Hivi hii Tabia ya wanawake (wake zetu) kuacha simu ovyo ni ya wanawake wote ama mimi tu?

Kero inakuja pale una issue ya muhimu inabidi itatulike muda huo halafu unapiga simu inaita hadi inakata. Hii mbaya sana

Pia kutokuwa na mfuko sio sababu maana unaweza kuwa unafua simu ukaiweka mahala penye usalama na ikipigiwa utasikia
Tàtizo mnawaacha na viswaswadu, mnunulie iPhone.
 
Ukiona hivyo na simu yake unaijua password hana mambo mengi ya kuficha ktk simu yake.
 
Hii ndio maana wanaume huwa hatupigi simu mra kwa mara nyumbani mana hampokei.

Sasa ukimuahidi zawadi na isije tabia yake itarudi .Nichangamoto kwakweli
 
Mkuu, ukiona mkeo anapokea simu haraka jua unagongewa,manake atataka kila mala awe na simu mkononi,ili hata huyo hawala yake akimtafta bahati mbaya wewe upo amuwahi kumtuliza kuwa "jamaa yupo" huyo wewe uliyenae anakuonesha indicator kuwa yeye hachepuki na unaweza kushka simu yake wakati na muda wowote kumkagua! Asanaleki,akibadilika utamjua.
 
Mkuu kwa hili kuwa Mpole tu!
Mimi nilishanyosha mikono nikaamua kutulia.
Hata mimi nishalala mika hadi basi.Kuna siku wageni walisubiri wafatwe barabarani kama masaa3 halafu wazazi sasa niliona kama kafanya makusudi.Mi nimekuja kuona simu yangu maana nilikuwa kwenye kikao simu nikaacha ofisini mzee kanitafut kama 4 yeye anajua nikiwa kazini juna muda akipiga nakata simu ila nitamrudia.

Hivyo ilibidi nipigie boda awapeleke japo ni mwendo wa kutembea kwa miguu kama dk saba tu
 
Tatizo la wanaume wengi hawaijui saikolojia ya wanawake ndio maana kila jambo ni kulalamika tu juu ya wanawake kuna mambo ni aibu kuyaandika kwa wanaume wenzio, jitahidi ukue mkuu.
 
Aisee Mimi mpaka sasa namtumia dada wa kazi kiwasiliana na mkewangu. Mtu unapiga simu mara 10 hapokei na yupo nyumbani na simu ipo nyumbani yani mpaka naona kama ananifanyia kusudi. Nikimuuliza anasema nilikua mbali na simu. Nimeamua kumzoea tu sasa nitafanyaje maana habadiliki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…