ni pamoja na kufanya mazoezi mepesi.......nilichoshindwa kuacha ni pombe kali - Vodka.....lakini nimejitahidi sana kuacha mavyakula ya ajabu ajabu hasa usiku...lakini wapi.......??...

Ttizo kila mtaalam wa mitishamba anakwambia dawa yake ni kiboko lakini wapi! ...nina mwaka wa tano sasa nahangaika na hili tumbo linanyima sana raha wakuu.....

Napokea ushauri wa kitaalam wa aina zote

Asanteni
 
Ukifanikiwa kupunguza chakula cha wanga ikiwemo sukari pamoja na mazoezi utafanikiwa.

Uwe na pesa ya kujihudumia.

Asubuhi chai bila sukari na mayai ya kuchemsha.
Saa nne: salad ya matunda
Saa sita samaki wa kuchoma na mboga za majani
Saa kumi carrots zichemshwe kidogo na hoho
Jioni maharage na mchicha.
 
Yani jioni ule maharage na mchicha? Sasa hapo utakua umekula chakula au mboga?
 
Tumia hii kifaa miezi miwili,asubuhi x10 na jioni x 10,toa J.pili,halafu ulete mrejesho
Screenshot_20211213-183321_Google.jpg
 
Fanya intermittent fasting mtafute YouTube mtu anaitwa Dr. Jason Fung.
 
Wataalam
Nimekuwa nikijiuliza hivi imeshindikana kweli kufanya surgery ya kuondoa mafuta toka kwenye tumbo? mi naona jinsi yalivyojirundika sehemu moja tumboni kama mnavyotuaminisha kupitia michoro yenu nk ni kazi rahisi zaidi kama imewezekana kuzalisha mwanamke kwa kisu? badala ya sijui kukata utumbo nk???au kuna kitu sijui hapa wataalam?
Nimehangaika sana kupunguza kitambi changu lakini sasa nimekata tamaa baada ya kubugia madawa mbalimbali ya kienyeji,herbal,food suplements , diet,kuacha kula wanga,mafuta ,sukari na nyama nyekundu......Yote haya nimefanya lakini wapi......yaani kuna madawa nikinywa naharisha mafuta mpaka nasikia kizunguzungu...lakini kitambi kinabaki pale pale hata sijui yale mafuta huwa yanapungua kutokeaga wapi.....hii ni pamoja na kufanya mazoezi mepesi.......nilichoshindwa kuacha ni pombe kali - Vodka.....lakini nimejitahidi sana kuacha mavyakula ya ajabu ajabu hasa usiku...lakini wapi.......??...Ttizo kila mtaalam wa mitishamba anakwambia dawa yake ni kiboko lakini wapi! ...nina mwaka wa tano sasa nahangaika na hili tumbo linanyima sana raha wakuu.....
Napokea ushauri wa kitaalam wa aina zote
Asanteni
Nenda kwanza hospital ukapime kujua kama hicho kweli ni kitambi, maana kuna tofauti kati ya kitambi na uvimbe, inawezekana una uvimbe kwenye tumbo na si kitambi
 
Ukifanikiwa kupunguza chakula cha wanga ikiwemo sukari pamoja na mazoezi utafanikiwa.

Uwe na pesa ya kujihudumia.

Asubuhi chai bila sukari na mayai ya kuchemsha.
Saa nne: salad ya matunda
Saa sita samaki wa kuchoma na mboga za majani
Saa kumi carrots zichemshwe kidogo na hoho
Jioni maharage na mchicha.
Mtu anataka kupunguza uzito halafu unaleta ushauri wa kula mayai? Are you serious?
 
Wataalam
Nimekuwa nikijiuliza hivi imeshindikana kweli kufanya surgery ya kuondoa mafuta toka kwenye tumbo? mi naona jinsi yalivyojirundika sehemu moja tumboni kama mnavyotuaminisha kupitia michoro yenu nk ni kazi rahisi zaidi kama imewezekana kuzalisha mwanamke kwa kisu? badala ya sijui kukata utumbo nk???au kuna kitu sijui hapa wataalam?
Nimehangaika sana kupunguza kitambi changu lakini sasa nimekata tamaa baada ya kubugia madawa mbalimbali ya kienyeji,herbal,food suplements , diet,kuacha kula wanga,mafuta ,sukari na nyama nyekundu......Yote haya nimefanya lakini wapi......yaani kuna madawa nikinywa naharisha mafuta mpaka nasikia kizunguzungu...lakini kitambi kinabaki pale pale hata sijui yale mafuta huwa yanapungua kutokeaga wapi.....hii ni pamoja na kufanya mazoezi mepesi.......nilichoshindwa kuacha ni pombe kali - Vodka.....lakini nimejitahidi sana kuacha mavyakula ya ajabu ajabu hasa usiku...lakini wapi.......??...Ttizo kila mtaalam wa mitishamba anakwambia dawa yake ni kiboko lakini wapi! ...nina mwaka wa tano sasa nahangaika na hili tumbo linanyima sana raha wakuu.....
Napokea ushauri wa kitaalam wa aina zote
Asanteni

piga tizi mkuu izo mitishamba sina hamu nazo kuna moja unakimbuza mwenge na kutapika znaweza ondoa baadhi ya organ uko tumboni sio kwa fujo zile.
 
Kwanza elewa kwamba mafuta yanahifadhiwa wapi mwilini kwako ni Genetics ndo maana wengine wanavimba vitambi wengine mapaja wengine mikono etc.

Pili idea ya "spot reduction" ni myth yaani ni uwongo ambao wengi wanaamini, hauwezi kupunguza mafuta ya tumbo kwa kufanya situps, hauwezi kupunguza mafuta ya mikono kwa kufanya mazoezi ya mikono etc.

Mafuuta yatapungua wapi ni genetics tena, unaweza ukapungua mafuta lakini ya tumbo yakabaki au yakawa ya mwisho kuondoka, na ukianza kunenepa tena yanaweza kuanza kurudi tumboni hauna control ya hili.

Achana na short term hacks na solutions, hauwezi kutumia dama za diet kwa mda mrefu, nyingi ndo kama ulivyoona zinakufanya uharishe, sidhani kama unaweza kuharisha zaidi ya wiki kabla haujagive up. Zengine zinaufanya moyo uende kasi, madhara yake ni makubwa baada ya mda.

Elewa kwamba itachukua muda mrefu.
Diet ndo key kubwa bila kubadili diet hakuna mazoezi yanayoweza kukuokoa, kwa kuanza achana na vitu vilivyoongezwa sukari, kama unakula chochote ambacho ni packaged food, angalia igridients zake, kama kuna sugar/honey/corn syrup achana nacho, ogopa vinywaji soda, juice, maziwa vina sukari nyingi sana, juice sio healthy kama waatu wanavyofikiri. Achana na bia, kama unahitaji pombe pombe kali ni bora zaidi kwa upande wa unene.

Kuwa active anglau kidogo, sio lazima ukimbie ila ni muhimu angalau kutembea KM kadhaa kwa wiki.

Mwisho inua vyuma, watu wengi hasa akina dada wanaogopa vyuma wanafikiri watavimba mwili kama bodybiuilder, usiogope kuvimba mwili kunahitaji madawa ya steroids hasa akina dada ni impossible kuvimba bila madawa.

Utakapoinua vyuma utajenga misuli, misuli ni mizito "dense" kuliko mafuta so kg zako zinaweza kuongezeka ila usioope hilo, bodyfat % yako itashuka na mwili wako utakuwa na mwonekano mzuri zaidi, misuli pia inachoma energy zaidi, yaani mtu mwenye misuli anachoma energy hata akiwa amelala hii tene itakusaidia kupunguza mafuta.
Hakikisha unaongeza uzito wa vyuma unavyotumia kila mwili unapoanza kuvizoea, GYM sio lazima unaweza kununua vya kwako au kutumia zile rubber band za mazoezi ili mradi ujenge misuli.

muscle.jpg
 
Hizo njia zote ulizotaja wewe unazifanya kama Temporary, yani unataka Temporary solution inashindwa kufanya kazi unabakia na permanent problem

Badili mfumo wako wa maisha ,
Anza na diet (acha kula vyakula vya wanga kabisa)
Kula protein , healthy fat, matunda yani vitamins ..na n.k

Usishinde njaa kula ushobe lakini usile wanga wala carbonated drinks soda , na beer ukinywa unafanya sukari ya mwili inayotokana na wanga kuchelewa kunyonywa ..

yani ni matataizo ya insulin kuwa nyingi inapelekea sukari kuzalishwa kwa wingi na sukari unaongezeka uzito maana itakuwa vigumu ku burn calories/kuchoma mafuta ya mwilini kwako ..

Fanya mazoezi ya viungo mwli mzima atlist 40dk na mara3 /week ruka kamba kimbia , push ups squats

Ukianza hiyo life style umemaliza tatizo jipange sasa usisubiri hadi uumwe kisukari ndio ujali afya yako
 
Back
Top Bottom