raraa reree
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 11,504
- 35,520
Sawa 🙏Kila lugha duniani ina maneno mepesi na maneno magumu (Kiswahili, Kilatini, Kigiriki, Kihadzabe, n.k).
Labda muwe na hoja nyingine, ila hii ya kutaka kiswahili kiwe na maneno yote mepesi mepesi (kwa kutohoa toka lugha zingine) mimi sioni kama lina mashiko.
Na ukipenda sana vitu laini laini, tepetepe au ndembendembe, utaanza kuamini hata neno "MFUNGWA" ni gumu mno, utapendekeza watu waliohukumiwa kutumikia adhabu gerezani waitwe "PRIZONA."
Sio sawa.
Kishkwambi daima, Kishkwambi milele.
Aya chukua sharubati glass mbili ntakuja kulipia 🙂