Hivi hakuna njia nyingine ya kupunguza Vitambi/Mafuta mwilini?


Kama unajua hesabu vizuri 1+1 = 2 n.k fanya mazoezi unayoyajua wewe, kula madawa yote ujuayo ila ukishindwa kuwa na utaratibu wa kula KITAMBI hakiishi unapunguza kila moja unaongeza moja au zaidi , Na jamaa zangu wanakimbia 5-10km kwa wiki mara 3 mpaka 4 tatizo ni moja - BIA unakimbia 10km asubuhi unapunzika jioni unakunywa bia 5 na nyama ! Hakuna ulichofanya. Simple, acha kula vya kula vya wanga jioni, kula mchana uwezavyo jioni matunda , mbogamboga au piga deshi kabiisa. Ni ngumu sana hasa ukiwa na wife anaepiga haswa [emoji23][emoji23] unaweza shindwa vumilia kama mimi ila nakomaaa napungua kidogo na kula tena [emoji23] pia ukiwa na uwezo kidogo kuwa na kale ka six park mashine kanauzwa kama 250k hv tosha kabisaa.
 
Tafta MCHEPUKO,
Kakope mkopo wa benki kisha mkabidhi afanye ujasiliamali.


Mwezi TU,
Kitambi kimeisha
 
Basilisha eating style yako ndio mchawi mkubwa, bila kusahau fasting husaidia na mazoezi, pia punguza kunywa soda ni hatari sana
Wengi wenye vitambi Ni walafi mno.
Asilimia kubwa Ni wapenzi wa kula viporo.

Kiporo hakijawahi muacha mtu salama.

Chunguza hata watoto wadogo wa vijijini wanafakamia viporo,
Wanavitambi utadhani watu wazima.
 
Mkuu unataka waanze kusema kaukwaa
Mawazo na stress zinapunguza mwili kwa Kasi ya kimondo.

Mtoa mada anaonekana Ni mtu alierelax sana, Hana purukushan kabisa.

Analala usngizi unakuja, anakula chakula kinashuka, Hana madeni, n.k
 

lifestyle.
 
Mi mwili wangu sijui Kama nitakuja kunenepa wala kua na kitambi.

Maana mi mfumo wangu wa maisha Ni mazoezi tosha.

Kuna MDA nakua bize sana nasahau mpaka kula
(najitahid sana Nile nishibe asbuh, Mara nyingi mchana najikuta nmesahau kula)

Nawaza Sana kukimbizana na malengo ya kiuchumi niliyojiwekea,
Nalala nimechelewa Sana,
Naamka mapema Sana,
Sili viporo asubuh,
Nipendi kula sembe na ubwabwa,
Nilishaacha kunywa bia,
Nilishaacha kunywa soda,
Nafanya Sana mapenzi,
Nakunywa maji mengi,
 
Yani jioni ule maharage na mchicha? Sasa hapo utakua umekula chakula au mboga?

usishangae ndugu yangu, hawa hawashindwi….mwingine anakula hayo majani tu na analala [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Bervy haujambo! [emoji1609][emoji1493][emoji1493][emoji16][emoji16]
 
Punguza kula sana. Hasa wanga. Anza kupunguza kwa kula nusu sahani ya wali. Punguza bia bia. Fanya mazoezi ya kukutoa jasho. Anza hata nusu saa kwa siku,utajiongeza muda baadae.

NB:- mazoezi yanahitajj moyo wa kujituma sana. Sio kitu chepesi. Ndio maana tunawasisitiza mapema kujibalance mapema kabla ya kitambi. Kupata kitambi ni ndani ya muda mfupi. Lakini kukitoa kitambi cha mwezi,itakuchukua aka 3
 
Umeshindwa acha pombe kali basi punguza.
Maana 200mls ya pombe kali zina ~ apro value of 400 calories kwenda juu na kuunguza hizo calories za 200mls tu za vodka yakupasa kukimbia jogging au kutembea kwa haraka more than 6kms.
Hii na hisi ndio kikwazo kwako na hiyo Pombe kali lazima utakua unashushia na nyama choma tuu kwa hiyo ni calories juu ya calories.
 
Kuna dada alikua anampikia mumewake mbaazi au maharage shata shata anywee chai tena akisindiza na chapati au mihogo. Alisema yeye amefundwa kuhusu kumtunza mume.

Ni mpaka mume alipokutwa na high level of cholesterol kwenye damu ndipo akili ilimuingia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…