Hivi haya majina ya vitu vipya kwa Kiswahili nani huwa anatunga?

Hivi haya majina ya vitu vipya kwa Kiswahili nani huwa anatunga?

Wawe wanashirikisha wadau bana.

Na hata kama hawashirikishi wengine watunge basi majina ama maneno mazuri. Sasa kama hili kishkwambi Yani unaltamka huku umekunja uso. Angalau wangeita tu tableti.

Mengine yanayokera jokofu wangeacha tu friji. Smart phone Eti simu janja. Eti password nywila unabaki kushangaa WTF?! Angalau wangeita tu paswedi.

Nahisi ni wakenya Hawa kwasababu juice eti kinywaji tamu unabaki kukasirika tu afadhali bongo tumekomaa na juisi. Shirikisheni wadau mnapotunga nakuita vitu kwa majina ya ajabu ajabu.

Sijui drones wanaziitaje?
Mimi nashauri badala ya kuwa na mabaraza ya Kiswahili kwa kila nchi mfano Tanzania (BAKITA) Tuwe na baraza LA kiswahili linalotumika kwa nchi zinazotumia Kiswahili .Ili Kiswahili kisitofautiane baina ya nchi moja na nyingine mfano Stima Hapo Kenya ni umeme.Mtanzania akienda Kenya akisikia Stima atashangaa hatajua maana.
 
Hata hili jina UVIKO_19 nani alitafsiri kutoka COVID_19 yaani Corona Hadi kuita UVIKO_19 vigezo gani walitumia wakati ni gonjwa jipya
Ukiachana na hiyo uliugonjwa wa juzi uliotokea Kusini Lindi mwanzoni walikosa jina ila kwa Sasa wanaita MGUNDA[emoji23]
 
Hivyo vitu havijatungwa jana ni tangu muda sana ni vile ww hujawahi kusoma kamusi ya kiswahili

Na Baraza la kiswahili ndio lenye jukumu la kutoa maana halisi ya maneno kwa kiswahili sio maamuzi ya mtu mmoja mmoja kama unavyodhani na hakuna neno jipya maneno ni yaapo enzi na enzi ni vile ww hukua unajua maana zake kwa kiswahili
 
Wawe wanashirikisha wadau bana.

Na hata kama hawashirikishi wengine watunge basi majina ama maneno mazuri. Sasa kama hili kishkwambi Yani unaltamka huku umekunja uso. Angalau wangeita tu tableti.

Mengine yanayokera jokofu wangeacha tu friji. Smart phone Eti simu janja. Eti password nywila unabaki kushangaa WTF?! Angalau wangeita tu paswedi.

Nahisi ni wakenya Hawa kwasababu juice eti kinywaji tamu unabaki kukasirika tu afadhali bongo tumekomaa na juisi. Shirikisheni wadau mnapotunga nakuita vitu kwa majina ya ajabu ajabu.

Sijui drones wanaziitaje?
Zamani kabla ya baraza la kiswahili, wazee wetu walikuwa wanasikiliza wazungu wakisema cabbage wao wanasema kabichi.. wazungu wakisema week wao wiki.. ila hawa watu wa baraza kujua kwingi ukimuuliza decorder kwa kiswahili inaitwaje wanaenda ofisini kujitungia tu kisha wanarudi na kisimbusi!..
 
Kiswahili lugha adhimu kabisa.

Mapendekezo yako ni kwamba kiswahili "kisingekuwepo kabisa", maana kila neno la kiingereza umependekeza kiswahili chake kiwe ni "kiingereza kiswahili". Nadhani sio sawia.

Umependekeza hivi:
1. Tablet ingeitwa tableti.
2. Fridge ingeitwa friji

Kwa mtazamo huo kiswahili kama lugha itakua vipi endapo itajibanza kwenye kiingereza kwenye kila kitu mkuu ?

Neno KISHKWAMBI ni neno mujarab kabisa lisilo na tashwishwi yoyote. Na hiyo ndio ladha halisi ya lugha ya kiswahili.

Karibu
Barabara.. asiyetaka aende akatabaruku akalale..
 
Kiswahili cha BAJITA ni kigumu kuliko Kingereza, na kinazidi kuwa kigumu.
 
Wawe wanashirikisha wadau bana.

Na hata kama hawashirikishi wengine watunge basi majina ama maneno mazuri. Sasa kama hili kishkwambi Yani unaltamka huku umekunja uso. Angalau wangeita tu tableti.

Mengine yanayokera jokofu wangeacha tu friji. Smart phone Eti simu janja. Eti password nywila unabaki kushangaa WTF?! Angalau wangeita tu paswedi.

Nahisi ni wakenya Hawa kwasababu juice eti kinywaji tamu unabaki kukasirika tu afadhali bongo tumekomaa na juisi. Shirikisheni wadau mnapotunga nakuita vitu kwa majina ya ajabu ajabu.

Sijui drones wanaziitaje?
Kuna mahali niliona eti iCU (intensive care unit) ni SADARUKI..!
Hivi mouse, (ile ya computer) ni kipanya cha kumpyuta, au?!

Halafu, kuna wanaharakati wa Kiswahili wanataka elimu yoote hadi chuo kikuu iwe Kwa Kiswahili tupu. Hapo ndo tutajua kwa nini hakuna Osama bila madevu🙄
 
taratibu tutazowea tukitilia mkazo,mfano neno lilotiliwa mkazo siku za karibuni ni neno"mubashara"limeshafahamika vyema kiasi mpaka linatumika mitaani hivi sasa.
 
wakenya Hawa kwasababu juice eti kinywaji tamu unabaki kukasirika tu afadhali bongo tumekomaa na juisi. Shirikisheni wadau mnapotunga nakuita vitu kwa majina ya ajabu ajabu. " Kiswahili inaitwa "Sharubati"
 
Zamani kabla ya baraza la kiswahili, wazee wetu walikuwa wanasikiliza wazungu wakisema cabbage wao wanasema kabichi.. wazungu wakisema week wao wiki.. ila hawa watu wa baraza kujua kwingi ukimuuliza decorder kwa kiswahili inaitwaje wanaenda ofisini kujitungia tu kisha wanarudi na kisimbusi!..
Hivi KING'AMUZI na KISIMBUSI ni vitu tofauti?
 
Afadhali waliokuja na jina la kibantu la KISHIKWAMBI kuliko wale wanaolazimisha kiswahili kiwe kiarabu kwa maneno mapya yanayochipukia. Kwa yale yalioathiriwa na ukoloni sawa ila kwa sasa tuna akili timamu

Nilishangaa sana aliyebadili jina la kiingereza lililozoeka la matangazo ya TV hewani kutoka LIVE na kuwa la kiarabu MUBASHARA

Huyo aliyebadili jina lililozoeleka la juice na kuleta neno la kiarabu SHARUBATI🙆‍♀️🙆‍♀️🙆‍♀️
 
Kila mtu anajitungia neno likikubalika na watu wengi ndio linakua neno, kwa mfano kishkwambi hili neno katunga mnyamwezi anaitwa Kishiwa Nkwabi ndio maana tablet akaipa jina kishkwambi, tutaona na kusikia mengi
 
Back
Top Bottom