wa kupuliza
JF-Expert Member
- Jun 15, 2012
- 15,216
- 37,757
Mayai ya kuchemsha Yana shida gani ukiachana na Ile shida ya kutengeneza kiwanda Cha vijambo?Mtu anataka kupunguza uzito halafu unaleta ushauri wa kula mayai? Are you serious?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mayai ya kuchemsha Yana shida gani ukiachana na Ile shida ya kutengeneza kiwanda Cha vijambo?Mtu anataka kupunguza uzito halafu unaleta ushauri wa kula mayai? Are you serious?
Mwingine aliharisha mpk pulu akawa anairudishia kwa kidole tu.piga tizi mkuu izo mitishamba sina hamu nazo kuna moja unakimbuza mwenge na kutapika znaweza ondoa baadhi ya organ uko tumboni sio kwa fujo zile.
Mnoo, Huwa nahisi sekunde zimesimama😂hii exersise inauma balaa
Ukifanikiwa kupunguza chakula cha wanga ikiwemo sukari pamoja na mazoezi utafanikiwa.
Uwe na pesa ya kujihudumia.
Asubuhi chai bila sukari na mayai ya kuchemsha.
Saa nne: salad ya matunda
Saa sita samaki wa kuchoma na mboga za majani
Saa kumi carrots zichemshwe kidogo na hoho
Jioni maharage na mchicha.
Wengi wenye vitambi Ni walafi mno.Basilisha eating style yako ndio mchawi mkubwa, bila kusahau fasting husaidia na mazoezi, pia punguza kunywa soda ni hatari sana
Mkuu unataka waanze kusema kaukwaaTafta MCHEPUKO,
Kakope mkopo wa benki kisha mkabidhi afanye ujasiliamali.
Mwezi TU,
Kitambi kimeisha
Mawazo na stress zinapunguza mwili kwa Kasi ya kimondo.Mkuu unataka waanze kusema kaukwaa
Wataalam
Nimekuwa nikijiuliza hivi imeshindikana kweli kufanya surgery ya kuondoa mafuta toka kwenye tumbo? mi naona jinsi yalivyojirundika sehemu moja tumboni kama mnavyotuaminisha kupitia michoro yenu nk ni kazi rahisi zaidi kama imewezekana kuzalisha mwanamke kwa kisu? badala ya sijui kukata utumbo nk???au kuna kitu sijui hapa wataalam?
Nimehangaika sana kupunguza kitambi changu lakini sasa nimekata tamaa baada ya kubugia madawa mbalimbali ya kienyeji,herbal,food suplements , diet,kuacha kula wanga,mafuta ,sukari na nyama nyekundu......Yote haya nimefanya lakini wapi......yaani kuna madawa nikinywa naharisha mafuta mpaka nasikia kizunguzungu...lakini kitambi kinabaki pale pale hata sijui yale mafuta huwa yanapungua kutokeaga wapi.....hii ni pamoja na kufanya mazoezi mepesi.......nilichoshindwa kuacha ni pombe kali - Vodka.....lakini nimejitahidi sana kuacha mavyakula ya ajabu ajabu hasa usiku...lakini wapi.......??...Ttizo kila mtaalam wa mitishamba anakwambia dawa yake ni kiboko lakini wapi! ...nina mwaka wa tano sasa nahangaika na hili tumbo linanyima sana raha wakuu.....
Napokea ushauri wa kitaalam wa aina zote
Asanteni
Yani jioni ule maharage na mchicha? Sasa hapo utakua umekula chakula au mboga?
atahimili maumivu?
Wengi wenye vitambi Ni walafi mno.
Asilimia kubwa Ni wapenzi wa kula viporo.
Kiporo hakijawahi muacha mtu salama.
Chunguza hata watoto wadogo wa vijijini wanafakamia viporo,
Wanavitambi utadhani watu wazima.
Kuna dada alikua anampikia mumewake mbaazi au maharage shata shata anywee chai tena akisindiza na chapati au mihogo. Alisema yeye amefundwa kuhusu kumtunza mume.Kama unajua hesabu vizuri 1+1 = 2 n.k fanya mazoezi unayoyajua wewe, kula madawa yote ujuayo ila ukishindwa kuwa na utaratibu wa kula KITAMBI hakiishi unapunguza kila moja unaongeza moja au zaidi , Na jamaa zangu wanakimbia 5-10km kwa wiki mara 3 mpaka 4 tatizo ni moja - BIA unakimbia 10km asubuhi unapunzika jioni unakunywa bia 5 na nyama ! Hakuna ulichofanya. Simple, acha kula vya kula vya wanga jioni, kula mchana uwezavyo jioni matunda , mbogamboga au piga deshi kabiisa. Ni ngumu sana hasa ukiwa na wife anaepiga haswa [emoji23][emoji23] unaweza shindwa vumilia kama mimi ila nakomaaa napungua kidogo na kula tena [emoji23] pia ukiwa na uwezo kidogo kuwa na kale ka six park mashine kanauzwa kama 250k hv tosha kabisaa.
honawezaje kuondoa hii mkuu?Insulin resistance....Ondoa kwanza huu ugonjwa...vinginevyo utatwanga maji kwenye kinu