Hivi hawa wanaokula kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan na Kwaresma ni hawana dini au ndo wanajiendekeza?

suala la kufunga ni la kiimani na sio maonyesho ni wewe na Muumba wako.
 
Quaresma Ni upagani haupo katika Maandiko
 
Hatujiendekezi ila wengine tunanyonyesha na ndio umetuona tunakula na kumimina juice. [emoji848][emoji848]
 
KUFUNGA SIO UTAKATIFU AU USAFI. KUNA WATU WAKIFUNGUA WANAFANYA MAMBO ZA AJABU KULIKO HATA SHETANI. KIPINDI HIKI HATA SHOGA KAFUNGA, AKIFUNGUA ANAENDELEA NA YAKE
 
Funga pekee haiwezi kumpeleka mtu peponi. Kuiona Pepo ni mjumuisho wa mambo mengi sana ya kiroho.

Kwanza wanaofunga katika roho na kweli ni wachache sana, wengi wanaigiza (wanashinda njaa tu).

Wapo wanaofunga ili wasionekana wanakinzana na watu wengine wa imani yao. Kwahiyo usipokula au kunywa tena kwa siku 40 tu (kwa Wakristo) au siku 30 tu (kwa Waislamu) haimaanishi ndiyo umemaliza kila kitu.
 
Kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan ni nguzo ya 4 ktk uislam ,Na Amesema Bwana Mtume amani Iwe juu yake kwamba Mwenye kufunga ktk Njia ya MwenEnzi Mungu basi MwenyEnzi Mungu humuweka mtu huyo (Muumini/Muislam) mbali na Moto wa Jehanam kwa umbali wa miaka 70 Pia faida ya wafungaji Siku ya hukumu/kusimama hesabu/Kiama wataingia ktk mlango maalum unaoitwa Rayyan kuingia ktk Pepo ya MwenyEnzi Mungu ni hayo tu machache kiimani/kinafsi ktk kupandisha watu ktk Darja ya UchaMungu lkn pia kuna Faida nyingi kiafya anazopata mfungaji kama kuchoma /kupunguza mafuta mwilini na kumpumzisha tumbo kwa umeng'enyaji/usagaji wa chakula .
 
Acha unafiki !! Kama kweli mnafunga, sasa iweje bajeti ya chakula iwe kubwa kupita kipindi ambacho hamjafunga ??! Mfano kabla ya mfungo unatumia 200,000/= ya chakula kwa mwezi, halafu ukifunga unatumia 500,000/= kwa mwezi badala ya kushuka hadi 20,000/= au 15,000/= kwa mwezi ??!
 
Wanaokula mchana niwakinanani,kwamana mazehebu yote,yapo kwenye mfungo
 
Inakuhusu Nini ?
🀣🀣🀣
 
Kushabu uliovuta leo? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Kule umeacha swali bila majibu
 
Wanaokula mchana niwakinanani,kwamana mazehebu yote,yapo kwenye mfungo
Wana vidonda vya tumbo, wengne waumini wa Nabii Tito wengine Rastaman... hawana rasta ila ni ma airee
 
Sabato hatuitambui hii Kwaresma wala pasaka ya tar 30, ni mchongo flan mwaisa
 
Aliyekuambia kuwa madhehebu yote yanafunga nani? Acha kukariri kijana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…