Hivi hii Tabia ya wanawake (wake zetu) kuacha simu ovyo ni ya wanawake wote ama mimi tu?

Ila mimi kama kuna taarifa ya wageni au maelekezo ya baba najitahidi nisipitwe na call yoyote.Ila kama hakuna maagizo yoyote hunipati ng'oo
 
dah hilo jambo linauma sana mkuu, mimi nimeshachoka mda tu sina la kufanya. Halafu wenyewe wanahisi ni normal situation kabisa hawahisi kama pana tatizo.
 
Muwekee bando la kutosha, pia mchatishe Mara kadhaa kwa siku.
Mkuu huko tumeshatoka kitambo sana ukiweka MB akiwa hana kazi atakaa na kuhakikisha hadi ziishe kabisa ndo anapata akili ya kufanya mambo mengine.Nadhani wewe na kwetu ni tofauti kwanza bando hawezi kukoswa maana ile pesa unayompa ya mahitaji ya familia ata balance hadi ibakie ya bando
 
Simu janja nilimpa baada ya kuona hakuna badiliko maana kuna vitu kwa sasa lazima muwasiliane via whatsap hasa kwa picha ama video.Kwa sasa smart haina mbadala.
 
Mi nauza 120,000 tu
Kumbe tangaza.sasa saa yenyewe anavaa anapoenda kanisani au ana safiri. Nadhani kuna kitu ambacho ninyi mnakiona ni sawa tu lakini mngelikuwa mnafunua mioyo yetu kwa ndani tunavyo kereka mnapotoa sababu hizo mgeacha mara moja!

Kwani unapo pika au kufua huwezi kuiweka mezani au sehemu yoyote iliyo karibu nawe ili ukipigiwa usikie? Inakuaje simu inakuwa mbali kiasi cha kupigiwa hadi mara4 husikii?
 
Hili lina vumilika kwakweli na wengi tumesha kubalaiana nalo maana kila ujanja umegonga mwamba na sababu ni zilezile miaka miaka.
 
Ulivyosema ni sahihi mkuu hata mimi kwenye hela ni hivyohivyo. Hela mara nyingi huwa nazikuta kwenye sofa na yeye anaendelea na shughuli zake na hana habari nilisema sana nikagonja labda atakuja kupoteza nipate sababu ya kumnyima lakini hajawahi mara nyingine unaingia uwani unakuta hela kwenye dirisha.


setensi yako ya mwisho "Nimeamua kuwa mpole tu " ndo jawabu mkuu hakuna namna hata mimi nilishanyanyua mikono juu nikiwa nashida nikipiga mara2 hapokei basi naangalia option nyingine ya kumpata.
 
Senior njia hii bora nitaanza ifanyia kazi. Sema kazi zetu mara nyingine simu unaacha unaingia .........hadi jioni saa12 hujashika simu napo nichangamoto pia. but nitajihidi sana kuitumia hii njia Ahsante sana
 
Watu mna mbinu sana asee. Hii imekaa kibabe lakini ni ya kumnyoosha kabisa.Shukrani
 
Tuko wengi.Mwenyewe alishaongea Hadi basi.Kuna muda hata kama nipo nyumbani anaamua Tu kupiga kwenye kasimu Ka nyumbani kwa sababu muda wote yenyewe inakua sebleni.Yangu kuna muda naikuta kwenye vyombo jikoni."Utaskia dada em nipib"
 
duu hawa viumbe kumbe tabia zinafanana sipati presha tena.
 
Tunajua sana majukumu yenu lakini hii haiwapi uhalali wa kutokupokea simu zetu kwa wakati jamani.Huwa tuna kasirika mno moyoni unatamani umeze mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…