Kiswahili lugha adhimu kabisa.
Mapendekezo yako ni kwamba kiswahili "kisingekuwepo kabisa", maana kila neno la kiingereza umependekeza kiswahili chake kiwe ni "kiingereza kiswahili". Nadhani sio sawia.
Umependekeza hivi:
1. Tablet ingeitwa tableti.
2. Fridge ingeitwa friji
Kwa mtazamo huo kiswahili kama lugha itakua vipi endapo itajibanza kwenye kiingereza kwenye kila kitu mkuu ?
Neno KISHKWAMBI ni neno mujarab kabisa lisilo na tashwishwi yoyote. Na hiyo ndio ladha halisi ya lugha ya kiswahili.
Karibu