Hivi hawa watu wa ile pesa tuma kwenye namba hii wanashughulikiwa kweli na mamlaka?

Hivi hawa watu wa ile pesa tuma kwenye namba hii wanashughulikiwa kweli na mamlaka?

Bado napata meseji zao. Sielewi hizi namba wanazotumia kama zimesajiliwa kwa NIDA na alama za vidole wanapata wapi ujasiri wa kutapeli watu maana kuwakamata ni jambo rahisi. Mamlaka husika nataka jibu vinginevyo kazi imewashinda.
Mamlaka yaweza kuwa Iko likizo KUU labda !
 
Wapo maeneo ya bungoni ilala mafao house ukifika unauliza pale chini watu wa ku track simu utaelekezwa ofisi zao sina namba zao kk
Kuna mahali nilisoma suala la ku-track simu ya mtu ni jukumu la jeshi la polisi pekee vinginevyo ni kuvunja sheria. Hii imekaaje. Maana tunapeleka loss reports huko polisi hakuna kinachofanyika!
 
ukiwa mjinga au ukiendekeza tamaa utatapeliwa tu na hakuna wa kumlaumu zaidi ya ujinga wako au tamaa zako
Basi ipitishwe sheria ukitapeliwa maadam hujalazimishwa usiende kuripoti polisi. Kama umeuziwa kitu feki au umetapeliwa DECI au Kalyanda and the like piga kimya. Right???
 
Niliongea na mmoja wa hao vijana alichonijibu nikasema Tanzania hii tusahau maendeleo.
Kila mwajiriwa anawaza pesa tu.
Jamaa nilimchimba biti akasema wao wanashikwa lakini wana pesa nyingi za wajinga hivyo huonga wanaachiwa kisha huendelea na kazi
 
Bado napata meseji zao. Sielewi hizi namba wanazotumia kama zimesajiliwa kwa NIDA na alama za vidole wanapata wapi ujasiri wa kutapeli watu maana kuwakamata ni jambo rahisi. Mamlaka husika nataka jibu vinginevyo kazi imewashinda.
Wanakula na mamlaka,polisi wenyewe matapeli.
Ila Kuna mwaka walisombwa kule Ifakara wakafungwa miaka 60,Kila mmoja
 
Ila hawa jamaa wanabahatisha na wanapata, me juzi nimeponea chupuchupu

Nilimpigia simu mkewangu nyumbani nikamuagiza achukue pesa mahali akamtumie mtu, na nilikuwa na haraka, hivyo nikamwambia atoke awahi kwa wakala halafu namba ya huyo mtu nitamtumia.
Basi kabla hajafika kwa wakala nikawa nishamtumia hiyo namba, akatuma hiyo hela. Lakini dakika chache baada ya kutuma tu, meseji ya majamaa wa tuma kwa namba hii ikaingia kwenye simu yake.

Dah! ya tulipishana kidogo tu
Ndio nasema hawa watu wana teknolojia ya kusoma mawasiliano yako siyo bure. Na hilo linaweza kumvuruga aliyetumiwa ujumbe na kwa haraka zile kama issue ilikuwa ni emergency mfano pesa ya matibabu ya mgonjwa mtu akatumbukia huko kwa tapeli. Sasa watu wanakuja hapa na hoja ya wajinga ndio waliwao. Kuna nyakati zenye stress ambapo akili haifanyi kazi sawasawa.
 
Mamlaka yaweza kuwa Iko likizo KUU labda !
Naamini wahusika wengi wanatusoma. Kama hamtashughulika kukomesha huu wizi msije kutuomba kura. Nendeni makwenu mkalime.
 
Niliongea na mmoja wa hao vijana alichonijibu nikasema Tanzania hii tusahau maendeleo.
Kila mwajiriwa anawaza pesa tu.
Jamaa nilimchimba biti akasema wao wanashikwa lakini wana pesa nyingi za wajinga hivyo huonga wanaachiwa kisha huendelea na kazi
Mauzauza tupu.
 
Waziri na watendaji wako upo hapo? Hata kama ni tetesi fuatilia. Vinginevyo msije kuomba kura zetu maana kazi imewashinda
 
Basi ipitishwe sheria ukitapeliwa maadam hujalazimishwa usiende kuripoti polisi. Kama umeuziwa kitu feki au umetapeliwa DECI au Kalyanda and the like piga kimya. Right???
kama mimi ni polisi halafu unakuja kulia umetapeliwa kwa kuambiwa tuma hela na wewe ukatuma tu kwa usiyemjua nakutia makofi,au kuambiwa weka 50,000 utavuna milioni halafu ukaweka nakutimua,kama umeporwa ,umekabwa,umechukuliwa kwa nguvu nitakusaidia
 
Bado napata meseji zao. Sielewi hizi namba wanazotumia kama zimesajiliwa kwa NIDA na alama za vidole wanapata wapi ujasiri wa kutapeli watu maana kuwakamata ni jambo rahisi. Mamlaka husika nataka jibu vinginevyo kazi imewashinda.
Hivi usipotuma huwa wanachukua kwa nguvu hela kwenye simu?
 
Back
Top Bottom