Hivi haya majina ya vitu vipya kwa Kiswahili nani huwa anatunga?

Wiki ina neno lake la Kiswahili, 'Juma'
 
Propera Shafti kuitwa kipopojoka, aiseee
baadae haya maneno mapya yatageuka kigujerati lugha mpya kabisa.
tungeenda humo humo tu mfano, pedeli, habu, ekseli, brekishuu, senta bolti, beringi, kompresa, rejeta, mausi, pointa, aipadi nk. tungojee tugundue vya kwetu ndipo tuvipe majina yetu.
mashine moja ina visehemu elfu na unavipa majina ya ajabu sijui kishtobe, kidhkwambi, kipshkuna dah!
 
sawa tu dunia inajongea zaidi kuwa moja na huenda miaka mia ijayo lugha zitajielekeza kuwa moja.
 
Drones huitwa ndege kipepeo[emoji1652]
 
Mkuu nifanyie hisani ya maneno haya:
1> Ukuruba
2>Usufuba
 
Covid 19 = Corona Virus Disease-19.

Uviko 19 = Ugonjwa wa Virusi vya Korona 19.

19 ni kwa ajili ya 2019, mwaka ugojwa huu ulipoanza. Corona/Korona ni jina la virus/kirusi kinachosababisha ugonjwa huu.
 
Mkuu nifanyie hisani ya maneno haya:
1> Ukuruba
2>Usufuba
Mkuu nimefukunyua lakini sijafanikiwa kupata maana toshelezi ya maneno hayo.

Nimeshindwa kuwa msaada katika hili. Utanisamehe sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…