Hivi hawa watu wa ile pesa tuma kwenye namba hii wanashughulikiwa kweli na mamlaka?

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Bado napata meseji zao. Sielewi hizi namba wanazotumia kama zimesajiliwa kwa NIDA na alama za vidole wanapata wapi ujasiri wa kutapeli watu maana kuwakamata ni jambo rahisi. Mamlaka husika nataka jibu vinginevyo kazi imewashinda.
 
TCRA na kitengo cha cyber wanatia aibu, haiwezekani mgundue namna ya kutulipisha kodi kwa luku ila majizi hayashikwi! Ukipoteza simu same case, kama haina docs za muhimu bora uiache tu mana utatumia gharama za kununua simu ingne
 
Mlitoa namba tuwe tuawaripoti huko lakini nimewaripoti sana sioni mabasiliko yoyote sasa nikipata hizi message huwa nazifuta tu
 
Bado napata meseji zao. Sielewi hizi namba wanazotumia kama zimesajiliwa kwa NIDA na alama za vidole wanapata wapi ujasiri wa kutapeli watu maana kuwakamata ni jambo rahisi. Mamlaka husika nataka jibu vinginevyo kazi imewashinda.
Nasumbuliwa na hawa majizi Kila baada ya siku mbili na natoa taarifa ila sijasikisa hata mmoja kakamatwa😡
 
TCRA na kitengo cha cyber wanatia aibu, haiwezekani mgundue namna ya kutulipisha kodi kwa luku ila majizi hayashikwi! Ukipoteza simu same case, kama haina docs za muhimu bora uiache tu mana utatumia gharama za kununua simu ingne
Kwenye kupoteza simu sahau kuipata. Nimesharipoti simu zaidi ya tatu hakuna hata moja ilipatikana. Unasubmit loss report unasubiri weekend ukiuliza unaambiwa labda simu ilichinjwa wakachukua spare parts kwa hiyo hatuwezi kui-trace!
 
Hukutembeza fungu mkuu amini, ukihonga wanaipata wiki hiyo hiyo au wanaku refer pa kuipata kuna watu private wanatoa huduma hyo kwa gharama lakn eti kulingana na thaman ya simu
 
TCRA na kitengo cha cyber wanatia aibu, haiwezekani mgundue namna ya kutulipisha kodi kwa luku ila majizi hayashikwi! Ukipoteza simu same case, kama haina docs za muhimu bora uiache tu mana utatumia gharama za kununua simu ingne

Kuna walo wako mitandaoni(Istagram na Fb)
Ambao wanamatangazo yao kuwa wao ni MO foundation(wanatoa mikopo)

Ukifatilizia process zao wanakupa hadi namba ya simu zao za kutuma hela ya makato (ambayo ndo utatapeliwa sasa)

Sasa hadi wanafanya ujinga huu hivi kweli mamnaka za kuhangaikia hawa watu hakuna?
Yaan wanatapeli kwa uhuru kabisa.
Watu wanavifaa vyakujua mnara wa mtumiaji hii laini yuko wapi ila daah nchi za Africa bana

Na hao wa Tuma kwa namba hii asilimia 90 ni mtandao wao wa serikali TTCL..
 
Nasumbuliwa na hawa majizi Kila baada ya siku mbili na natoa taarifa ila sijasikisa hata mmoja kakamatwa😡
Watuambie wanafanya kazi suyo kula mishahara kwa kodi zetu halafu sisi tunaumizwa na wezi. Kama wameshindwa watafute hata contract na kampuni za cyber security za nje. Mtu unaibiwa simu kwa mfano na simu ina IMEI lakini simu inashindwa kupatikana. This is no way to go!
 
Bado napata meseji zao. Sielewi hizi namba wanazotumia kama zimesajiliwa kwa NIDA na alama za vidole wanapata wapi ujasiri wa kutapeli watu maana kuwakamata ni jambo rahisi. Mamlaka husika nataka jibu vinginevyo kazi imewashinda.
Nashangaa watu wapo TCRA wanatunisha vitambi wameshindwa kabisa kuoambana na huu utapeli
 
Hukutembeza fungu mkuu amini, ukihonga wanaipata wiki hiyo hiyo au wanaku refer pa kuipata kuna watu private wanatoa huduma hyo kwa gharama lakn eti kulingana na thaman ya simu
Kumbe ni mpaka nitembeze fungu🤔 Mama yetu Samia na mawaziri wako mnasikia hayo madudu?? Mkuu hebu nipe contact za hao watu private nicheki nao. Please dm me
 
Hii nchi hakuna kitengo kinachofanya kazi yake kwa usahihi, uaminifu na uadilifu. Kila sehemu ni janja janja tu...
Mdogo wangu alipoteza iphone yake, tulifanikiwa kuipata baada ya miezi 2 lakini ilikula karibu laki 2. Polisi wanapenda rushwa sana ndio wafanye kazi, bila hivyo hakuna msaada utapata...
 
Mtandao unaotumiwa sana na matapeli ni Airtel mitandao mingine siyo sana nadhani kuna maboresho wamefanya ila Airtel bado wanatapeliwa sana
 
Kuna walo wako mitandaoni(Istagram na Fb)
Ambao wanamatangazo yao kuwa wao ni MO foundation(wanatoa mikopo)

Ukifatilizia process zao wanakupa hadi namba ya simu zao za kutuma hela ya makato (ambayo ndo utatapeliwa sasa)

Sasa hadi wanafanya ujinga huu hivi kweli mamnala za kuhangaikia hawa watu

Na hao wa Tuma kwa namba hii asilimia 90 ni mtandao wao wa serikali TTCL..
Nina mashaka kama huu utaratibu wa usajili wa line za simu umesaidia lolote kweye KYC (Know your customer). It seems kuna loophole mahali
 
Tapeli anafanya utapeli,namba yake imesajiliwa chini ya kampuni husika ya simu na kampuni inajua kabisa kuwa hiyo namba ni ya tapeli na inanyamazia.
Ila ikitokea kila utapeli unapofanyika na makampuni ya simu yanapewa penati ndefu, huu utapeli utakoma.
 
Hii nchi hakuna kitengo kinachofanya kazi yake kwa usahihi, uaminifu na uadilifu. Kila sehemu ni janja janja tu...
Mdogo wangu alipoteza iphone yake, tulifanikiwa kuipata baada ya miezi 2 lakini ilikula karibu laki 2. Polisi wanapenda rushwa sana ndio wafanye kazi, bila hivyo hakuna msaada utapata...
Sasa wizara husika itoe majibu kwa hili. Hatuwezi kuendelea na holelaholela ya namna hii. Ni aibu kwa serikali
 
TCRA kitengo cha cyber security wanachojua ni kukamata watu wanaompinga Raisi tu... Kushughulikia kesi za wizi wa mtandaoni aah... Matapeli wamejaa kila kona sasa hivi, mara watu wa mikopo, mara nafasi jeshini. Na watanzania wengi hawana uelewa wa mambo mengi hivyo kutapeliwa ni rahisi sana.
 
muda mwingine huwa nahisi wana shirikiana nao, kwasababu hakuna Cha maana hao tcra hufanya.
Nimesokia tetesi kua wezi wanafanya editing ya IMEI za simu. Hata kama ni kweli hakuna njia cyber security expert anaweza ku trace back the original IMEI? Nchi za wenzetu ukiibiwa simu ukiripoti na vielelezo mitandao yote inaiblock hiyo IMEI kwa hiyo simu hata ukiweka line nyingine haifanyi kazi.
 
Back
Top Bottom