Hivi hii harufu ya baadhi ya mitaa ya jijini Dar naisikia peke yangu tu?


Hakika kuna Jambo la kufanya
 
Nenda Dodoma ndio utashangaa,yaani mitaro ya maji machafu inatoa balaa halafu kama vile kila kitu kipo sawa,hakuna Mamlaka inayojishughulisha kuondoa hali hiyo,hayo ni baadhi ya maeneo machache tu huenda asilimia kubwa ya mikoa mingine nayo ipo hivyo hivyo pia,nchi yetu kwa kweli bado sana
 
Utakua unaishi karibu na chemba za Hospital moja wapo jijini
 
Ni kweli haujaongopa. Dar inanuka hasa mchana muda wa jua kali. Usiku ni kawaida sana kukuta vifurushi vya "nnya" na chupa za mikojo zimetupwa pembezoni mwa mitaro.
 
Kuna siku Dar iliwahi kuacha kunuka? Ni moja ya Miji ya hovyo kuishi.

Mkiambiwa dhibitini ujenzi holela na kuzaana hovyo hamtaki,komaeni
 
Wivu tu unakusumbua, au umetumwa na mabeberu, Macdm bwana!
 
zamani marehemu Ephraim Kibonde kwenye kipindi cha jahazi alikuwa ana utani wake anaita Dar "jiji kunuka"
 
Wahuni huku wanatembea na kiberiti kimejazwa nyaa(Kama ambavyo ulikua Zamani ukienda hosp. kupima choo unaenda umekiweka kwny kiberiti), kila akisikika handasi anakifunua ananusa full kudindisha,hii harufu ya nyaa itakuja kuwakera lini huko road?
Dah! Wahuni hamuwezekani, nakuona katika uborabwako.
 
Kiduku lilo alioongea sana humu kwamba watu wa Dar wamebanana sijui wanapumuaje watu walimcheka.

Ukikaa nje kwa mda siku unafika Dar utashangaa makelele,wenzetu ukienda sokoni pako na utulivu ,ukiingia zile malls na supermarket kubwa kubwa unakuta mziki tulivu watu wanafanya shopping. Siku ukiingia dar upo kama club inayopigwa miziki zaidi ya 100 tofauti ,hapa mwuza sumu ya mende spika inapiga kelele ,mbele mwuza CD anapiga mziki wake kwa nguvu ,hapa mwuza nyama anapasua mifupa ,kule mwuza sim card anatangaza ,pembeni gari ya promotion ya tigo inapiga mziki ,makonda wanapiga debe ,piki piki na bajazi zinapiga honi na mziki, mno visu naye anachanganya baiskeli. Mwinjilisti naye kashika bible na mic pembeni ya barabara anahubiri . Ili mradi vurugu mtindo mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…