Hivi haya majina ya vitu vipya kwa Kiswahili nani huwa anatunga?

Hivi haya majina ya vitu vipya kwa Kiswahili nani huwa anatunga?

Zamani kabla ya baraza la kiswahili, wazee wetu walikuwa wanasikiliza wazungu wakisema cabbage wao wanasema kabichi.. wazungu wakisema week wao wiki.. ila hawa watu wa baraza kujua kwingi ukimuuliza decorder kwa kiswahili inaitwaje wanaenda ofisini kujitungia tu kisha wanarudi na kisimbusi!..
Wiki ina neno lake la Kiswahili, 'Juma'
 
ivi ni Bakita bhana...
JamiiForums-1639747749.jpg
 
Propera Shafti kuitwa kipopojoka, aiseee
baadae haya maneno mapya yatageuka kigujerati lugha mpya kabisa.
tungeenda humo humo tu mfano, pedeli, habu, ekseli, brekishuu, senta bolti, beringi, kompresa, rejeta, mausi, pointa, aipadi nk. tungojee tugundue vya kwetu ndipo tuvipe majina yetu.
mashine moja ina visehemu elfu na unavipa majina ya ajabu sijui kishtobe, kidhkwambi, kipshkuna dah!
 
Kiswahili lugha adhimu kabisa.

Mapendekezo yako ni kwamba kiswahili "kisingekuwepo kabisa", maana kila neno la kiingereza umependekeza kiswahili chake kiwe ni "kiingereza kiswahili". Nadhani sio sawia.

Umependekeza hivi:
1. Tablet ingeitwa tableti.
2. Fridge ingeitwa friji

Kwa mtazamo huo kiswahili kama lugha itakua vipi endapo itajibanza kwenye kiingereza kwenye kila kitu mkuu ?

Neno KISHKWAMBI ni neno mujarab kabisa lisilo na tashwishwi yoyote. Na hiyo ndio ladha halisi ya lugha ya kiswahili.

Karibu
sawa tu dunia inajongea zaidi kuwa moja na huenda miaka mia ijayo lugha zitajielekeza kuwa moja.
 
Wawe wanashirikisha wadau bana.

Na hata kama hawashirikishi wengine watunge basi majina ama maneno mazuri. Sasa kama hili kishkwambi Yani unaltamka huku umekunja uso. Angalau wangeita tu tableti.

Mengine yanayokera jokofu wangeacha tu friji. Smart phone Eti simu janja. Eti password nywila unabaki kushangaa WTF?! Angalau wangeita tu paswedi.

Nahisi ni wakenya Hawa kwasababu juice eti kinywaji tamu unabaki kukasirika tu afadhali bongo tumekomaa na juisi. Shirikisheni wadau mnapotunga nakuita vitu kwa majina ya ajabu ajabu.

Sijui drones wanaziitaje?
Drones huitwa ndege kipepeo[emoji1652]
 
Kiswahili lugha adhimu kabisa.

Mapendekezo yako ni kwamba kiswahili "kisingekuwepo kabisa", maana kila neno la kiingereza umependekeza kiswahili chake kiwe ni "kiingereza kiswahili". Nadhani sio sawia.

Umependekeza hivi:
1. Tablet ingeitwa tableti.
2. Fridge ingeitwa friji

Kwa mtazamo huo kiswahili kama lugha itakua vipi endapo itajibanza kwenye kiingereza kwenye kila kitu mkuu ?

Neno KISHKWAMBI ni neno mujarab kabisa lisilo na tashwishwi yoyote. Na hiyo ndio ladha halisi ya lugha ya kiswahili.

Karibu
Mkuu nifanyie hisani ya maneno haya:
1> Ukuruba
2>Usufuba
 
Hata hili jina UVIKO_19 nani alitafsiri kutoka COVID_19 yaani Corona Hadi kuita UVIKO_19 vigezo gani walitumia wakati ni gonjwa jipya
Ukiachana na hiyo uliugonjwa wa juzi uliotokea Kusini Lindi mwanzoni walikosa jina ila kwa Sasa wanaita MGUNDA[emoji23]
Covid 19 = Corona Virus Disease-19.

Uviko 19 = Ugonjwa wa Virusi vya Korona 19.

19 ni kwa ajili ya 2019, mwaka ugojwa huu ulipoanza. Corona/Korona ni jina la virus/kirusi kinachosababisha ugonjwa huu.
 
Back
Top Bottom