Hivi hamsomi mazingira? No way tutamuona akiwa live tena!

Mkuu wewe unachanganya mambo. Kuna watu wanataka raisi afe/auwawe au wanachotaka watu ni kufanya revolution ya kuitoa serikali madarakani alafu uchaguzi urudiwe kukiwa na tume huru?
Hayo maandamano watu wanayotaka lengo lake raisi auwawe? Nafikiri umewaza nje ya mstari
 
Wakimalizana lazima watufuate humu, na majina yetu bandia

Sisemi ni TISS . Ila Pengine labda TISS wenye dhamana ya kuteka wana tabia moja ambayo haibadiliki.
(Ila kuteka sio kazi ya TISS)

Wanateka yule ambae wameambiwa wamteke. Na ni yule ambaye either anamuandama mmoja wa Viongozi na kusema siri zake...

Na mbaya zaid ukapatia jambo ambalo walifanya siri na kuliweka wazi. Watakutafuta.

Na watakutafuta kwa lengo MOJA KUU. Ni ili wajue nani alikuambia ili wajue nani kavujisha siri yao n wamshugulikie.
Au pengine una ushahidi wa kitu ambacho wao hawahitaj ushahidi.

Polepole lazima ameshabanwa sana na kashawataja wale wote ambao wako na yeye. Na hilo ni kazi ya wana usalama wa nchi.

Otherwise ukisema ya kusema huku JF ambayo hayana ushahidi.

Hawakutafuti na hawakugusi maana wanajua ni kawaida raia kuongea. Ni haki yako.
 
Mdude au Chaula walikuwa na jipya gani mkuu? Chaula imemsababisha picha tu, kweli picha ndio upanic hadi kumtoa mtu uhai?

Hapa tunasakwa kitambo siku melo akiingia kwenye kumi na nane zao, humu tutapoteana maana wao wanataka kusifiwa tu
 

mkuu nahisi wewe ndie unaechanganya, soma maelezo ya mleta mada wa wanchangiaji waliowengi. wameshakubali kuwa CCM watafanya uchaguzi na serikali wataunda, sasahivi wanacho wish ni kuuliwa kwa raisi.
 
Tukinyamaza inawezekana hata kwa muda mfupi kukamilisha unayosema... Tatizo maneno yetu mengi ndio yanampa shetani nguvu kwa kuchambua na kujiimarisha.

Tupunguze mdomo sababu midomo yetu inawawia vigumu wazalendo kukomboa taifa
 
mkuu nahisi wewe ndie unaechanganya, soma maelezo ya mleta mada wa wanchangiaji waliowengi. wameshakubali kuwa CCM watafanya uchaguzi na serikali wataunda, sasahivi wanacho wish ni kuuliwa kwa raisi.
Nimepitia tena comments zote mbona sioni hao watu wakisema afe/auwawe?
 
Mdude au Chaula walikuwa na jipya gani mkuu? Chaula imemsababisha picha tu, kweli picha ndio upanic hadi kumtoa mtu uhai?

Hapa tunasakwa kitambo siku melo akiingia kwenye kumi na nane zao, humu tutapoteana maana wao wanataka kusifiwa tu

Ya Mdude ni makubwa sana.
Haya ndio yawe mfano.

Alikuwa ana tukana na kuongelea vibaya kwa Viongozi wa ngazi zote.
Kuanzia Wilayan Had kwa Raisi.
Amepotezwa na huwez jua amri imetoka kwa nani.

Kumbuka Sativa alivyokamatwa aliulizwa "umemuudhi kiongoz gan? Na wale waliomkamta.
Na baadae alivyofatwa na Mafwele pale osterbay karakana na Mafwele kukonfirm kuwa ni Sativa . Na Mafwele akaaondoka. Wale majamaa waliomkamata wakamwambia "itakuwa umemkosea mtu mkubwa sana. Maana mpaka boss amekuja " .

Ila sasa wale waliomchukua asubuh swali likawa lingine.

Hii inaonyesha kuwa hoja yao ni kuchunguza ni nani anawasaliti ili wamuwekee vikwazo.
 
Nimepitia tena comments zote mbona sioni hao watu wakisema afe/auwawe?

 

View: https://m.youtube.com/watch?v=GiAs8sxU8uk
☝️Hizi ndio nyimbo wanazopiga vijana wa ‘generation z’ huko kwenye social media huku wakiweka picha ya Polepole.

Soma comments sasa, aisee hawa watoto wako tayari kwa lolote.

Time will tell

Waende wenyewe instagram tafuta yeyote anaejiita captain Tesha; maana kuna account zaidi ya 200 waone wanayo post hao watoto.


View: https://m.youtube.com/watch?v=BtuwbQun3Dw&pp=ygUOTW9zZXMgWmFtd2FuZ2HSBwkJ_AkBhyohjO8%3D
Ukienda huko mwendo wa ‘patriotic songs’ zikiambatana na picha ya Polepole, chozi linaweza kukutoka ukifuatilia sana wanayo posts.

Kuna watoto wanaweza propaganda za ki-demagogue, askofu Gwajima aoni ndani.
 
Dah,

Umenikumbusha Saanane. A bright young fellow nilikuwa nabadilishana naye mawazo anaenda next level ambayo wachache walikuwa wanaenda.
 
Mkuu unasema ukikosoa huku jf hawakutafuti? Ugumu ni jinsi ya kupata hao watu lakini sio kuwa hawaangaiki kutafuta

Huko kwingine tik tok na ista kila leo wanatekwa. Twitter kuna dogo anaitwa Kiduku nae kachukuliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…