Hivi hii kauli ya "ndio hivyo sasa" ina maana gani ukijibiwa na mke wako

Hivi hii kauli ya "ndio hivyo sasa" ina maana gani ukijibiwa na mke wako

Paul dybala

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2023
Posts
524
Reaction score
2,097
Wakuu, iko hivi:

Wife alikuwa na ratiba ya kwenda saloon, kitu ambacho alilazimisha sana. Sikupenda kumzuia, kwa hiyo nikamuelekeza kuwa atachukua ten kwenye hesabu ya mauzo dukani, lakini ahakikishe anawahi kufunga ili ratiba zingine za nyumbani zisiharibike, maana anapenda sana kupika usiku, na nimeshamkataza mara nyingi kwa kuwa muda huo mtoto anakuwa amechoka na ana njaa. Tulikubaliana hivyo.

Natoka zangu kijiweni saa nne hivi na kufika nyumbani, lakini namkosa mtu yeyote. Nikampigia kujua tatizo ni nini, kwa nini bado yuko saloon ilhali mtoto ni mdogo na kuna mbu?

Akanieleza kuwa alikuta foleni. Nikamjibu, "Kama ulikuta foleni, kulikuwa na ulazima gani wa kusubiri, wakati kesho nayo ni siku na hiyo si kitu cha lazima?"

Akanijibu, "Ndio hivyo sasa..." Wakuu, nilitaka nimfuate saloon nimzibue makofi, lakini akili ikaniambia nimchukue mtoto twende tukale chipsi. Huko nako kukawa na foleni, muda ukaenda hadi saa tano na mtoto hajala.

Kwa jibu lake hilo, nimepata tafsiri kwamba sasa ananiachia nione ninachofaa kufanya. Leo nimepanga, ikifika saa tano na anaanza kuwasha jiko, mimi nitalizima. Hapa hakuna kupika usiku huu; hii tabia lazima iishe. Mtu anakuwa na muda mwingi wa kujivuta, mpaka asukumwe ndio afanye kitu. Anapofungua duka saa moja, badala ya kuwahi, utaona anaanza na nguo chafu huku biashara haijaendelea. Huyu dawa yake inachemka, tuone kama atapata hata hela ya vocha. Nimepanga nimtafute chalii kutoka mkoa, anunue kitololi ili niwe nawasambazia maji mwenyewe huku nikikomaa na boda.
 
Pole sana mkuu. Hawa viumbe huwa wana changamoto sana. Inawezekana ulianza nae kwa mtindo huu wa kumbebisha muda wote ktk kipindi cha mapenzi motomoto. Chakufanya weka mkazo wa utaratibu mpya na uwe unamaanisha ukilasirika. Usimlegezee tena. Sio kichapo lkn
 
😂
FB_IMG_1730567656832.jpg
 
Back
Top Bottom