Mfano 1
Kuna rafiki yangu alikuwa ameoa ana mtoto mmoja naye. Wakipishana kidogo, mwanamke hapiki chakula, anahama chumba, hafui nguo wala hafanyi usafi wowote na hawasemeshani hadi nyinyi marafiki zake mnanuniwa. Kupishana kupo ila mambo yote huwa yanaendelea kama kawaida hadi unyumba unapewa na story zinapigwa kama kawaida. Kama wewe mwanaume unaweza kuendelea na hii ndoa?
Mfano 2.
Kuna wanawake wanapenda kukutawala na kukufanya kuwa hauna maamuzi kwasababu ya hela zake, dini yake au mila zake. Hapo utasema mwanaume tafuta hela ili mkeo asikuzidi. Ndiyo jambo jema, kukiwa kuna ushindani ndani ya ndoa yaani mmoja wenu kwakuwa ana hela basi ampelekeshe mwenzake kwa kuwa hana basi hiyo siyo ndoa kwasababu ndoa ni upendo, kuvumiliana na kuheshimiana wala siyo kuwa na ushindani miongoni mwenu kwasababu nyie ni mwili mmoja (maendelo ni ya kwenu nyote) Kila mtu ana ridhiki yake kwahiyo huwezi kushindana au kumdhuia mwenza wako asikudhidi kipato ndiyo akuheshimu. Kama kipato chake ndiyo kinamfanya hakudharau, mwache aishi na kipato chake maana kipato chake ndiyo mume wake.